Mwanza inarudi nyuma huku Arusha ikiendelea

Angalia hizo figure za Tanga 2007, 2008, 2009, 2010

Halafu kitu kingine kwa vigezo vyako basi Arusha ni ya nne inazidiwa na hiyo mikoa mitatu hapo juu...
Mkuu unaongelea 2010 kushuka chini?? Mbona hutaki kuongelea 2010 kupanda juu??

Arusha kuzidiwa per capita na Iringa na Kilimanjaro hilo silibishii.. Kilimanjaro mpaka vijijini wanaishi vizuri sana.. Mimi binafsi kijijini kwangu sasahivi mpaka gesi inauzwa na watu walishaachana na kupikia kuni.. Kwahiyo ukiniambia Kilimanjaro inaizidi Arusha kwa kipato cha mmoja mmoja sina cha kubisha sababu vijiji vya wachagga huwezi kuvilinganisha na vya umasaini..
 
Dar es salaam ina vyanzo vingi kuna bandari, kuna viwanda vingi pia kuna baadhi ya mambo yanafanyika Dar es salaam mapato yanaingia Dar, hata ule uwanja wa ndege unaingiza sana mapato...

Pia Dar es salaam kutokana na "centralization of power" mambo mengi yanafanyika huko, sasa kama asilimia kama 80 ya mapato yanatoka Dar maana nilisikia wakiongea hivyo, yaani uchukue mikoa kama ishirini ujumlishe haifikii Dar es salaam...

Sasa chukua pato lote la Dar es salaam ugawanye kwa watu kama milioni nne wa huko, bado itaonekana watu wana kipato kikubwa kulingana na vyanzo, lakini huko ndio slum zimejaa sana kila sehemu...
Hapo tupo sawa, lakini je kama watu million 2 wa Mwanza wangefanya kazi za kiuchumi sawasawa, ziwa lingetumika vizuri na fursa ya kuwa Jiji ambalo lingeweza kuunganisha nchi zote za maziwa makuu mnadhani mngekuwa wapi leo?? Hivi unajua Shinyanga inanyanyuliwa na ile economic junction iliyopo Kahama?? Wafanyabiashara wengi wa Mwanza wamekimbilia Kahama ambako ndio wanaona wanafanya biashara vizuri.. Na ndio maana hata ukusanyaji wa mapato kwa Mwanza bado ni tatizo maana fursa na rasilimali watu mliyonayo hamuitumii kisawa sawa..
 
ACHENI KUSHAMBULIANA KWA MANENO MAKALI,MIJI YOTE NI YETU WATANZANIA NA TUKO HURU KUISHI POPOTE HATUHITAJI PASSPORT.JADILINI KWA MISINGI ISIYOTUGAWA KIKANDA,KIKABILA,KIDINI N.K.
 
Mkuu unaongelea 2010 kushuka chini?? Mbona hutaki kuongelea 2010 kupanda juu??

Arusha kuzidiwa per capita na Iringa na Kilimanjaro hilo silibishii.. Kilimanjaro mpaka vijijini wanaishi vizuri sana.. Mimi binafsi kijijini kwangu sasahivi mpaka gesi inauzwa na watu walishaachana na kupikia kuni.. Kwahiyo ukiniambia Kilimanjaro inaizidi Arusha kwa kipato cha mmoja mmoja sina cha kubisha sababu vijiji vya wachagga huwezi kuvilinganisha na vya umasaini..
Na mimi hapo sina cha kubisha, lakini utakaponiambia Arusha ni maskini zaidi ya Iringa hapo nitabisha...

Mfano ukichukua 2000 ukigawa kwa 20 unapata 100, lakini ukichukua 1000 ukagawa kwa 5 unapata 200

hapo unaweza ukahitimisha chaguo la pili ni zuri wakati hujaangalia vigezo vingine...
 
Mkuu binafsi sijawahi kufika Iringa kwahiyo siwezi kuongea sana hapa..

Lakini kumbuka tu Iringa imeizidi Arusha kwa population kwahiyo GDP per capita ya Iringa ni kubwa zaidi ya Arusha si kwasababu ya uchache wa watu... Iringa wanalima sana na kilimo kwao kinawalipa vizuri. Hii ndio maana hata Ruvuma maisha yanaonekana ni mazuri kuliko hata ya Mwanza.. Kilimo Kilimo Kilimo..
 
Ipo namna hii, idadi ya watu Mwanza ni kubwa ukichukua lile pato lote ukagawanya kwa idadi ya watu inaonekana kipato cha mtu mmoja mmoja ni maskini...

