Mwangonda wa TISS ni Jasusi

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
Kwenye viunga vya St Peters kutoka 1995 hadi 2005 kinatajwa kuwa ni kipindi kigumu sana kwa Tanzania kufuatia mambo kadhaa wa kadha yaliyofuatana. Mosi ilikuwa nchi haijatengamaa kiuchumi tangu tutoke vitani Uganda miaka kumi hivi nyuma (1980), Pili nchi ilikuwa imepitia majaribio mawili ya mapinduzi yaliyofeli, Tatu tulikuwa tumekabiliwa na shinikizo la kimataifa kwamba lazima kuwe na mfumo wa vyama vingi na turuhusu Demokrasia itawale nchi, na Nne, tulikuwa tumetoka kukabiliwa na changamoto ya uchaguzi wa vyama vingi kwa mara ya kwanza, kumbuka tulikotoka tulikuwa tukifanya chaguzi kwakupigia kura Mwalimu Nyerere au Kivuli.

Huu ulikuwa mtihani mkubwa uliokuwa ukiikabili idara ya Usalama ya wakati huo ikitambulika kama Tawi Maalumu, Ulikuwa ni mtihani kwelikweli kwakuwa Tangu mwaka 1962 hadi 1992 Chama kilikuwa ndio serikali yaani nchi ilikuwa ya chama kimoja, na kwa msingi huo Idara hiyo ya Usalama ilikuws sehemu ya Chama tawala kwa sheria, muundo na vitendo.

Unapoizungumzia Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania ya leo (TISS) utafanya kosa kubwa sana kujaribu kufuta ama kutotambua nani alifanya mageuzi kutoka chombo kisicho cha kisheria kikifahamika kama Tawi Maalumu (SB) hadi kuwa idara ya kiutumishi wa umma yenye miiko na maadili yake bila kumtaja Mzee Apson Mwang'onda akihudumu kwakuasisi chombo hiki katikati ya viunga vya St Peters kule Masaki

Kwenye korido za Ujasusi wazee wanakumbuka siku za mwanzo za shinikizo la mageuzi ya kuundwa upya kwa chomo hiki na kuzaa TISS, wanakumbuka Mwang'onda alivyokabiliwa na upinzani juu ya mawazo yake kwamba chombo hiki kitenganishwe na miundo ya kijamaa ambayo ilikuwa na nguvu za kisiasa,

Hoja yake ikiwa kwamba kama Katiba ya Nchi imefanyiwa marekebisho na kutambua kuwa Tanzania ni nchi ya muundo wa Vyama vingi, ni wakati sasa TISS mpya isiwe sehemu ya chama bali iwe sehemu ya serikali tu, na kwamba nguvu kubwa ielekezwe katika kuangazia uwekezaji mpya toka Magharibi na Mashariki na kudhitibi soko huria.

Wagumu na makuwadi wa soko huria wakasema hii itahatarisha chama kushika hatamu ukizingatia hawa wengi wao hawakutaka mfumo wa vyama vingi, mvutano huu ukahitimishwa kwa bunge la ndioooo la mzee Msekwa na hatimaye 20 June 1997 Rais Benjamin Mkapa akaidhinisha sheria iliyoanzisha safari mpya ya TIS hii ya sasa.

Ndani ya TISS Mwang'onda anatajwa kama Jasusi aliyeleta neema kwa maafisa katika mambo makuu mawili, Kwanza mageuzi ya muundo wa TISS kuwa kazi ya Utumishi wa Umma inayotambuliwa kisheia na yenye miiko ya kiutumishi, hapa faida kubwa ikawa rasmi ukistaafu unalipwa pesheni zako, na pia ikasaidia kwamba mtumishi huyu huwezi kumfukuza kazi bila kufuata taratibu za ajira Tanzani.

Pili ni kuwa utumishi wa mtumishi huyu ukawa huru, lakini kazi za mtumishi huyu zikalindwa kwakuwekewa sheria ya siri rasmi. Hili lilisaidia usalama zaidi wa maafisa hawa katika majukumu yao.

