Mwanyamaki Kumburuza Mwakyembe mahakamani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,197
217,152
Kama ulidhani sakata la ubunge kyela limemalizika basi futa mawazo hayo , taarifa kutoka kyela zinabainisha kwamba mgombea wa UKAWA Mh Abraham Mwanyamaki anaelekea mahakamani kupinga ubunge wa mwakyembe , tayari wananchi wa kyela wamefahamishwa kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika jimboni hapo , inasemekana kuna kata imeongezwa kinyemela huko Mwaya inaitwa serengeti , maana yake ni kwamba safari hii kyela ilikuwa na kata mbili zinazoitwa serengeti ! Moja ya mjini (ambayo ni halali ) na nyingine ya mwaya ( ambayo ni ya magumashi ), tuendelee kutega sikio .
 
tafsiri ya demokrasia ya kweli kwa wana UKAWA ni kwamba, uchaguzi unatakiwa upigwe tena, tena na tena mpaka mgombea wao apate kura za kutosha.
 
Hiv kumbe jamaa hakushinda kihalali?
Siyo kihalali tu bali hakushinda kabisa , mpaka leo wananchi wa kyela wanaandamana kwenda kwenye ofisi za mkurugenzi kudai atangazwe mwanyamaki .
 
tafsiri ya demokrasia ya kweli kwa wana UKAWA ni kwamba, uchaguzi unatakiwa upigwe tena, tena na tena mpaka mgombea wao apate kura za kutosha.
Hatutakubali haki ipotee hivihivi , mwakyembe anaujua ukweli wote kwamba hakushinda , na kwa ushahidi uliokusanywa hatoki mahakamani .
 
Siyo kihalali tu bali hakushinda kabisa , mpaka leo wananchi wa kyela wanaandamana kwenda kwenye ofisi za mkurugenzi kudai atangazwe mwanyamaki .

Hii nchi inaboa sana kwani karatasi za vituoni huyo mwanyamaki si alishinda?
 
Lakini cha kushangaza mwakyembe kapewa 52% eti kwamba kapata kura 44,296
Mwanyamaki akapewa 46.8% eti kapata kura 39,379
 
Hatutakubali haki ipotee hivihivi , mwakyembe anaujua ukweli wote kwamba hakushinda , na kwa ushahidi uliokusanywa hatoki mahakamani .

Kama hamkubali kuweni Museven akiwa na bunduki 7 na wenzake 27 walichukua nchi
 
Kwa mwakyembe kuna mengi sana. Tetesi zinasemekana kuna sanduku moja liliingizwa likiitwa Serengeti gani sijui ambalo wala halipo kyela. Wakala wa CHADEMA wakati anapinga kuhusu kura za sanduku lile akapigwa na ocd kwamba ana makelele. Nakala zote za kura za vituoni anazo mwamnyaki.

Zinaonyesha pamoja na hilo sanduku la bakshish mwakyembe alizidiwa.

Ninaona ushauri wa kwenda mahakamani ni mzuri. Tena awahi mapema kbla supu haijapoa.

Kinachotakiwa ni haki itendeke bila kujali ni mwakyembe au ni Mwamnyaki.

Haki huimarisha taifa.
 
Siyo kihalali tu bali hakushinda kabisa , mpaka leo wananchi wa kyela wanaandamana kwenda kwenye ofisi za mkurugenzi kudai atangazwe mwanyamaki .
wee vp watangazwe wangapi ubunge? kama ana ushahidi aende mahakamani mwakyembe kashatangazwa mshindi.
 
Siyo kihalali tu bali hakushinda kabisa , mpaka leo wananchi wa kyela wanaandamana kwenda kwenye ofisi za mkurugenzi kudai atangazwe mwanyamaki .
hebu acheni Majungu enyi Wanyakyusa
kwani ni lazima mshinde? kwa kumuangusha
Mwakyembe ni JEMBE kwa Tanzania nzima ndiye aliyemng'oa Lowassa
mlilipwa mkamdhalilisha na kote akashinda
sasa JPM atamchagua kuwa Waziri Mkuu wa Serikali yetu
sasa mumtake msimtake kwetu atapitia Wabunge maalum 10 wa Rais
 
Kwa mwakyembe kuna mengi sana. Tetesi zinasemekana kuna sanduku moja liliingizwa likiitwa Serengeti gani sijui ambalo wala halipo kyela. Wakala wa CHADEMA wakati anapinga kuhusu kura za sanduku lile akapigwa na ocd kwamba ana makelele. Nakala zote za kura za vituoni anazo mwamnyaki.

Zinaonyesha pamoja na hilo sanduku la bakshish mwakyembe alizidiwa.

Ninaona ushauri wa kwenda mahakamani ni mzuri. Tena awahi mapema kbla supu haijapoa.

Kinachotakiwa ni haki itendeke bila kujali ni mwakyembe au ni Mwamnyaki.

Haki huimarisha taifa.
Umeandika kistaarabu sana mkuu , Mungu akulinde .
 
Watu wanatafakari kati ya Mwakyembe,Lukuvi na Mhongo nani waziri mkuu nyinyi mnaleta stori za ovyo kabisa humu.

Mbona mmchelewa sana wenzenu wanasonga mbele.
Kwa mujibu wa sheria za nchi hii ni kwamba waziri anateuliwa kutokana na wabunge waliochaguliwa majimboni , sasa huyu katangazwa hakuchaguliwa .
 
hebu acheni Majungu enyi Wanyakyusa
kwani ni lazima mshinde? kwa kumuangusha
Mwakyembe ni JEMBE kwa Tanzania nzima ndiye aliyemng'oa Lowassa
mlilipwa mkamdhalilisha na kote akashinda
sasa JPM atamchagua kuwa Waziri Mkuu wa Serikali yetu
sasa mumtake msimtake kwetu atapitia Wabunge maalum 10 wa Rais
Sasa mbona mlimtelekeza bila msaada ? Mkasubiri mpaka agalagazwe ndio mumuokoe kwa mlango wa uani ! Haya sasa wananchi wa kyela wameuza mpunga na cocoa ili kugharamia kesi mahakama kuu .
 
Erythropoietin/erythrocyte wew mwakembe alikokosea nin mbona kwanzia 2014 unamwaandama sana DR . Mwakembe,mara oo!!! Hatoki mara anahali ngumu ona sasa ulivyoumbuka na unafiki wako , hivi huyu dr,alikutelekeza akaoa mke mwingine ndio maana una hasira naye
kwanin usiwe hata na chembe ya busara kuanzia kumpokea FISADI ,huku ukipingana na matamshi yako ?
 
Back
Top Bottom