Lakini sio kwamba ipo chini unaposema kuikamata sijui ni kiaje...?! Ila kwa rank ya serikali ipo namba mbili baada ya Dar es salaam...
Huo ni uongo! Hesabu haziwi hivyo. Idadi ya watu wakiwa na pesa wote ukigawanya bado GDP itakua juu. Refer Dar es Salaam. Haijalishi watu ni 1,2,..........n, bado wakiwa na uchumi imara haiwezi kuwa na madhara. Madhara ni pale wengi sana wana uchumi wa kujimudu na wengi sana wako hali mbaya, kadri ilivyo italeta kuwa wale wa hali nzuri wameshindwa kubalance!

Pamoja na uwingi mkubwa wa Watu, bado China iko vizuri kuliko nchi nyingi zenye watu wachache!
 
Hapo tupo sawa, lakini je kama watu million 2 wa Mwanza wangefanya kazi za kiuchumi sawasawa, ziwa lingetumika vizuri na fursa ya kuwa Jiji ambalo lingeweza kuunganisha nchi zote za maziwa makuu mnadhani mngekuwa wapi leo?? Hivi unajua Shinyanga inanyanyuliwa na ile economic junction iliyopo Kahama?? Wafanyabiashara wengi wa Mwanza wamekimbilia Kahama ambako ndio wanaona wanafanya biashara vizuri.. Na ndio maana hata ukusanyaji wa mapato kwa Mwanza bado ni tatizo maana fursa na rasilimali watu mliyonayo hamuitumii kisawa sawa..
Hapo pia inategemea na wanaokusanya mapato, huko kwenye uvuvi unaweza ukakuta wale wavuvi wadogo hawalipi kodi...

Katika sensa ya mwaka 2002 mkoa wa Mwanza ulikuwa ukiongoza kwa idadi ya watu Tanzania ikifuatia Dar es salaam halafu inakuja mikoa mingine ya kanda ya ziwa, Shinyanga na yenyewe ilikuwemo na Kagera, lakini baada ya kuigawanya na kupatikana mikoa ya Geita na Simiyu idadi ya watu imepungua...

Kwa hiyo ilichoisaidia Shinyanga kwa sasa idadi yake ya watu sio kubwa, lakini ukiangalia katika ile ripoti nyingine ya UNDP ilikuwemo, ukijaribu kuchunguza ile mikoa iliyotajwa kuna wananchi maskini zaidi ina idadi kubwa ya watu mfano Mwanza, Kagera na Geita...
 
Huo ni uongo! Hesabu haziwi hivyo. Idadi ya watu wakiwa na pesa wote ukigawanya bado GDP itakua juu. Refer Dar es Salaam. Haijalishi watu ni 1,2,..........n, bado wakiwa na uchumi imara haiwezi kuwa na madhara. Madhara ni pale wengi sana wana uchumi wa kujimudu na wengi sana wako hali mbaya, kadri ilivyo italeta kuwa wale wa hali nzuri wameshindwa kubalance!

Pamoja na uwingi mkubwa wa Watu, bado China iko vizuri kuliko nchi nyingi zenye watu wachache!
Nadhani umenisaidia kumuelewesha mkuu... Asante sana.
 
Huo ni uongo! Hesabu haziwi hivyo. Idadi ya watu wakiwa na pesa wote ukigawanya bado GDP itakua juu. Refer Dar es Salaam. Haijalishi watu ni 1,2,..........n, bado wakiwa na uchumi imara haiwezi kuwa na madhara. Madhara ni pale wengi sana wana uchumi wa kujimudu na wengi sana wako hali mbaya, kadri ilivyo italeta kuwa wale wa hali nzuri wameshindwa kubalance!

Pamoja na uwingi mkubwa wa Watu, bado China iko vizuri kuliko nchi nyingi zenye watu wachache!
Kwa case ya Dar es salaam nimeeleza jaribu kuangalia, halafu si kweli ya kwamba Dar es salaam watu wote wana pesa na maisha mazuri...

Idadi kubwa tu watu wamechoka...
 
Hapo pia inategemea na wanaokusanya mapato, huko kwenye uvuvi unaweza ukakuta wale wavuvi wadogo hawalipi kodi...

Katika sensa ya mwaka 2002 mkoa wa Mwanza ulikuwa ukiongoza kwa idadi ya watu Tanzania ikifuatia Dar es salaam halafu inakuja mikoa mingine ya kanda ya ziwa, Shinyanga na yenyewe ilikuwemo na Kagera, lakini baada ya kuigawanya na kupatikana mikoa ya Geita na Simiyu idadi ya watu imepungua...

