Wananchi wa Kyela wasema sasa basi CCM na Mwakyembe, sasa na Abraham Mwanyamaki (CHADEMA)

mwamajinja mapunga

JF-Expert Member
Dec 23, 2014
1,074
607
Katika uzinduzi wa kampeni za CHADEMA/UKAWA uliofanyika tar. 5/9/2015 Kyela mjini maeneo ya viwanja vya mchaga Kyela wenyewe huviita viwanja vya SUGU... Ambapo Wananchi wa Kyela walimpokea shujaa wao na tegemeo kijana makini ndg Abraham Mwanyamaki kwa nderemo na vifijo, shamra shamra za ngoma, madereva wa bodaboda wanaomuunga mkono na wananchi wengi walio na wasio na vyama.....mgombea aliambatana na ndg. JOSEPH MBILINYI (MB) A.K.A SUGU AU RAIS WA MBEYA, pIA NA MWANDISHI MAHIRI WA GAZETI LA MWANAHALISI NDG SAED KUBENEA... ambapo mheshimiwa Sugu alimnanga mwakyembe kwa unafiki, uzandiki na mambo ya kutunga kwa wananchi, pia alisikitika kuona kyela vumbi linatimka kila mahali ni aibu kwa mbunge,,,,akafuatia saed kubenea ambaye alitoa nyaraka ambazo ziliandikwa na dr. mwakyembe kwa jeshi la polisi kuwa anafuatiliwa na watu wanataka kumuua, akaongeza kuwa dr. mwakyembe hana legacy ya kuongelea RICHMOND Hata kidogo na akasisitiza kuita press conference kuongea kilicho moyoni na na kusema uongo wa dr. mwakyembe alichokisema ni uongo kwa kuwahadaa watz, pia akagusia mabehewa feki ya mwakyembe, n.k IMG_20130601_033228.jpg IMG_20130601_033228.jpg IMG_20130601_033536.jpg IMG_20130601_030537.jpg IMG_20130601_033224.jpg
 
Nilikuwepo mjini Kyela siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana.

Nilipoona kichwa cha habari hapa nikahamasika kusoma nipate ile radhi niliyoionja mwaka jana. SIJAIPATA...

Andika vizuri, ni kama umekurupuka, taarifa haijikamilishi.


Tafakari...
 
Nilikuwepo mjini Kyela siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana.

Nilipoona kichwa cha habari hapa nikahamasika kusoma nipate ile radhi niliyoionja mwaka jana. SIJAIPATA...

Andika vizuri, ni kama umekurupuka, taarifa haijikamilishi.


Tafakari...

Angalia hata picha basi.
 
Angalia hata picha basi.




Mkuu DALLAI LAMA, nimezingatia picha pia.

Nilichokuwa na bashasha nacho ni maudhui yatokanayo na kichwa cha habari. Kama lengo lilikuwa ni kutuhabarisha muitikio wa wana Kyela kwenye mkutano ule basi angeweka heading inayoendana na picha.



Tafakari...
 
Mzee wa " Na mwachia mungu" Mnafiki mkubwa, wivu, fitna, chuki na uongo ndivyo vilivyo mjaa rohoni. Kidogo tu angezaliwa mwanamke.
 
Sijui ni kwanini huwa nawaona wanafiki hawa watu,Mwakyembe,Sitta na Mwambalaswa. Mungu anisamehe.
 
Back
Top Bottom