Mwanyasi yuko salama baada ya kupata ajali mbaya.....

Mwanyasi yuko salama baada ya kupata ajali mbaya.....

Dark City

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2008
Posts
16,252
Reaction score
11,653
Habari za siku nyingi ndugu wana MMU,

Napenda kuwashirikisha habari nilizopata muda mfupi uliopita kumhusu mwenzetu Mwanyasi, katibu wetu wa Tanga Wing ambaye alipotea ghafla kwa muda mrefu. Kama mwezi mmoja na nusu uliopita, tulijaribu kumtafuta kwa kila njia lakini hatukumpata. Tulihisi kwamba labda yuko vijijini kikazi na ndiyo maana hapatikani. Leo kanipigia simu na kunipatia habari ambazo zimenisikitisha sana.

Ni kwamba kama mwezi mmoja uliopita, Mwanyasi alipata ajali ya pikipiki na kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo. Alikaa pale kwa muda na madaktari wakampatia rufaa ya kwenda Muhimbili. Wakati huo alikuwa hajitambui na alipopata fahamu kidogo, alikuwa akiongea mambo ambayo hayaeleweki (was halucinating). Muhimbili walimfanyia kipimo cha MRI na kugundua kuwa alikuwa amepasuka mishipa midogo kwenye ubongo na kusababisha damu kuvuja kwenye ubongo (brain haemorrhage). Alipatiwa dawa na kukaa Muhimbili kwa zaidi ya mwezi mmoja, akiwa bado hajitambui. Kwa sasa amepata nafuu na kurudi Tanga.

Nimeongea naye muda mfupi na kustuka sana kwa hili tukio lililompata. Hata hivyo, nimefarijika sana kwamba ndugu yetu yuko mzima na anaendelea vizuri.

Nimemwomba sana Mwanyasi na namshukuru kwa kukubali ombi langu la kuwajulisha ndugu zetu wengine wa JF, wana Tanga Wing, Arusha Wing na wadau wengine ambao walikuwa naye karibu.

Naomba tuzidi kumwombea apone kabisa na kurejea katika shughuli zake.

Babu DC!!

cc: KOKUTONA CHUAKACHARA, YNNAH, PakaJimmy, black womani, Preta, Mzee wa Rula, Filipo, Lily Flower, Smile, gfsonwin, Madame B, watu8, Arusha one, LiverpoolFC, Mungi, Fixed Point, amu, Paloma, Husninyo, Dena Amsi
 
^^
Usihofu Mungu bado anakuhitaji utimize kazi yake.
Get well soon our dear
^^

Kweli kabisa ....

Ila nimejifunza kutochukulia kimzaha kitendo cha member kutoonekana JF kwa muda mrefu...

Imenisikitisha sana kwani pamoja na kuwa na namba zake za simu, tulishindwa kumpata...

Babu DC!!
 
asante sana mzee mwenzangu kwa taarifa nami nilijaribu kimtafuta sikumapata nikajua mambo mengi mjini kumbe mwenzetu alipatwa na matatizo naamini mwenyezi mungu mwenye huruma amekuwa naye siku zote hadi kufikia hapo tuendele kumwombea aendele kumjalia kupona haraka... Dark City tupo pamoja
 
Last edited by a moderator:
asante sana mzee mwenzangu kwa taarifa nami nilijaribu kimtafuta sikumapata nikajua mambo mengi mjini kumbe mwenzetu alipatwa na matatizo naamini mwenyezi mungu mwenye huruma amekuwa naye siku zote hadi kufikia hapo tuendele kumwombea aendele kumjalia kupona haraka... Dark City tupo pamoja


Ahsante sana mzee mwenzangu,

Unajua tulimtafuta sana hadi tukakata tamaa...baadhi ya wadau walihisi kwamba labda yuko nje ya nchi...Kumbe alipata matatizo makubwa kiasi hicho. Na pia inasikitisha kwamba alilazwa jirani na ofisini kwangu ila sikujua hata niende kumwona.

Mungu ni mkubwa na sasa amemwezesha kupata nafuu...

Babu DC!!
 
Pole sana Manyansi.
Kumbe watu tukipotea huwa tunawapa tabu wengine tabu namna hii?? sikujua hili ila leo nimelitambua.

Mungu yu mwema sana na wema wake upo kwa Manyansi hata sasa. Haijalish kwamba Manyansi kapita mapto gani lakini bado wema wa Mungu upo katikati yake na bado anashughulika na maisha yake.Jina la MUngu wa Yakobo likuinue Manyansi na Mungu akutumie msaada toka patakatifu pake. Mungu azikumbuke sadaka zako na kuzitakabali dhabihu zako na siku ya leo zikutetee mbele za uso wa Mungu kwamba na wewe unahitaji uponyaji.

Daima kumbuka ALICHUBULIWA KWA MAKOSA YAKO, ALIJERUHIWA KWA MAOVU YAKO, ADHABU YA AMANI YAKO ILIKUWA JUU YAKE, NA KWA KUPIGWA KWAKE WEWE UMEPONA.
 
Last edited by a moderator:
Duh hiyo ni mbaya sana. mwenyezi mungu ampe nafuu mapema na amwepushe na mabaya mengine kama alivyomwepusha kwa hili. Yeye tu ndiye mlinzi wetu na ndiye mjuzi wa kila jambo. Inshaallah utapona tu ndugu yetu.
 
Back
Top Bottom