Mwandishi wa Mwananchi Elias Msuya aitwa Polisi kuhojiwa kwa makala "Polisi na Hofu ya Watawala"

Mimi nilitarajia watoe taarifa na kuchukua hatua kwa watumishi wao ili kujitenga na utopokaji wao kumbe wanakwenda mkamata aliye wala tahadhari??
 
Huu uchambuzi wa Elias Msuya sikuusoma jana. Ngoja niusome kwa makini sasa hivi. Asanteni polisi kwa kutuhamasisha.

Hata mimi nimehamasika ikabidi nilitafute gazeti hilo la jana na kulisoma....Kiukweli makala hiyo ya Elias Msuya, kwa maoni yangu, siyo mbaya sana, isipokuwa imejaa generalization jambo ambalo siyo sahihi...Nadhani pia polisi wanaweza wakamshikia kuhusu ununuzi wa magari 777 ya polisi kama ni kweli au la...mantiki ya makala hiyo ni kukosoa utendaji wa jeshi la polisi jambo ambalo ni jema...Hata hivyo makala hiyo imeandikwa sawa na uandishi wa humu JF yaani hakuna uhariri...Laiti kama makala hiyo ingehaririwa kwa kuondoa generalizations kusingekuwa na tatizo lolote...Nadhani wahariri wa Mwananchi watajifunza kuhusu suala hili ili makala ziwe zinapitiwa vizuri...haya ni maoni yangu tu...
 
Huu uchambuzi wa Elias Msuya sikuusoma jana. Ngoja niusome kwa makini sasa hivi. Asanteni polisi kwa kutuhamasisha.
Ni kweli mkuu wakati mwingine polisi kwa vihere here vyao huwa wanasababisha habari ambazo zisingejulikana na wengi sasa kujulikana. Hata mimi imbebidi nitafute gazeti na kusoma makala hiyo.
 
Polisi wameacha majukumu yao na kuamua kufanya kazi ya kujipendekeza kwa watawala.
 
Vitendo wanavofanya ni dhairi kufanya taarifa hiyo iweze kufika kwa watu wengi. Mfano mii binafsi sikuisoma hiyo habari lakini wananifanya nilitafute hilo gazeti niwezze kusoma kwa undani.

Nakumbuka miaka ya awali kwa vyama vingi Tanzania (1995). Kulikuwa na MGOMBEA MMOJA wa urais upande wa upinzani, wananchi walikuwa wanasukuma gari lake, lakini Hayati Baba wa Taifa alitoa kauli kuwa msimfanye chochote au kumkamata hata wakiamua kumbeba kwani mtampandisha kisiasa. Na ndivvyo ilivyokuwa.

Sasa haya yabayofanyika yanazidi kuwafumbua watu macho na kuanza kuhoji ni kitu gani kimetokea hadi huyu mtu kuitwa polisi?????

Ni kwa nini hatupendi kuambiwa ukweli pale tunapokosea????? Hakuna mtu aliye kamili hapa Duniani.


MIZAMBWA
INANIUA SANA!!!
 
