Kansigo
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 2,670
- 2,156
Mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Frank Sanga na mwandishi wake, Elias Msuya wameitwa na polisi kuhojiwa kuhusu makala iliyochapishwa na gazeti hilo kuhusu utendaji wa jeshi hilo.
Wakati Msuya alipigiwa simu jana na kuhojiwa leo asubuhi kuhusu makala aliyoandika, Sanga ameitwa leo na tayari ameondoka ofisini kwake kwenda Kituo Kikuu cha Polisi kuitikia wito huo.
Makala hiyo ya uchambuzi yenye kichwa cha habari “Polisi na Hofu ya Watawala Kuondoka Madarakani”, ilichapishwa na gazeti hilo jana.
Chanzo: Mwananchi