Mwandishi wa Mwananchi Elias Msuya aitwa Polisi kuhojiwa kwa makala "Polisi na Hofu ya Watawala"

Huu uchambuzi wa Elias Msuya sikuusoma jana. Ngoja niusome kwa makini sasa hivi. Asanteni polisi kwa kutuhamasisha.
Kweli Dunia ya Mungu Vitu vya mzungu.. Wadanganyika sasa ni waelevu na wanajiamini. Wanahitajika waandishi Jasiri kama hao. Naahidi kumwekea mawakili 17.
 
Haya maneno "uchochezi, uvunjifu wa amani" nk nayasikia sana yakitumiwa na serikali kukamata na kushitaki watu. Hivi mkuu ni nani kachochewa? Na baada ya kuchochewa amefanya nini cha kuvunja amani na utulivu? Hivi wananchi wa leo na elimu na akili zote walizo nazo bado mnafikiri ni watu wa kuchochewa kwamba hawawezi kufikiri na kutafakari wao wenyewe? Hili neno linatumika vibaya kubinya uhuru wa watu kujieleza. Vinginevyo toeni mifano ya watu waliochochewa na kuwa baada ya kuchochewa walifanya nini? Ni kama hilo neno "intelijensia" Hilo nalo limekuwa fasheni ya polisi kuzuia uhuru wa watu kukusanyika na kubadilishana mawazo au kujieleza. Utasikia eti mkutano umezuiwa au maandamano yamezuiwa kutoka na kupata habari za "kiintelijensia" Sasa kama umepata habari za kiintelijensia si ndiyo itakuwa vizuri kuwakamata hao watakaosababisa vurugu na kuwaacha wale wasio kuwa na shida kuendelea na mkutano wao? Mbona CCM wanamkutano 23 na polisi wamejazana Dodoma ili kukabiliana na wale watakoleta fujo na hii huenda ni baada ya kupata taarifa za kiintelijensia. Sasa jiulize kwanini hawazuii mkutano wa CCM kutokana na taarifa za kiintelijensia kuwa BAVICHA wamepanga kuwasaidia wao kuzuia mkutano wa CCM badala yake wao polisi ndio wamejazana kuulinda ni kwanini wasijazane pia kulinda mikusanyiko ya wapinzani kama wafanyavyo ya CCM baada ya kupata taarifa hizo hizo za kiintlijensia?! Ngumu kuelewa!

Tulimumu. umeandika vizuri sana...sisemi hivyo kwa unafiki. bali kwa dhati kabisa...lugha yako pia ni ya ustaarabu mkubwa kinyume na wengi wanaodhani dola inawakandamiza....congratulations... Umegusia suala la intelijensia ninavyoelewa mimi kwa uzoefu wangu intelijensia ni neno pana...linaweza kumananisha taarifa kutokana kwa sources mbalimbali wakiwemo wachambuzi na hata polisi wenyewe wanaofanya kazi kwa siri ndani ya jamii...lakini pia maana yake nyingine ni uchambuzi wa issue yenyewe unaofanywa na polisi wenyewe kwa kuzingatia uzoefu, taaluma na mafunzo yao, kwamba suala hili likifanyika matokeo yake yatakuwa hivi na vile kwa hiyo polisi tufanye hivi...

Neno uchochezi maana yake pia ni pana...unaweza ukaandika makala yenye mwelekeo wa propaganda kwa lengo la kuwashawishi watu...ukisemas na kuandika kuwa kiongozi Fulani ni dikteta na bila kuthibitisha udikteta wake na kwa kufanya hivyo ukiwa na lengo la kiitikadi au kisiasa, huo pia ni uchochezi kwa maana unahamasisha jamii imchukie kiongozi huyo au mamlaka...

Sheria ile ya magazeti kwa maana ya Newspaper Act ya 1976 imeweka wazi ni maana ya uchochezi lakini hata Penal code imeainisha vipengele kuhusu masuala haya pamoja na masuala ya uhaini....

Uchochezi kwa hakika limelezwa wazi katika sheria zetu za nchi....lakini kinachojitokeza ni kuwa wananchi wengi hawajui sheria...lakini ignorance of the law is no defence...

