*TAARIFA KWA UMMA*
*UPUNGUFU WA MAJI KWENYE MAENEO YANAYOPATA MAJI KUPITIA KITUO CHA KONA YA BWIRU*
Tumepokea taarifa kutoka TANESCO, kuwa *Tarehe 25 Juni, 2020 (Alhamisi) kuanzia Saa 2:00 Asubuhi hadi Saa 10:00 Jioni* watakuwa na maboresho ya miundombinu na hivyo watakata umeme kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo eneo la Kituo cha Kusukuma Maji (Booster Station) cha Kona ya Bwiru.
Kufuatia taarifa hiyo ya TANESCO, tunasikitika kuwataarifu wateja wetu wa maeneo ya *Kitangiri, Bwiru, Ibungilo, Kawekamo, Lumala, Kiseke, Nyamanoro, Seleman Nassor, Pasiansi, Mondo, Ilemela na Uwanja wa Ndege* kuwa kutakuwa na upungufu wa maji hadi hapo huduma ya nishati ya umeme itakaporejea kwenye hali yake ya kawaida.
Tunawashauri kutunza maji yatakayotosha katika kipindi hicho ambacho kutakuwa hakuna umeme.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Imetolewa *Tarehe 24 Juni, 2020* na: -
………………………………….
*OFISI YA UHUSIANO*
*MWAUWASA*
_Upatapo taarifa hii, tafadhali mfahamishe na mwingine.
Hizi ndio taarifa zao kila siku