Matokeo ya mageuzi hayo wote tumeyaona, upande wa siasa kulikuwa na bado kuna matokeo chanya kwa wahafidhina na makuwadi wa soko huria, huku upande wa uchumi kuligeuka shamba la bibi kila mwenye kapu akivuna na kuondoka. Achilia mbali porojo za Tanzania mpya ama sijui Tanzania ya Viwanda. Hayo yote hayawezi kutendeka ama kufikia malengo ikiwa TISS haijafanyiwa mabadiliko iondoke kwenye mifumo ya kijamaa na falsafa za chama Dola,

Ni vigumu na sitaki kuamini kuwa hii ndio heshima tunayokupa mtu mhimu sana kwa nchi yetu mzee wetu Apson Mwang'onda uliyebeba alama ya mageuzi ya Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania.



Na Yericko Nyerere
 
Huu ujinga wa kusifia watu wakifa ndio sinaga mimi..

wakati wake ndio ufisadi wa EPA, Mgodi Wa Kiwila ulichukuliwa kinyemela, ufisadi wa Uuzwaji wa NBC, Uuzwaji wa nyumba za serikali kwa bei za sawa na bure na ushenzi mwingine kibao.

Mpaka Mkapa anaenda kujenga jumba la kifahari south africa yeye anamkenulia meno tu, alishindwa nini kudhibiti ayo mambo?
 
Heading imekaa kiajabu: ni sawa na mtu aseme "yule dereva anaendesha gari ni dereva".
 
Huu ujinga wa kusifia watu wakifa ndio sinaga mimi..

wakati wake ndio ufisadi wa EPA, Mgodi Wa Kiwila ulichukuliwa kinyemela, ufisadi wa Uuzwaji wa NBC, Uuzwaji wa nyumba za serikali kwa bei za sawa na bure na ushenzi mwingine kibao.

Mpaka Mkapa anaenda kujenga jumba la kifahari south africa yeye anamkenulia meno tu, alishindwa nini kudhibiti ayo mambo?
Umeona wapi mtu anang'atwa na mbwa wake mwenyewe?
Ikitokea hivyo basi huyo mbwa ana ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
 
Yericko Nyerere,

jaji mfawidhi ,

Jasusi hasifiwi , yaani vyombo vya ulinzi na usalama watumishi wake hawasifiwi bali husubiriwa kupata lawama pale chombo kinapokuwa kimeshindwa kufanya kazi kwa ufasaha.

Hata uandishi wako umeonesha kuwa unauma na kupuliza kuhusu kazi za huyo Mzee.

Lala salama Mzee. Apson M..
 
ni kweli hatutofika popote tukishindwa kutenganisha maslahi ya taifa vs maslahi ya chama dola.
 
wewe huna uwezo hata wa kuandika makala kwenye gazeti la michezo unadharau mwenzio aliyeandika kitabu? lumumba buku 7 shida sanaaaa
HAWAJIELEWI na hivi mau amekata mrija saa hii wamebaki kuimba nyimbo za sifa na kuabudu kama harmoniser
 
Wewe msukule wa lumumba FC buku saba umeandika kitabu gani??
Hawa wamemtenga sana Apson kwenye msiba , viongozi wa zama zilizopita ndio wamemzika ...ujumbe wa serikali ya sasa ulikuwa wa mawaziri wa kawaida ....angalau kama rais alishindwa kwenda ingetakiwa waziri mkuu au makamu awepo pale
 
Hawa wamemtenga sana Apson kwenye msiba , viongozi wa zama zilizopita ndio wamemzika ...ujumbe wa serikali ya sasa ulikuwa wa mawaziri wa kawaida ....angalau kama rais alishindwa kwenda ingetakiwa waziri mkuu au makamu awepo pale
Ndiyo kawaida yao mkuu
 
Back
Top Bottom