Mwanza: Apigwa risasi baada ya kujaribu kupora bank

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limesema Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 hadi 35 amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na Polisi, akidaiwa kuingia katika Benki iliyopo Rock City Mall, Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, tukio hilo limetokea Septemba 13, 2026, saa 7 mchana ambapo Mwanaume huyo ambaye utambulisho wake bado haujafahamika, anadaiwa kuingia benki kama Mteja na kumtaka Mhudumu ampatie fedha ya kula.

Polisi imesema baada ya Mhudumu kujaribu kumpa utaratibu wa kutoa na kuweka fedha, Mwanaume huyo aliendelea kusisitiza apewe fedha, hali iliyomfanya Mhudumu kuhisi hatari na kwenda kwa Wafanyakazi wenzake kutafuta msaada.

Inadaiwa Mwanaume huyo aliruka kaunta na kuelekea kwenye vyumba vya kuhesabia fedha, akamsukuma Mhudumu na kuingia naye ndani, hali iliyozua taharuki kwa Wafanyakazi na Wateja ambapo Askari waliokuwa wakitoa ulinzi katika benki hiyo walifika na kumtaka ajisalimishe, lakini kwa mujibu wa Polisi, alikaidi amri hiyo na akitaka kuwanyang’anya silaha.

Polisi imesema Askari walimdhibiti kwa kumpiga risasi kiunoni upande wa mguu wa kulia na kusababisha jeraha lililovuja damu nyingi ambapo alibainika kuwa amefariki dunia wakati akikimbizwa Hospitalini.

View attachment 3670492
Mtu mmoja anawaagiza kudhibiti Bank imejaa watu na walinzi na wahudumu mpaka wamuue kwa Riaasi?

Kirang njoo uone Tz hakuna anayejali uhai wa mtu.

Huyo ni Teja alikuwa na njaa na arosto ya pesa, Maana hata mwizi hawezi kufanya hayo
 
Yaani mtu amerukaje akaingia ndani ya counter wakati bank zote zina vioo na vitundu vidogo. Ni bank gani iliyowazi kiasi hicho mpaka mtu arukie ndani.
Unampigaje mtu risasi na hana silaha au unawezaje kumnyang'anya askari silaha na yeye yko ndani ya counter.
Pale mall kuna askari wengi sana pamoja na suma jkt. Inakuwaje watu wote hao kushindwa kumdhibiti mtu mmoja ambaye tena yuko ndani mpaka watumie risasi.
Hii ndio comment yangu pia,haijakaa sawa kwenye kuruka counter na kuomba pesa ya kula !
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limesema Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 hadi 35 amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na Polisi, akidaiwa kuingia katika Benki iliyopo Rock City Mall, Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, tukio hilo limetokea Septemba 13, 2026, saa 7 mchana ambapo Mwanaume huyo ambaye utambulisho wake bado haujafahamika, anadaiwa kuingia benki kama Mteja na kumtaka Mhudumu ampatie fedha ya kula.

Polisi imesema baada ya Mhudumu kujaribu kumpa utaratibu wa kutoa na kuweka fedha, Mwanaume huyo aliendelea kusisitiza apewe fedha, hali iliyomfanya Mhudumu kuhisi hatari na kwenda kwa Wafanyakazi wenzake kutafuta msaada.

Inadaiwa Mwanaume huyo aliruka kaunta na kuelekea kwenye vyumba vya kuhesabia fedha, akamsukuma Mhudumu na kuingia naye ndani, hali iliyozua taharuki kwa Wafanyakazi na Wateja ambapo Askari waliokuwa wakitoa ulinzi katika benki hiyo walifika na kumtaka ajisalimishe, lakini kwa mujibu wa Polisi, alikaidi amri hiyo na akitaka kuwanyang’anya silaha.

Polisi imesema Askari walimdhibiti kwa kumpiga risasi kiunoni upande wa mguu wa kulia na kusababisha jeraha lililovuja damu nyingi ambapo alibainika kuwa amefariki dunia wakati akikimbizwa Hospitalini.

