DOKEZO Waathirika wa Mradi wa Rusumo hatujalipwa fidia na Serikali, pia tunalazimishwa kuhama

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wananchi tulioathiriwa na Mradi wa Umeme wa Rusumo Hydroelectric Power Project baada ya busting bado hatujapewa fedha za kuhama ili kupisha mchakato huo wa umeme.

Maafis wa Serikali wanaendelea kutuzungusha huku na kule bila mafanikio.

Serikali Kuu itusaidie maana baadhi ya maafisa wanatuamrisha tutoke kwenye nyumba zetu ili wafanye ukarabati wakati bado pesa za kuhama hatujapewa, huu ni mwaka umeisha tunazungushwa tu.

Nakumbuka aliyekuwa Waziri wa Nishati, January Makamba, Julai 17, 2022 alisema waathirika wote watalipwa fidia Septemba 2022 kwa wakazi 1,041, pia kuna nyumba 304 zitakarabatiwa baada ya kuathirika, lakini baada ya kutoa tamko hilo ukimya umetawala na hakuna kinachoendelea.

Nimeambatanisha na video ambayo inaonesha jinsi Waziri alivyotoa ahadi ambayo haijatekelezeka.

==== =====

Kuhusu Mradi wa Rusumo, soma hapa = Makamba: Mradi wa umeme wa Rusumo hydropower project kukamilika mwezi Novemba 2022
 
Back
Top Bottom