Kwa hiyo ilichoisaidia Shinyanga kwa sasa idadi yake ya watu sio kubwa, lakini ukiangalia katika ile ripoti nyingine ya UNDP ilikuwemo, ukijaribu kuchunguza ile mikoa iliyotajwa kuna wananchi maskini zaidi ina idadi kubwa ya watu mfano Mwanza, Kagera na Geita...
Mkuu unafikiri hata Arusha wauzaji wadogo wa madini wanalipa kodi?? Mtu anatoka na Tanzanite yake anaingia Nairobi anavuta pesa yake anarudi Arusha.. Ndio maana ikaonekana Tanzanite inauzwa zaidi nje Kenya kuliko Tanzania..

Idadi ya watu itakakiwa iwe nyenzo muhimu ya kuharakisha kipato cha watu wa eneo husika na sio kufanya kipato kishuke kama unavyosema. Unafikiri Dar ingekuwa na watu Million 1 ingekuwa kama hivyo ilivyo?? Dar Kinondoni pekee au Sinza pekee inaweza ikawa imebeba watu wa wilaya nzima wa wilaya flani.. Sasa hapo biashara lazima ifanyike, circulation ya pesa inakuwa juu na ndivyo hivyo hivyo TRA inajikusanyia chake. Sinza kila baada ya nyumba mbili kuna Bar, zile Bar za Sinza tu nina hakika zinakusanya kodi TRA zaidi ya hata Wilaya yote kwa ujumla ya mikoa fulani..

Kwahiyo population ya kanda ya ziwa ilitakiwa iwe nyenzo ya mzunguko mkubwa wa pesa na ufanyaji wa biashara na sio kutafutia excuse kama hizi unazotoa.. Kwenye uchumi nilisoma Factors of Production ambazo ni Nguvu Kazi (Labour), Ardhi, Mitaji na Ujasiriamali.. Mwanza au Kanda ya Ziwa kwa ujumla mna watu na ardhi lakini mmekosa mitaji na ujasiriamali.. Hilo halina ubishi
 
We jamaa wewe, kwa Dar es salaam si nimekuelezea umeona ni sawa...
Mkuu Dar si umekubali wana vyanzo vingi vya mapato au ulitaka nibishe?? Au wewe unabisha kwamba Dar hakuna maisha mazuri kulinganisha na wapi.. Mimi nilichoelewa ni kwamba umekubali Dar iko mbele
 
Kwa case ya Dar es salaam nimeeleza jaribu kuangalia, halafu si kweli ya kwamba Dar es salaam watu wote wana pesa na maisha mazuri...

Idadi kubwa tu watu wamechoka...
Ni kweli mkuu wapo wengi wamechoka Dar, ni kweli. Pia ni kweli wapo wengi matajiri Mwanza ni kweli. Inapokuja suala la Takwimu, haiwi kama unavyotaka wewe mkuu!
Tufanye hivi:-
1. Dar es Salaam watu 7
2. Mwanza watu 5
3. Arusha watu 4
4. Ruvuma watu 4.

Kama Dar watu wana Tsh 500,600,700,800,900,1000 na 1100(mfano)
Mwanza: 700,900,400,200,100
Arusha: 600,500,800,1000
Ruvuma:400,500,750,600

Na ikiwa ili mkoa uonekane una maisha duni kipato cha mkazi wake kiwe ni chini ya Tsh 575 kwa siku.

Ni dhahiri Mwanza itakuwa ni maskini kwa muktadha wa jaribio hilo, ingawa wapo watu wana pesa kama hizo Tsh 900 nk. Huu ni mfano mwepesi ambao siyo rasmi ila unajaribu kureflect jinsi gani inawezwa kutajwa kuwa sehemu fulani kuna maisha duni!
 
Mkuu unafikiri hata Arusha wauzaji wadogo wa madini wanalipa kodi?? Mtu anatoka na Tanzanite yake anaingia Nairobi anavuta pesa yake anarudi Arusha.. Ndio maana ikaonekana Tanzanite inauzwa zaidi nje Kenya kuliko Tanzania..

Idadi ya watu itakakiwa iwe nyenzo muhimu ya kuharakisha kipato cha watu wa eneo husika na sio kufanya kipato kishuke kama unavyosema. Unafikiri Dar ingekuwa na watu Million 1 ingekuwa kama hivyo ilivyo?? Dar Kinondoni pekee au Sinza pekee inaweza ikawa imebeba watu wa wilaya nzima wa wilaya flani.. Sasa hapo biashara lazima ifanyike, circulation ya pesa inakuwa juu na ndivyo hivyo hivyo TRA inajikusanyia chake. Sinza kila baada ya nyumba mbili kuna Bar, zile Bar za Sinza tu nina hakika zinakusanya kodi TRA zaidi ya hata Wilaya yote kwa ujumla ya mikoa fulani..

