Mwanyasi yuko salama baada ya kupata ajali mbaya.....

Mwanyasi yuko salama baada ya kupata ajali mbaya.....

Habari za siku nyingi ndugu wana MMU,

Napenda kuwashirikisha habari nilizopata muda mfupi uliopita kumhusu mwenzetu Mwanyasi, katibu wetu wa Tanga Wing ambaye alipotea ghafla kwa muda mrefu. Kama mwezi mmoja na nusu uliopita, tulijaribu kumtafuta kwa kila njia lakini hatukumpata. Tulihisi kwamba labda yuko vijijini kikazi na ndiyo maana hapatikani. Leo kanipigia simu na kunipatia habari ambazo zimenisikitisha sana.

Ni kwamba kama mwezi mmoja uliopita, Mwanyasi alipata ajali ya pikipiki na kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo. Alikaa pale kwa muda na madaktari wakampatia rufaa ya kwenda Muhimbili. Wakati huo alikuwa hajitambui na alipopata fahamu kidogo, alikuwa akiongea mambo ambayo hayaeleweki (was halucinating). Muhimbili walimfanyia kipimo cha MRI na kugundua kuwa alikuwa amepasuka mishipa midogo kwenye ubongo na kusababisha damu kuvuja kwenye ubongo (brain haemorrhage). Alipatiwa dawa na kukaa Muhimbili kwa zaidi ya mwezi mmoja, akiwa bado hajitambui. Kwa sasa amepata nafuu na kurudi Tanga.

Nimeongea naye muda mfupi na kustuka sana kwa hili tukio lililompata. Hata hivyo, nimefarijika sana kwamba ndugu yetu yuko mzima na anaendelea vizuri.

Nimemwomba sana Mwanyasi na namshukuru kwa kukubali ombi langu la kuwajulisha ndugu zetu wengine wa JF, wana Tanga Wing, Arusha Wing na wadau wengine ambao walikuwa naye karibu.

Naomba tuzidi kumwombea apone kabisa na kurejea katika shughuli zake.

Babu DC!!

cc: KOKUTONA CHUAKACHARA, YNNAH, PakaJimmy, black womani, Preta, Mzee wa Rula, Filipo, Lily Flower, Smile, gfsonwin, Madame B, watu8, Arusha one, LiverpoolFC, Mungi, Fixed Point, amu, Paloma, Husninyo, Dena Amsi

Nampa pole sana. Mungu ni mwema! Ampe uzima tele na amhimarishe.
 
Wanajamvi nawashukuru sana kwa salaam zenu jamani,
Namshukuru Mungu leo nimeweza kuwapa taarifa hii nikiwa mzima! Nilipoteza ufahamu kwa muda wa mwezi mmoja na wiki 2 hiyo haikuwa rahisi kutoa taaarifa yoyote kwenu ndugu zangu.
Nawaashukuru wote kwa salaam na kunitakia heri, zaidi namshukuru Mungu kwa kuniponya.

Ahsante ndugu zangu wana JF.
 
pole dearest! nitakupigia
 
Mbaya sana hii, lakini unasema asante Mungu kwa kumuongezea uhai Mwanyasi!
 
Mwenyenzi MUNGU mwingi wa Rehema na ampe Ndugu yetu Mwanyasi nguvu na apone mapema na arudi katika afya njema..........................................Hakika tutamwombea muda wote arudi katika afya yake ya kawaida kwani hakuna kinachoshindikana kwake Bwana wetu!
 
Last edited by a moderator:
Mungu pekee wa kumrudishia sifa na idumu kwake daima!

Pamoja sana Mwanyasi Kamanda wetu!!!!!!!!

Wanajamvi nawashukuru sana kwa salaam zenu jamani,
Namshukuru Mungu leo nimeweza kuwapa taarifa hii nikiwa mzima! Nilipoteza ufahamu kwa muda wa mwezi mmoja na wiki 2 hiyo haikuwa rahisi kutoa taaarifa yoyote kwenu ndugu zangu.
Nawaashukuru wote kwa salaam na kunitakia heri, zaidi namshukuru Mungu kwa kuniponya.

Ahsante ndugu zangu wana JF.
 
Last edited by a moderator:
Wanajamvi nawashukuru sana kwa salaam zenu jamani,
Namshukuru Mungu leo nimeweza kuwapa taarifa hii nikiwa mzima! Nilipoteza ufahamu kwa muda wa mwezi mmoja na wiki 2 hiyo haikuwa rahisi kutoa taaarifa yoyote kwenu ndugu zangu.
Nawaashukuru wote kwa salaam na kunitakia heri, zaidi namshukuru Mungu kwa kuniponya.

Ahsante ndugu zangu wana JF.

Mungu mkubwa
tumefurahi kukuona
nilifikiri Smile anakuogesha na maji ya ukili ukajisahau kuingia hapa
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka hadi kuna siku tulikuwa tunachart na YNNAH tukawa tunaulizana bila majibu.....na siku ile tukaonga ukanambia simu za Mwanyasi hazipokelewi.....sijui kahama mji kimya kimya.

Basi tunamshukuru Mungu kwa miujiza yake. Mungu aendelee kumlinda na ampe maisha marefu

Ahsante KOKUTONA Mungu ni mwema!
 
Last edited by a moderator:
This is shocking newz!

Kuna siku alinambia atahamia kijijini, mi nikadhani ametimiza azma yake kimyakimya, kumbe ndivyo sivyo.

Nianze kwa kutoa pole za kutoka ndani ya roho yangu kwa mpendwa wetu
Mwanyasi, kijana ambaye sisi wengine tunajuana naye kwa undani hadi kwa masuala ya kibinafsi. Pole sn mpendwa. Lakini naamini kuwa Mungu atawalaye ana mpango mwema sn na si wewe tu, bali hata sisi rafiki zako, maana amekuongezea wewe na sisi siku za kuwa pamoja, ishara kwamba kuna mambo kadha wa kadha ambayo tunapaswa kuendelea kuyajadili pamoja.

Pia nichukue nafasi hii adhimu kutuma salamu zangu za pole kwa memberz wote wa Tanga Wing kwa tukio hili baya na la kusikitisha. Bila shaka Mungu alimaanisha kitu kwa kulificha jambo hili machoni penu, huenda mngejua tungepata tatizo la ziada.
Poleni sana Dark City, KOKUTONA, YNNAH, Arabela na CHUAKACHARA. Mungu atawafariji nyote kwa jinsi yake.

Sisi Arusha Wing kama wazazi wenu tunawaahidi kuwa tuko pamoja nanyi, na dua zetu pokeeni,
Amina.

Mkuu PakaJimmy ahsante sana Mungu ni mwema!
Niko vizuri kwa sasa, namshukuru Mungu mipango yake haitabiriki!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom