Napendekeza TISS ivunjwe, iundwe Upya

The Whistleblower

Senior Member
Dec 9, 2022
137
224
Hii Taasisi ilikuwa imara sana enzi za mwalimu Nyerere na mwisho kabisa kwa Mkapa,baada ya hapo imekuwa Taasisi ya kisiasa.

Inafanya kazi kwa maslahi ya wanasiasa na siyo Taifa na ndiyo sababu hali ya maisha ya watu inazidi kuwa mgumu kila siku iitwayo leo.

Kazi kubwa ya TISS ni kulinda usalama wa nchi kiuchumi na mipaka yake, hii Taasisi inayohitaji watu wanaoipenda nchi yao kwa Dhati, yaani Wazalendo kweli kweli na siyo makada wa UVCCM.

Siku hizi mtu akiwa kada mwaminifu wa Chama anapewa kazi TISS.

Ndo maana yameibuka magenge mengi mno yanayohujumu Uchumi wa Tanzania kuanzia mitandaoni hadi mitaani.

TISS ivunjwe, iundwe upya.
 
Naunga mkono hoja na niliwahi kushauri
P
Watu wengi walishauri hivyo watalaam hadi wananchi wa kawaida.

Lakini swali moja nimuulize Mleta Mada ni Lini Hicho chombo au vyombo vingine vimewahi kuwa na Wafanya kazi wasio na kadi ya ccm?
It has been so for so long.

Wewe Pascal Mayalla unajua Mpaka miaka ya 90s Mwanafunzi akienda Shule sekondari, Chuo au hata jeshini alikuwa haulizwi cheti cha kuzaliwa wala cha Taaluma. Kwanza aliulizwa una Kadi ya CCM?
 
Waanze kuvunja wapi sasa?
Kwamba wavunje vuup?
Halafu kitokee nini?
Mizizi yote mpaka washona viatu waganga wauza kahawa wote wavunjwe?

Halafu hao wapya waanzie wapi kupata habari? Nani awafunze hao wapya.
Wakati hao wapya wakiwa mafunzo shughuli zao nani atazisimamia?.
Kuunda upya Taasisi ya usalama wa Taifa siyo kuwafukuza kazi wafanyakazi wake, maana yake ni kubadili utendaji wake kwa ujumla,na waajiriwa wapya wasiwe makada wa CCM wala CHADEMA,wawe Wazalendo kweli kweli
 
Hii Taasisi ilikuwa imara sana enzi za mwalimu Nyerere na mwisho kabisa kwa Mkapa,baada ya hapo imekuwa Taasisi ya kisiasa ...
siasa ni maisha ni kila kitu kwenye maisha.

Tatizo sio TISS tatizo ni siasa mbovu.
Kama tutahitaji kujenga Taifa letu inatupasa tushiriki vyema katika siasa.

Wananchi ndio wenye nchi hivyo tukipata mwamuko wa nguvu tutaweza kujenga Taifa imara na lenye uchumi imara.
 
Kuunda upya Taasisi ya usalama wa Taifa siyo kuwafukuza kazi wafanyakazi wake, maana yake ni kubadili utendaji wake kwa ujumla,na waajiriwa wapya wasiwe makada wa CCM wala CHADEMA,wawe Wazalendo kweli kweli
Naunga mkono hoja.

Nani wakuanza hiyo step?

Mtu mmoja alisema kuna Symbiosis kati ya hizo taasisi muhimu.

So they are inseparable...any attempt can lead to death of one or both
 
Ikivujwa TISS ya sasa itaundwa TISSCCM. Itajaa kijani tu.
Tatizo like palepale.
Katiba Katiba mpya sheria
Zikiwekwa zisimamiwe.
Watunhawa hawatakiwi kuteuliwa tuu.
Wafanyiwe usali na mwisho waende mafunzo ya kutenda haki!

Hii mambo ya kuenda mahali unajifanya kumkamata mtu au kuleta fujo eti unanijua mimi ni Nani! Ujinga.

Hawatakiwi kukamata hii ni kazi ya polisi wao wafanye kazi yao ya kutafiti !
 