Kwahiyo population ya kanda ya ziwa ilitakiwa iwe nyenzo ya mzunguko mkubwa wa pesa na ufanyaji wa biashara na sio kutafutia excuse kama hizi unazotoa.. Kwenye uchumi nilisoma Factors of Production ambazo ni Nguvu Kazi (Labour), Ardhi, Mitaji na Ujasiriamali.. Mwanza au Kanda ya Ziwa kwa ujumla mna watu na ardhi lakini mmekosa mitaji na ujasiriamali.. Hilo halina ubishi
Okay sawa... basi inatakiwa wawezeshwe sasa...
Mkoa hauna tatizo ila ni watu wana tatizo, miundombinu ipo...
 
Mkuu Dar si umekubali wana vyanzo vingi vya mapato au ulitaka nibishe?? Au wewe unabisha kwamba Dar hakuna maisha mazuri kulinganisha na wapi.. Mimi nilichoelewa ni kwamba umekubali Dar iko mbele
Nilikutolea mfano ukichukua mikoa kama ishirini jumlisha mapato yake haifiki kwa Dar ukikokotoa yale mapato gawanya kwa idadi ya watu karibia wote wataonekana mambo safi...

Wizara ya fedha ukisoma ile taarifa ime base kwa sensa ya mwaka 2012, ndio maana wakasema mikoa yenye unafuu ya umaskini kwa Dar wakatoa kama asilimia 4 kama nakumbuka vizuri, yaani kwa kifupi ile idadi ya watu milioni 4 ni asilimia nne tu ndio maskini, yaani kwa makadirio ni watu kama laki moja na sitini elfu ndio maskini...

Je kwa uhalisia hiyo ni kweli...?!
 
Ni kweli mkuu wapo wengi wamechoka Dar, ni kweli. Pia ni kweli wapo wengi matajiri Mwanza ni kweli. Inapokuja suala la Takwimu, haiwi kama unavyotaka wewe mkuu!
Tufanye hivi:-
1. Dar es Salaam watu 7
2. Mwanza watu 5
3. Arusha watu 4
4. Ruvuma watu 4.

Kama Dar watu wana Tsh 500,600,700,800,900,1000 na 1100(mfano)
Mwanza: 700,900,400,200,100
Arusha: 600,500,800,1000
Ruvuma:400,500,750,600

Na ikiwa ili mkoa uonekane una maisha duni kipato cha mkazi wake kiwe ni chini ya Tsh 575 kwa siku.

Ni dhahiri Mwanza itakuwa ni maskini kwa muktadha wa jaribio hilo, ingawa wapo watu wana pesa kama hizo Tsh 900 nk. Huu ni mfano mwepesi ambao siyo rasmi ila unajaribu kureflect jinsi gani inawezwa kutajwa kuwa sehemu fulani kuna maisha duni!
Kwa hizo hesabu zako inakuwa kana kwamba walihoji kila mmoja ana kipato gani, je ni kweli walifanya hivyo...?! Nilisoma kwenye magazeti zile takwimu za wizara ya fedha zilitokana na sensa ya mwaka 2012, je walikokotoa kwa mtindo upi...?!

Au walikuwa wakihoji...?!
 
Nilikutolea mfano ukichukua mikoa kama ishirini jumlisha mapato yake haifiki kwa Dar ukikokotoa yale mapato gawanya kwa idadi ya watu karibia wote wataonekana mambo safi...

Wizara ya fedha ukisoma ile taarifa ime base kwa sensa ya mwaka 2012, ndio maana wakasema mikoa yenye unafuu ya umaskini kwa Dar wakatoa kama asilimia 4 kama nakumbuka vizuri, yaani kwa kifupi ile idadi ya watu milioni 4 ni asilimia nne tu ndio maskini, yaani kwa makadirio ni watu kama laki moja na sitini elfu ndio maskini...

Je kwa uhalisia hiyo ni kweli...?!
Mkuu hizi ni kama hesabu za wastani tu... Na takwimu za kiuchumi ndio vilivyo kila mahali..

Usishangae ya Dar kuwa 4% tu ndio maskini, shangaa Tanzania maskini ni 28% tu... Je hiyo ni kweli??

Data za kiuchumi zinachukuliwa collectively na sio personally...
 
Back
Top Bottom