Mwanza: Apigwa risasi baada ya kujaribu kupora bank

Huyo atakuwa hana akili timamu ndio wiza gani wa bank huo? Pili hao askari wameshindwa kumthibiti bila kutumia nguvu ya ziada kama alikuwa hana siraha zaidi ya kuwalazimisha cashier wampe pesa tu?!
Spot on! Ndiyo maana huwa tunasema nchi yetu staarabu bado kabisa. Huyú kuna uwezekano atakuwa ni mgonjwa wa akili na polisi walichotakiwa kufanya ni kum- contain. Hakuna jambazi anayepora kwa njia hii.
 
Jeshi la polisi kazi Bure kabisa.

Inamaanisha Askari wa Jeshi la Polisi amekosa mbinu za kumdhibiti Raia asiyekuwa na silaha bila kutumia Bunduki! Hapakuwa na ulazima wa kutumia Bunduki.

Hakuna mhalifu hapo, wameua Raia aliyekuwa na Njaa.

Simpletons!
Police wapo kwenye taharuki asije akapigwa kabari km yule aliepigwa na daktari sasa wakaona nguvu hawana ngoja watumie manati
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limesema Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 hadi 35 amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na Polisi, akidaiwa kuingia katika Benki iliyopo Rock City Mall, Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, tukio hilo limetokea Septemba 13, 2026, saa 7 mchana ambapo Mwanaume huyo ambaye utambulisho wake bado haujafahamika, anadaiwa kuingia benki kama Mteja na kumtaka Mhudumu ampatie fedha ya kula.

Polisi imesema baada ya Mhudumu kujaribu kumpa utaratibu wa kutoa na kuweka fedha, Mwanaume huyo aliendelea kusisitiza apewe fedha, hali iliyomfanya Mhudumu kuhisi hatari na kwenda kwa Wafanyakazi wenzake kutafuta msaada.

Inadaiwa Mwanaume huyo aliruka kaunta na kuelekea kwenye vyumba vya kuhesabia fedha, akamsukuma Mhudumu na kuingia naye ndani, hali iliyozua taharuki kwa Wafanyakazi na Wateja ambapo Askari waliokuwa wakitoa ulinzi katika benki hiyo walifika na kumtaka ajisalimishe, lakini kwa mujibu wa Polisi, alikaidi amri hiyo na akitaka kuwanyang’anya silaha.

Polisi imesema Askari walimdhibiti kwa kumpiga risasi kiunoni upande wa mguu wa kulia na kusababisha jeraha lililovuja damu nyingi ambapo alibainika kuwa amefariki dunia wakati akikimbizwa Hospitalini.

View attachment 3670492
Bank haina hata Jina ? Rock city mall kuna ABSA, Stanbic , NMB...
 
Police wetu hawana akili kabisa. Kumuua chizi asiye na silaha wala uwezo wa kupiga MTU ngumi ni uchizi pia.
 
Nawapongeza polisi kufanya vizuri kazi waliyosomea. Lakini kuna benki ambayo bado mtu anaweza kuruka kaunta na kuingia kwa teller? Siku hizi si wanakaa ndani kwenye vioo vinene na kunakuwa na tundu dogo? Mara ya mwisho kuona uwezekano wa mtu kuingia kwa teller ilikuwa NMB Clock Tower mwaka 2006 kurudi nyuma.
 
Back
Top Bottom