Kuunda upya Taasisi ya usalama wa Taifa siyo kuwafukuza kazi wafanyakazi wake, maana yake ni kubadili utendaji wake kwa ujumla,na waajiriwa wapya wasiwe makada wa CCM wala CHADEMA,wawe Wazalendo kweli kweli
Kama una point..
Jambo linarudi pale pale hapo kwa wazelendo haswaa!
Hao wazelendo haswaa wapo?
Nani ndo atakaebadili utendaji wa wengin?
Huyo anaewabadilisha wengine ndo yanajirudi hayo hayo ya kisiasa.

Suala sio TISS suala ni mfumo mzima wa Taifa sio Elimu sijui majukum ya vyeo suala ni mfumo mzima juu ya taifa.
Na ili mfumo ubadilike ni mpaka Katiba pekee ibadilike ndo itabadilisha na majukum ya utendaji wa wafanyakazi wafanyabishara na mwananchi wa kawaida.
 
Kakudanganya nani kwamba haijulikani? Hivi watanzania mmelishwa nini na chama hadi kufikia mahali uwezo wa kufikiri hakuna kabisa.
Wananchi ndiyo TISS namba moja.
Hawa wafanyakazi wa TISS ni waajiriwa tu, hivyo kuvunja TISS ni wananchi kujielewa kwa kuwa active zaidi katika ulinzi wa nchi na uundaji wa serikali.
Ni muhimu sana kwa wananchi kujua kuwa wao wana haki ya kuwa TISS namba moja, vinginevyo kizazi chao cha baadaye chaweza kuwa watumwa katika nchi yao.
 
Rekebisha kauli yako, Haijawahi kuwa Imara, Toka imeanzishwa imekuwa ni Tawi la Chama Tawala.
 
Waanze kuvunja wapi sasa?
Kwamba wavunje vuup?
Halafu kitokee nini?
Mizizi yote mpaka washona viatu waganga wauza kahawa wote wavunjwe?

Halafu hao wapya waanzie wapi kupata habari? Nani awafunze hao wapya.
Wakati hao wapya wakiwa mafunzo shughuli zao nani atazisimamia?.
Nooo mkuu systems haifanyi kazi hivyo,hao wote uliowataja ni informers ambao wanakua na handlers wao,informers hawataathirika ,nchi imekua kama choo ya public
 
Hii Taasisi ilikuwa imara sana enzi za mwalimu Nyerere na mwisho kabisa kwa Mkapa,baada ya hapo imekuwa Taasisi ya kisiasa.

Inafanya kazi kwa maslahi ya wanasiasa na siyo Taifa na ndiyo sababu hali ya maisha ya watu inazidi kuwa mgumu kila siku iitwayo leo.

Kazi kubwa ya TISS ni kulinda usalama wa nchi kiuchumi na mipaka yake, hii Taasisi inayohitaji watu wanaoipenda nchi yao kwa Dhati, yaani Wazalendo kweli kweli na siyo makada wa UVCCM.

Siku hizi mtu akiwa kada mwaminifu wa Chama anapewa kazi TISS.

Ndo maana yameibuka magenge mengi mno yanayohujumu Uchumi wa Tanzania kuanzia mitandaoni hadi mitaani.

TISS ivunjwe, iundwe upya.
Ni Bora ya jeshi la polisi kuliko hao watu, ni watu wanaotumika kukomoa watu tu, hawana jipya lolote. Shame on them
 
TISS ivunjwe, iundwe upya.
Ninakubaliana nawe katika yote uliyo andika kuhusu taasisi hii.

Lakini, je, itawezekana vipi kuivunja na kuunda upya wakati watawala ni hao hao wanaolindiwa maslahi na taasisi hiyo?

Nitakuelewa ukisema kuwa pawepo (kwa miujiza?) na watu wenye uzalendo wa kweli juu ya nchi hii watakaosimamia mabadiliko makubwa ya mfumo mzima uliopo sasa.
Utaanzia wapi sasa hivi kubadili chochote, wakati kila kona imeshikiliwa na 'machawa' ambao wao wimbo wao muhimu katika maisha yao ni "Mama, Mama"?
 
Back
Top Bottom