Kabisa Mimi naikumbuka Nyegezi,. Na Mapuya yake pale Luchelele. Na watoto dogodogo pale Nganza. Na Wazee wasiojua kucheza "disco music" pale Buhemba- Ehh. I love u Mwanza.beautiful Mwanza,
lazima siku moja na mimi nifike huko!!
Taka za nini tena hapo ... umaharibu bwana ..... other wise very coool indeed
Mwanakijiji do you see??
Mji wa Mwanza umezungukwa na milima ya mawe, milima ya almasi, milima ya dhahabu, maji baridi, na samaki watamu
Mwanza Oooh Mwanza
-Remmy Ongala
Unajua Kibunango umekuwa kama clairvoyant vile, Mwanza was on my mind leo hii.Nilikuwa nasema ingekuwa safi sana kama mtu anaenda bongo halafu ana skip hustle and bustle ya Dar na kwenda Mwanza. Previously I had the same thoughts about Tanga, kuna vibe tofauti na noxious Dar.
absolutely... ningependa picha ya kona ya kwenda Isamilo pale kwenye kibanda cha kuuza kanda kwenye "I turn, U turn we all turn to U turn"...
Picha hii najaribu kuonyesha maisha ya kila siku ya Waakazi wa Mwanza, Hapo kuna mfanyakazi wa CBO yupo busy na simu yake, wengine wamesimama huku kuna taka rukuki chini ambazo zinatakiwa kuwa ndani ya kontena...
Pembeni kuna mtu anatafuta chupa za maji zilizotumika kwa ajili ya kuzirecycle, Iwapo wakaazi wa Mwanza wangekuwa wanatenganisha taka, wangeweza kulicycle chupa za maji na kijipatia kipato, aidha wangeweza kureuse baadhi ya taka na kubana matumizi, muhimu zaidi wangepunguza taka wanazotupa kwenye majaa. Taka za jikoni ni rasilimali tosha kwa mbolea ya Mboji, hivyo basi kama taka zote za jikoni kasoro majivu zingekuwa zinatumika katika kutengeneza mbolea, ni taka chache sana ambazo zingekuwa zinatupwa na kufika jaa kuu la Buhongwa..