Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 42,958
- 51,163
La katikati ni makoroboi
Lile soko sikupata kuelewa mipaka ya bidhaa za wauzaji ni kama vile soko zima owner ni mmoja
La katikati ni makoroboi
Mkuu hao zimamoto ni wa kuonea huruma tu!! Kwani hayo magari waliyonayo kwa pressure ya maji inayotumika, hata dk kumi ni nyingi maji yanaisha, wanatakiwa kuwa na magari mengi, na yenye ujazo mkubwa!! Kuna gari la kuzima moto halimashauri ya jiji walipewa msaada toka ujerumani hadi sasa ni zaidi ya mwaka lipo bandarini, kisa kodi, na wale waliotoa msaada wamekataa kuliilipia kwani wametoa bure, walipie tena kodi?!! Ndio lipo tu lina haribika!!Ila nimeshangaa yaani jeshi letu la Zimamoto wanaishiwa maji wanarudia tena mengine moto unakolea. Ingependeza wangekuwa angalau magari mawili kiasi kwamba moja likishiwa maji lingine liendelee kuzima
Eeeeeeh maskini sasa wale waliokuwa wamekopa mitaji bank si ndo mwanzo wa kuuziwa nyumba zao, watoto kushindwa kwenda shule, familia kurudi katika umaskini? Hapo ndo unajua suala la kuwa insured ni muhimu sana japokuwa kwa mazingira ya kitanzania ni wachache wanaojali suala hili.Soko la Mlango mmoja jijini Mwanza linateketea kwa moto muda huu na jitihada za kuudhibiti zinaendelea chini ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, amethibitisha kutokea kwa moto huo huku akisema bado chanzo cha moto hakijafahamika lakini hapo baadaye atatolea maelezo.
Mkuu, kumbe wewe ni jirani yangu?Yaani mie mwenyewe nimepita panatisha. Wamefunga barabara ya kukatisha hapo.
Sehemu muhuimu sana Mwanza ya kujipatia viatu bomba vya mitumba, washkaji watakuwa wamepata hasara sana.Yaani nimeangalia huo moto, nimewahurumia sana. hili soko ni kama vile huko Dar pale wanapoita MCHIKICHINI - KARUME
Round hii mwanza kumekucha walah!.Soko la Mlango mmoja jijini Mwanza linateketea kwa moto muda huu na jitihada za kuudhibiti zinaendelea chini ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, amethibitisha kutokea kwa moto huo huku akisema bado chanzo cha moto hakijafahamika lakini hapo baadaye atatolea maelezo.
Yaani mie mwenyewe nimepita panatisha. Wamefunga barabara ya kukatisha hapo.
Chanzo cha moto sikijui lakini nilikua kati ya watu waliofika mwanzo kabisa kwenye zoezi la uokoaji.Chanzo cha huo moto ni nini!?
Napajua sana pale, ni pafinyu sana. Ni wakati sasa wa kutengeneza jengo lililoimara kushinda yaliyopo kwa sasa maana ni ngumu hata kwa zimamoto kuingia pale. Pole kwa waathirika(wenye maduka).Chanzo cha moto sikijui lakini nilikua kati ya watu waliofika mwanzo kabisa kwenye zoezi la uokoaji.
Nilichokiona, Tanesco, zimamoto na ffu waliwahi eneo la tukio na muda waliofika wangeweza kuokoa na kuuzuia moto usisambae.
Gari ya zimamoto na police zilishindwa kuingia ndani ya soko kwasababu hakuna barabara ya gari kupita. Njia zilizopo ni za waenda kwa miguu tena kupishana kwa shida.
Niliona mabomba mawili ya maji tena yalikua na pressure ndogo sana ikabidi watu wawe wanachota maji mtoni.
Kwa anayepafahamu, mule katikati ya soko kuna mtaro mkubwa wa maji, maduka ya kuanzia pale kwenye mtaro kuja upande wa mjini kati, yote yameteketea. Kwa upande huo yaliyosalimika ni yale yanayopakana na hotel za CBE.
Ukiwa na ofisi na umeajiri watu, jitahidi wasaidizi wako waione ofisi yako kama yao. Kuna vijana tulikuanao mwanzo kwenye zoezi la uokoa lakini kabla moto haujafika kwenye duka la bosi wao, walisema tunaogopa kuvunja makufuli kwasababu bosi ni mkali sana. tumempigia simu kasema tumsubiri yupo njiani anakuja. Bosi kafika anakuta moto upo juu ya paa. Kufungua mlango akakutana na moshi na hakuweza kuingia ndani kuokoa kitu hata kimoja.
Soko la mlango mmoja barabara hakuna lakini hakuna tahadhari ya kujikinga na majanga ya moto.
Ila sio kwa avatar hii mkuu
Poleni sana Nah. Naona mwezi huu majanga yamewaandamaYaani mie mwenyewe nimepita panatisha. Wamefunga barabara ya kukatisha hapo.
Poleni sana Sokoro, Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu mnachopitia. Utakuta kuna mtu kapoteza mpendwa wake kwenye ajali ya MV NYERERE na leo tena kapoteza mali yake hapo sokoni!Kumbe uko mwanza, na mimi nimepita hapo asubuhi nikaona hilo janga baya likiteketeza mali za watu. Inauma sana maana litakuwa limewaumiza kiuchumi pia.
Binafs nakisubiru kwa hamu sanaSijui hapo Mwanza wamemkosea nini Mungu,wiki panton kuzama,wiki solo chali,nafikiri bado kifuatacho kinanyemelea kwa kishindo kikubwa sana.