Mwanza: Soko la Mlango mmoja lateketea kwa moto

Mwanza: Soko la Mlango mmoja lateketea kwa moto

Mungu tu aingilie kati, hii mikopo sijui tutarejesha vipi
 
Mjinga ni yule mwenye shauku ya kujifunza kwa sababu hajui ...
Mpumbavu ni yule anayejua lipi la kufanya lakini hafanyi ...
Tuko upande upi?
Nafikiri ni upumbavu
Na hili la ujinga naona hatujifunzi pia

Sasa sijui tuna balaa gani
Matukio kama haya yanatokea sehemu tofauti lakini bado yanajirudia kama ya meli na vivuko na mabasi na hili la masoko.

Soko limejengwa miaka kutegemea na wachuuzi na idadi inaongezeka
Soko la wafanya biashara 1000 wanapangwa 5000 kama ya MV
 
Mkuu hao zimamoto ni wa kuonea huruma tu!! Kwani hayo magari waliyonayo kwa pressure ya maji inayotumika, hata dk kumi ni nyingi maji yanaisha, wanatakiwa kuwa na magari mengi, na yenye ujazo mkubwa!! Kuna gari la kuzima moto halimashauri ya jiji walipewa msaada toka ujerumani hadi sasa ni zaidi ya mwaka lipo bandarini, kisa kodi, na wale waliotoa msaada wamekataa kuliilipia kwani wametoa bure, walipie tena kodi?!! Ndio lipo tu lina haribika!!


ccm oyee
 
Ila nimeshangaa yaani jeshi letu la Zimamoto wanaishiwa maji wanarudia tena mengine moto unakolea. Ingependeza wangekuwa angalau magari mawili kiasi kwamba moja likishiwa maji lingine liendelee kuzima

We endelea kushangaa,kama walisitisha zoezi la uokoaji/uopoaji kwa kukosa taa,unategemea nini kwenye janga hili la moto.
 
Duh na maisha yenyewe yalivyo halafu biashara yako inateketea inasikitisha sana. labda serikal itawapa fidia m1.5 wahanga. poleni sana
 
Nafikiri ni upumbavu
Na hili la ujinga naona hatujifunzi pia

Sasa sijui tuna balaa gani
Matukio kama haya yanatokea sehemu tofauti lakini bado yanajirudia kama ya meli na vivuko na mabasi na hili la masoko.

Soko limejengwa miaka kutegemea na wachuuzi na idadi inaongezeka
Soko la wafanya biashara 1000 wanapangwa 5000 kama ya MV

Haya yako planned ili kila mara tuendelee kuwaona wanaotuongoza wanafanya kazi kumbe hakuna kitu kinachofanyika. Tujiulize ...
Ushuru unaotozwa kila siku / mwezi / mwaka fedha zinafanya nini?
 
Wajitahidi kuzima kabla giza halijaingiaa....maana huyo bwana anaogopa Giza kuliko kifo..achelewi kusitisha uzimaji moto paka kesho maana Giza limeingia
 
Ila nimeshangaa yaani jeshi letu la Zimamoto wanaishiwa maji wanarudia tena mengine moto unakolea. Ingependeza wangekuwa angalau magari mawili kiasi kwamba moja likishiwa maji lingine liendelee kuzima

NAHUJA,niwatakie pole sana wale wote wanaogushwa kwa namna moja au nyingine na tukio hili la moto katika soko hilo. Kwa taarifa tuu ni kwamba hayo magari ya zima moto yanakuwa na uwezo mkubwa sana wa ku-pump maji tena kwa pressure kubwa kiasi kwamba ujazo wa tenki la gari husika tena kwa kulinganisha na uwezo wa gari hilo kubeba maji huisha kwa haraka sana. Kwa kifupi hayo magari ni kama pump na si kuwa ni matanki ya maji.

Sehemu za mijini,huwa kunatakiwa kuwe na bomba la maji pamoja na point za kuunganisha mabomba na endapo moto unatokea na hivyo gari la zimatoto linaunganishwa kwenye hiyo sehemu kwa mipira au mabomba ili kuruhusu uzimaji wa moto kwa urahisi kwenye maeneo ya jirani na moto unapotokea.

Nimeona nitoe elimu hii kwasababu watu wengi wanadhani na kulalamikia jeshi la uokoaji na zima moto wakidhani kuwa wanapokuja kuzima moto wanakuwa na maji ya kutosha kuzima moto husika. Isitoshe, siyo kila moto unatakiwa kuzimwa kwa maji na tukumbuke daima tunapofanya ujenzi tukumbuke kuzingatia uwepo wa njia au nafasi kwa ajili ya kuruhusu wazima moto na jeshi la uokoaji kupita hasa sehemu zenye mikusanyiko mikubwa ya watu kama masokoni, nyumba za ibada nk.

Tujifunze kila mara tukio au janga la maafa linapotokea.Tena pia kwa kuchukua pia tahadhari,fikiria moto kama huo ushike nguzo za umeme alafu ziangukie kwenye mapaa ya majumba yenye makazi ya watu. Hali itakuwaje?

Ni mimi,

Mwenzetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom