A
Anonymous
Guest
Wilaya ya Kigamboni, Kata ya Kisarawe 2, Mitaa ya Mwasonga, Sharrif na Madege wamelipwa fidia isiyo stahiki na Mwekezaji ambaye ni Kampuni ya Nyati Sand Resources Ltd inayomilikiwa na Strandline Resources ya Australia (84%) na Serikali ya Tanzania (16%).
Awali, Mwaka 2016, wahusika walikuja na mpendekezo hayo ya kutaka kutulipa Sq Meter kwa Shilingi 3,000, lakini baadaye wakareje na kutengeneza mazingira ya vitisho na kuanza kuwalipa Wananchi kati ya Tsh. 1,730 mpaka Tsh. 3,000 kwa Sq Meter.
Walipokuja mara ya pili, pamoja na Wananchi kulalamika na kupeleka malalamiko kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa, Wizara, Bungeni lakini mamlaka zinazohusika zikafumba macho na zimeendelea kufumba macho na kumuacha mwekezaji alipe Wananchi pesa kiduchu kwa fidia ya maeneo yao yaliyochukuliwa kwa ajili ya kupisha mradi wa madini ya mchanga.
Wananchi asilimia 90 wamekubali kulipwa fedha hizo kiduchu kisha wakitakiwa kwenda kujitafutia viwanja wenyewe na kujenga kwa gharama zao wenyewe, waliosalia mpaka sasa ni takribani Asilimia 10 ndio hawajalipwa kwa kuwa wamekataa malipo.
Ukweli ni kuwa sisi wakazi wa Kigamboni tunafahamu thamani ya ardhi yetu, kwani kuna wawekezaji wamekuwa wakilipa Shilingi 30,000 kwa sq metre moja, sasa hii ambayo tunalipwa na mwekezaji haikidhi hata kupata kiwanja na kujenga nyumba sehemu nyingine Dar es Salaam labda uamue kwenda nje ya mjini kabisa.
Tumekuwa tukifuatilia kwa muda mrefu kuwa wanachokifanya si sawa lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.
Baadhi ya wanaosimamia Mradi huo ambao bado haujaanza wanadai Serikali ndio imepanga lakini mwekezaji alikuwa tayari kulipa malipo mazuri.
Viongozi wetu wa Serikali za Mtaa hawana nguvu ya kutengeneza hoja kwa kuwa inavyoonekana ni maagizo kutoka juu.
Miaka ya nyuma Naibu Waziri Mkuu wa sasa, Dotto Biteko akiwa Waziri wa Nishati aliwahi kufika hapa tukamweleza hoja zetu, akawa kimya na hakutupata majibu mpaka leo.
Hiyo inakuonesha kuwa jinsi gani kuna mazingira tata ndio maana hata Serikali za Mtaa hawana ubavu wa kufanya chochote.
Tunaomba Dunia ifahamu kuwa Wananchi waliochuku fedha wamefanya hivyo kwa kuwa wanahofia usalama wao na ambao hawajachukua hatujui nini kitawatokea kwa kuwa mradi haujaanza na kunaonekana kuna mazingira flani ya ‘udalali’.