MWAUWASA: Kulikuwa na hitilafu ya mfumo wa maji Stendi ya Mabasi Nyegezi (Mwanza), huduma imerejea

MWAUWASA: Kulikuwa na hitilafu ya mfumo wa maji Stendi ya Mabasi Nyegezi (Mwanza), huduma imerejea

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
WhatsApp Image 2025-03-25 at 10.31.14_ddb42674.jpg


Stendi ya Mabasi Nyegezi ni moja ya wateja wakubwa wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) na Mamlaka imeweka utaratibu wa kufanya ukaguzi wa huduma na miundombinu yake mara kwa mara.

Palitokea hitilafu katika mfumo wa usambazaji maji kwa muda mfupi mwishoni mwa wiki iliyopita lakini ilirekebishwa na huduma inaendelea kwa sasa.

Ilivyokuwa taarifa ya awali kuhusu Stendi hiyo ~ Vyoo vya Umma katika Stendi ya Nyegezi Mwanza havina maji zaidi ya mwezi

Mamlaka imefanya Mawasiliano na Uongozi wa Stendi ili kuboresha mawasiliano yanayolenga kupeana taarifa kwa haraka mara Hitilafu zinapojitokeza ili kuboresha huduma.

Vivien Temu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
MWAUWASA
 
Heb jamii forum mfanye research swala la maji mwanza mtaona madudu mengi sna msaidie kuripot maana bila kuripot watu wanahangaika sna maji mwanza
 
Jamii forum njooni wenyewe hapa Nyegezi na viunga vyake achaneni na majibu marahisi haya kwa uhai wa watu! Hawa wanajibu kirahisi sana haiwezekani mwezi mzima maji maramoja yakitoka hitilafu why?????

Hi kero imekua sugu alafu wakisemwa Ndo wanakuja hapa kujibu wanaona aibu!

Mwanza kunashida kubwa ya maji hawataki kukiri kunashida gani!
Kuna mitaa nyegezi maji yakitoka kwako nikama dhahabu ya siku Moja mateso mwezi mzima na kitu!

Mnalipwa kwa Kodi zetu Mwauwasa acheni siasa kabisa kwenye maisha ya watu.

Mtu ahangaike kupata chakula ,alipe Kodi ya serekari then aanze kufikiria na maji wakati mmeajiliwa kwa ajaili ya kazi hiyo acheni bwana

Alafu huyu anaejibu amekua akijibu Ili kuisafisha mamlaka hebu atake ofisni aje mitaani aache mzaha kabisa mara kadhaa amekua akitoa majibu marahisi kwa maswali magumu sio sahii kwa maadili ya kazi yake aje mitaani ajionee ndipo ataoe majibu.

(maji yakitoka maramoja yanakatika mwezi mzima ,jibu lao hitilafu)
Mungu anawaona.

Na vijana wenu mtaani wanakiri hawwelewi ....... Jamii forum chunguzeni na njooni mseme hadharani hapa
 
Back
Top Bottom