mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 96,479
- 138,343
Labda walimuambia lala chini jamaa akagoma akaendelea kuonesha viashiria labda ana silahaJeshi la polisi linasikitisha sana! Sasa mtu kama huyo usikute ana changamoto ya afya ya akili, teja au ana msongo wa mawazo! Kulikuwa kuna ugumu gani wa kumkamata kwa njia ya kawaida?
Mtu hana silaha! Unampiga risasi ya kiunoni kwa sababu gani? Eti alikataa kujisalimisha! Alikuwa anakimbia? Sasa mtu yuko kwenye kizimba cha mtoa huduma, si lilikuwa ni jambo la kumkamata tu na kwenda kumhoji kituoni!
Kwa nini hili jeshi linaamini sana kwenye matumizi makubwa ya nguvu, huku askari wake wakitumia akili kidogo kwenye kutatua matatizo ya msingi? Ndiyo kusema uhai wa binadamu hauna kabisa thamani kwenye hii nchi? Kwa nini wameamua kujipa jukumu la kuwa watoa hukumu badala ya mahakama?
Sitetei uhalifu! Ila siamini kama nguvu iliyotumika inaendana na tukio lenyewe.
Au maaskari waliogopa kupigwa kama yule askari mwenzao wa usalama barabarani?
Ova