Baadhi yetu hatukubaliani na wewe...kauli yako hapa ni ya uchochezi...ni aina ya watu ambao mnaleta hoja halafu yakitokea mnaingia mitini...ni uongo kusema nusu ya watanzania watamalizikia kwenye magereza, hii ni kauli ya uchochezi na isiyo na ukweli wowote...umekuwa 'alarmist' kwa issues ambazo ni za kawaida...sasa hivi naanza kuisoma makala hiyo, ili name nione ni kwa vipi imefanya hao Ndugu zetu waitwe na polisi, lakini ni 'uongo' kuanza kubashiri kuwa nusu ya watanzania wataishia magerezani..
Haya maneno "uchochezi, uvunjifu wa amani" nk nayasikia sana yakitumiwa na serikali kukamata na kushitaki watu. Hivi mkuu ni nani kachochewa? Na baada ya kuchochewa amefanya nini cha kuvunja amani na utulivu? Hivi wananchi wa leo na elimu na akili zote walizo nazo bado mnafikiri ni watu wa kuchochewa kwamba hawawezi kufikiri na kutafakari wao wenyewe? Hili neno linatumika vibaya kubinya uhuru wa watu kujieleza. Vinginevyo toeni mifano ya watu waliochochewa na kuwa baada ya kuchochewa walifanya nini? Ni kama hilo neno "intelijensia" Hilo nalo limekuwa fasheni ya polisi kuzuia uhuru wa watu kukusanyika na kubadilishana mawazo au kujieleza. Utasikia eti mkutano umezuiwa au maandamano yamezuiwa kutoka na kupata habari za "kiintelijensia" Sasa kama umepata habari za kiintelijensia si ndiyo itakuwa vizuri kuwakamata hao watakaosababisa vurugu na kuwaacha wale wasio kuwa na shida kuendelea na mkutano wao? Mbona CCM wanamkutano 23 na polisi wamejazana Dodoma ili kukabiliana na wale watakoleta fujo na hii huenda ni baada ya kupata taarifa za kiintelijensia. Sasa jiulize kwanini hawazuii mkutano wa CCM kutokana na taarifa za kiintelijensia kuwa BAVICHA wamepanga kuwasaidia wao kuzuia mkutano wa CCM badala yake wao polisi ndio wamejazana kuulinda ni kwanini wasijazane pia kulinda mikusanyiko ya wapinzani kama wafanyavyo ya CCM baada ya kupata taarifa hizo hizo za kiintlijensia?! Ngumu kuelewa!
 
Baadhi yetu hatukubaliani na wewe...kauli yako hapa ni ya uchochezi...ni aina ya watu ambao mnaleta hoja halafu yakitokea mnaingia mitini...ni uongo kusema nusu ya watanzania watamalizikia kwenye magereza, hii ni kauli ya uchochezi na isiyo na ukweli wowote...umekuwa 'alarmist' kwa issues ambazo ni za kawaida...sasa hivi naanza kuisoma makala hiyo, ili name nione ni kwa vipi imefanya hao Ndugu zetu waitwe na polisi, lakini ni 'uongo' kuanza kubashiri kuwa nusu ya watanzania wataishia magerezani..


Kaka ungeisoma kwanza halafu uandike. Kwa sababu unaongelea kitu ambacho hukijui/hujakiona na unatoa conclusion na kuchukua msimamo hiyo si sawa.
 
Hongera sana Jeshi la Polisi kwa kupambana na Wachochezi
 
Kama ni kweli polisi wetu wamefikia mwisho wao wa kufikiri.
Makala hiyo nimeiona na kusoma kwa umakini mkubwa hauna uchochezi wowote...
 
Wangeadika Mwanahalisi na Mseto ungesikia wafungwe tu wamezoea kuandika habari za kichochezi
 
View attachment 366236

Mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Frank Sanga na mwandishi wake, Elias Msuya wameitwa na polisi kuhojiwa kuhusu makala iliyochapishwa na gazeti hilo kuhusu utendaji wa jeshi hilo.

Wakati Msuya alipigiwa simu jana na kuhojiwa leo asubuhi kuhusu makala aliyoandika, Sanga ameitwa leo na tayari ameondoka ofisini kwake kwenda Kituo Kikuu cha Polisi kuitikia wito huo.

Makala hiyo ya uchambuzi yenye kichwa cha habari “Polisi na Hofu ya Watawala Kuondoka Madarakani”, ilichapishwa na gazeti hilo jana.

Chanzo: Mwananchi
Tuwekee article yenyewe tafadhali.
 
wakati nchini uholanzi wameanza kufunga baadhi ya magereza kwa kukosa wafungwa,kuna baadhi ya nchi barani Afrika zinaendelea kujenga magereza!!! hebu tujiulize tofauti iliyopo hapo
 
Back
Top Bottom