Dereva wa gari lililogonga na kusababisha vifo vya watu sita Mwanza akamatwa

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Oswald Kaijage (39) mkazi wa Buswelu kwa tuhuma za kusababisha ajali katika eneo la Kiseke mkoani humo na kupelekea vifo vya watu 6 na wengine 16 kujeruhiwa

Ajali hiyo ilitokea siku Jumamosi nyakati za asubuhi katika eneo la Kiseke Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza ambapo Dereva huyo akiendesha gari lenye namba za usajili T 476 DZL aliwagonga wananchi waliokuwa wakifanya mazoezi na kusababisha vifo 6 na majeruhi na kisha kukimbia kusikojulikana.

Screenshot 2023-07-24 at 17.47.04.png

Screenshot 2023-07-24 at 17.48.24.png

Pia soma
- Mwanza: Watu 6 wafariki kwa kugongwa na gari wakifanya mazoezi
 
Huyu alitakiwa alivyokimbia pale aende kujisalimisha kituo cha polisi. Na angesema alikimbia ili asiuawe na wananchi wenye hasira kali.

Kwa kufanya hivyo angekuwa walau na urafiki na jeshi la polisi maana asingewasumbua.

Sasa yeye kakimbia anasababisha polisi kutumia resources zao kumsaka, maana yake hapo ashakuwa adui wa polisi na ndugu wa hao watu aliowagonga.

Kazi anayo
 
Back
Top Bottom