Ilongailunga
JF-Expert Member
- Jan 18, 2012
- 1,388
- 895
ni haki yake kwenda mahakamani. wasisahau na rungwe....
Nae alikubali kura zihesabiwe upya?
ni haki yake kwenda mahakamani. wasisahau na rungwe....
kuna watu wanamwandama sana mwakyembe na mbaya zaidi kat ya wote wanaomwandama hawaishi kyela. Wengi wanaiangalia kyela pale mjini tu ndio hapo wanamlaumu. Lakn kwamimi niliyekulia kyela tangu enzi za akina kasyupa, mwakipesile na mpaka hii ya mwakyembe hakuna mbunge aliyefanya vzr zaidi ya mwakyembe. Kyela maeneo ya vijijin kuna sehem watu walikuwa wanaliwa na mamba sababu ya ukosefu wa barabara, watu walikuwa wasombwa na maji.
Hakuna
Kuna maeneo kuuona umeme ilibidi mpaka uje kyela mjini, kuna watu wamekunywa maji ya mito tangu uhuru mpaka alipoingia mwakyembe 2005 lakn sasa hvi barabara zinapitika mpaka vijijin sitimbi, umeme mpaka mashamban, maji mpaka yamejaa tele. Lakn bado watu hawaoni tofauti.
Kuna kipindi mwakyembe alikuwa anaonekana adui wa ccm yote hyo kwaajili ya kuipigania maendeleo ya kyela. Lakn yote hayo hawayaoni.
Kwa wanakyela wachache mnaomchukia mwakyembe mjue mnajisumbua. Mungu yu pamoja na mwakyembe atampigania kama alivyompigania kipindi jitu jeupe lilivyotaka kumfanyia figisu.
Mwakyembe hajawakosea wanakyela anatenda kadri ya uwezo wake na kadri bajeti inavyopangwa.
Hiv kumbe jamaa hakushinda kihalali?
tafsiri ya demokrasia ya kweli kwa wana UKAWA ni kwamba, uchaguzi unatakiwa upigwe tena, tena na tena mpaka mgombea wao apate kura za kutosha.
.
Mwakyembe amefanya nini Kyela cha maana? Orodhesha.
Na usidanganye. Daraja lililjengwa na wanajeshi enzi zile ndilo unasema kaejnga mwankyembe?
Kyela kila siku watu na madumu ya utafuta maji. Maji hakuna ni shida tena wako ziwani kila siku mafuriko yanawakimbiza.
Unataka kusema nini juu ya barabara. Unasahau kwamba kila mwaka tunaona vile sehemu mbali mbai za kyela zinakatika wkati wa mvua watu wanatembea wamebeba baiskeli mabegani wakivuka maji ajili ya ukosefu wa barabara?
Wadanganye wengine lakini usiwasemee uwongo wanakyela. Uwongo huo ni wa Mwakyembe tu lakini sisi hapata. "Ubutungulu bubibi fijo".
Mwakyembe hajashinda kihalali...
tupe vielelezo vinavyoonesha hajashinda kihalali
Mkuu weka siasa kando, tafuta nduguzo wa Kyela wakusimulie A - Z ilivyokuwa....
Harrison alikuwa kashakatwa na raia karudi kwa nguvu ya CCM
Ibara number 41 ya katiba ya JMT inazungumzia uchaguzi wa raisi. Ninaomba wanasheria mtusaidie kupata ufafanuzi kifungu cha saba.
(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwaamechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidikuliko mgombea mwingine yeyote.
(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzikwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basihakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka yakuchunguza kuchaguliwa kwake.
Ufafanuzi ninaoumba ni kama tangazo la tume juu ya raisi litakuwa na kinga ya kutokuchunguzwa na mahakama yoyote hata pale ambapo maamuzi ya tangazo hilo hayajazingatia matakwa ya Ibara hii ya 41 mfano kama kifungu cha 6 ama chochote kikiwa kimekiukwa.
Kifungu cha saba kinasema wazi "Iwapo mgombea ametangazwa na tume ya uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa raisi kwa mujibu wa ibara hii (ya 41)". Vipi kama kilichotangazwa hakiko kwa mujibu wa ibara hii? Bado tangazo hilo ni legally binding?
Swali lingine, ni chombo gani kinatakiwa kuhakiki compliace ya tume ( iliyopewa nguvu hiyo kwenye) ili kujiridhisha kwamba inachokitangaza kimefanyika inline with stipulations za ibara hii ya 41?