View attachment 3670492
Maelezo ya habari hii ina mapungufu, Polisi walitumia nguvu kupita kiasi na kuua omba omba!
Ningelisimama na Polisi iwapo omba omba huyo angelikuwa na silaha.
Polisi hawajatumia weledi kumdhibiti mtuhumiwa.
 
Kwa maelezo hayo mliyotoa huyo sio mwizi wala sio jambazi bali ni mtu aliyerukwa na akili.
Hakuna mwizi aje kizembe hivyo kwa kujionyesha waziwazi na mkononi hana silaha.
Nasikitika sijui kwa nini imetumika nguvu kubwa mno kumdhibiti mtu kama huyo ambaye ilitakiwa afungwe kamba tu na kupelekwa hospitali
 
Yaani mtu amerukaje akaingia ndani ya counter wakati bank zote zina vioo na vitundu vidogo. Ni bank gani iliyowazi kiasi hicho mpaka mtu arukie ndani.
Unampigaje mtu risasi na hana silaha au unawezaje kumnyang'anya askari silaha na yeye yko ndani ya counter.
Pale mall kuna askari wengi sana pamoja na suma jkt. Inakuwaje watu wote hao kushindwa kumdhibiti mtu mmoja ambaye tena yuko ndani mpaka watumie risasi.
Excuse yao ndio hio 'alitaka kumnyqng'anya askari silaha' hawa polisi wetu hovyo sana.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limesema Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 hadi 35 amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na Polisi, akidaiwa kuingia katika Benki iliyopo Rock City Mall, Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, tukio hilo limetokea Septemba 13, 2026, saa 7 mchana ambapo Mwanaume huyo ambaye utambulisho wake bado haujafahamika, anadaiwa kuingia benki kama Mteja na kumtaka Mhudumu ampatie fedha ya kula.

Polisi imesema baada ya Mhudumu kujaribu kumpa utaratibu wa kutoa na kuweka fedha, Mwanaume huyo aliendelea kusisitiza apewe fedha, hali iliyomfanya Mhudumu kuhisi hatari na kwenda kwa Wafanyakazi wenzake kutafuta msaada.

Inadaiwa Mwanaume huyo aliruka kaunta na kuelekea kwenye vyumba vya kuhesabia fedha, akamsukuma Mhudumu na kuingia naye ndani, hali iliyozua taharuki kwa Wafanyakazi na Wateja ambapo Askari waliokuwa wakitoa ulinzi katika benki hiyo walifika na kumtaka ajisalimishe, lakini kwa mujibu wa Polisi, alikaidi amri hiyo na akitaka kuwanyang’anya silaha.

Polisi imesema Askari walimdhibiti kwa kumpiga risasi kiunoni upande wa mguu wa kulia na kusababisha jeraha lililovuja damu nyingi ambapo alibainika kuwa amefariki dunia wakati akikimbizwa Hospitalini.

View attachment 3670492
Hivi na nyie mnaamini kabisa polisi wa nchi na taarifa zao?
 
Jeshi la polisi linasikitisha sana! Sasa mtu kama huyo usikute ana changamoto ya afya ya akili, teja au ana msongo wa mawazo! Kulikuwa kuna ugumu gani wa kumkamata kwa njia ya kawaida?

Mtu hana silaha! Unampiga risasi ya kiunoni kwa sababu gani? Eti alikataa kujisalimisha! Alikuwa anakimbia? Sasa mtu yuko kwenye kizimba cha mtoa huduma, si lilikuwa ni jambo la kumkamata tu na kwenda kumhoji kituoni!

Kwa nini hili jeshi linaamini sana kwenye matumizi makubwa ya nguvu, huku askari wake wakitumia akili kidogo kwenye kutatua matatizo ya msingi? Ndiyo kusema uhai wa binadamu hauna kabisa thamani kwenye hii nchi? Kwa nini wameamua kujipa jukumu la kuwa watoa hukumu badala ya mahakama?

Sitetei uhalifu! Ila siamini kama nguvu iliyotumika inaendana na tukio lenyewe.
Au maaskari waliogopa kupigwa kama yule askari mwenzao wa usalama barabarani?
 
Back
Top Bottom