Woh! hiyo picha ya kwanza ni hotel ya nssf, hapa nssf nimewavulia kofia! zamani hapa lilikuwa josho la mbwa, kuna watu waliandamana hadi kwa RC wakipinga kuondolewa kwa josho hilo eti mbwa wao watapata ukurutu.
picha ya tatu ni shopers plaza ya ppf, hili jengo lina car park ya gorofa tano ukitaka kudrive hadi juu sawa au vipi unalipandisha kwa lift maalumu. nyuma yake kuna ka libraly koko, nadhani katafutiwe sehemu nyingine tulivu.
funiko itakuwa hiyo hotel ya moil inayotegemewa kujengwa pale uwanja wa nyamagana. Hotel hii itakuwa na hadhi ya nyota tano na vyumba 300. viwanja vya long tenis, busket ball, budminton, squash na gim. kwa ujumla indoor games zote zitakuwepo. Sio Movenpik kama wewe sio mlevi utaboreka zaidi ya vinywaji hakuna cha ziada.
Hiyo picha ya pili niwafanyakazi wa budege sijui hii kampuni ni ya kinjeketile, angekuwa mwingine angekwisha fukuzwa siku nyingi.
mwanza airport itakuwa international airport sio muda mrefu, ndo itakuwa mwisho wa ATC kwenda mwanza kwani abiria wengi niwafanyabiashara wanaokwenda zao Dubai na hongkong.