Vipi ikitokea msemaji wa tume, on insanity, corruption, Rebellion, conspiracy, au threat grounds akamtangaza mtu kuwa raisi bila taratibu na mahitaji ya ibara hii ya 41 kufuatwa, bado itakuwa ni lawful, binding and enforceable announcement?
NAOMBA TUJADILIANE NA KUELEIMISHANA KWA HOJA. Na ni vizuri tukiwa tunarejea mfano wa kifungu cha sita hapo juu.
Hivi watanzania tumefikia huku ! Eti mtu aachwe akisigina sheria kisa tunataka awe waziri ? Sasa kama ataharibu katika ngazi ya ubunge unadhani akiwa waziri itakuwaje ?Hebu nisaidie Kisheria, kama atakuwa Mbunge wa kuteuliwa na akawa Waziri Mkuu
ninyi mliempeleka Mahakamani akaukosa huo Ubunge wa Kyela mtapata faida gani?
mjaribu kuiga makabila ya wenzenu, hasa wa kaskazini, km wana mgombea yupo ngazi ya juu na hasa uwaziri ni nadra sana kumpinga, ni makabila machache km Wanyakyusa, wagogo ndio ambao hawajali cheo/uwaziri wa mgombea wao ni bora WAKOSE WOTE
nawashauri Harrison Mwakyembe mumuwache tu yeye ni Jembe la Magufuli, kuanzia Kura za maoni CCM mlimchafua
Mkamkodi Lowassa na Kubenea wakammalize kisa tu kasema ukweli kuhusu Richmond
Unajua Mgirik hata bado sijajua unachotetea , kama kweli unamuogopa Mungu wako na unajua kilichotendeka kyela tubu dhambi zako , nakuombea msamaha wa nguvu sana kwa muumba , mimi naamini umeteleza tu .acha kuudanganya umma. Ww uko dar unatoa taarifa za kyela wakat sisi tuliopo huku hatujaona kitu kama hyo.
Mkuu nikuulize ulienda kupiga kura kyela?
Alichofanyiwa mwambigija rungwe hakikubaliki na wala hakijawahi kukubalika popote .ni haki yake kwenda mahakamani. wasisahau na rungwe....
Unajua Mgirik hata bado sijajua unachotetea , kama kweli unamuogopa Mungu wako na unajua kilichotendeka kyela tubu dhambi zako , nakuombea msamaha wa nguvu sana kwa muumba , mimi naamini umeteleza tu .
Ni kijiji gani kilichoahidiwa kuondolewa maji ya kichocho ambacho kimeondolewa , kwanini mradi wa maji wa DANIDA umekufa ? Je kwanini kata feki imechomekwa ili kuwezesha ushindi kwa mtu anayejiamini kumwaga maendeleo kyela ?sijateleza hata kidogo naongea yaliyotendeka. Baadhi aliyofanya mwakyembe nmeyataja hapo juu ila kama ni uongo yakanushe ww na uniambie nani kayafanya.
Au kukurahisishia nenda pale mbeya mjin kwa jimbo la sugu au iringa mjin kwa msigwa halafu njoo na matokeo waliyoyafanya kwa kipind chao uone kwann namktaa hata mwanyamaki
Sijawahi kuona kesi nyepesi ya uchaguzi kama kesi hii ya kyela.Duuuu kazi ipo, lkn ni haki yake kushtaki
Vipi kwa tafsiri ya CCM na ZEC Zanzibar? Wao ili demokrasia itamalaki inatakiwa uchaguzi ufutwe na kurudiwa tena hadi mgombea wao ashinde?
Kama dai hilo ni la uzushi, anayeenda mahakamani atapoteza fedha yake bure. Ila kama kweli hiyo kata haipo imewekwa kinyemela, huna sababu ya kutetea ushetani huo.
Ni kijiji gani kilichoahidiwa kuondolewa maji ya kichocho ambacho kimeondolewa , kwanini mradi wa maji wa DANIDA umekufa ? Je kwanini kata feki imechomekwa ili kuwezesha ushindi kwa mtu anayejiamini kumwaga maendeleo kyela ?
Ni kijiji gani kilichoahidiwa kuondolewa maji ya kichocho ambacho kimeondolewa , kwanini mradi wa maji wa DANIDA umekufa ? Je kwanini kata feki imechomekwa ili kuwezesha ushindi kwa mtu anayejiamini kumwaga maendeleo kyela ?