Polisi wanalazimika kuweka tahadhari kuhsiana na mkutano wa CCM kwa sababu baadhi ya Wana-CHADEMA wanasema watajaza huko Dodoma kwa kile wanachoita eti 'kuisaidia' polisi kuzuia mkutano wa CCM...Wana-CHADEMA wametangaza publicly kuwa vijana wapatao 5,000 watakuwa huko Dodoma kuzuia mkutano huo...Sasa polisi hawawezi kupuuza habari hizi...CCM nao wanasema kuwa hao sijui BAVICHA na waje huko Dodoma kwani wataona cha mtemakun... Ni wazi polisi hawawezi kupuuzia 'majigambo' hayo ya pande zote mbili kwa hiyo lazima waweke ulinzi kwani uongozi wa nchi utakuwa kule...Mikutano ya CCM mara nyingi huwa inakuwa na amani isiyohitaji usimamizi wa polisi wengi...lakini safari hii lazima polisi wawepo kwa kuwa 'wajivuni' wa CHADEMA wanataka kuleta fujo...
 
Kaka ungeisoma kwanza halafu uandike. Kwa sababu unaongelea kitu ambacho hukijui/hujakiona na unatoa conclusion na kuchukua msimamo hiyo si sawa.

Nashukuru...nimesoma na kuielewa...mimi nimesema uchochezi kwa huyu aliyeandika kuwa nusu ya watanzania tutaishia magerezani na siyo ile makala...makala ile nimeisoma na kuielewa, siyo mbaya sana isipokuwa tatizo la ile feature/news analysis haikuwa edited, ina makosa mengi ya kiuandishi na imejaa generalization...I am writing this from a professional point of view. Lakini yule aliyetoa comment humu JF kuwa nusu ya watanzania tutaishia magerezani na kwamba magereza mengi itabidi yajengwe ni alarmist na mchochezi kwa kuwa hakuna ukweli huo wa nusu ya Watanzania (25 milioni) tuishie magerezani...uandishi wa aina ile ni kuhamasisha watu waichukie serikali.
 
Baadhi yetu hatukubaliani na wewe...kauli yako hapa ni ya uchochezi...ni aina ya watu ambao mnaleta hoja halafu yakitokea mnaingia mitini...ni uongo kusema nusu ya watanzania watamalizikia kwenye magereza, hii ni kauli ya uchochezi na isiyo na ukweli wowote...umekuwa 'alarmist' kwa issues ambazo ni za kawaida...sasa hivi naanza kuisoma makala hiyo, ili name nione ni kwa vipi imefanya hao Ndugu zetu waitwe na polisi, lakini ni 'uongo' kuanza kubashiri kuwa nusu ya watanzania wataishia magerezani..

kubashiri=kutabiri, kudhani,
 
Haya maneno "uchochezi, uvunjifu wa amani" nk nayasikia sana yakitumiwa na serikali kukamata na kushitaki watu. Hivi mkuu ni nani kachochewa? Na baada ya kuchochewa amefanya nini cha kuvunja amani na utulivu? Hivi wananchi wa leo na elimu na akili zote walizo nazo bado mnafikiri ni watu wa kuchochewa kwamba hawawezi kufikiri na kutafakari wao wenyewe? Hili neno linatumika vibaya kubinya uhuru wa watu kujieleza. Vinginevyo toeni mifano ya watu waliochochewa na kuwa baada ya kuchochewa walifanya nini? Ni kama hilo neno "intelijensia" Hilo nalo limekuwa fasheni ya polisi kuzuia uhuru wa watu kukusanyika na kubadilishana mawazo au kujieleza. Utasikia eti mkutano umezuiwa au maandamano yamezuiwa kutoka na kupata habari za "kiintelijensia" Sasa kama umepata habari za kiintelijensia si ndiyo itakuwa vizuri kuwakamata hao watakaosababisa vurugu na kuwaacha wale wasio kuwa na shida kuendelea na mkutano wao? Mbona CCM wanamkutano 23 na polisi wamejazana Dodoma ili kukabiliana na wale watakoleta fujo na hii huenda ni baada ya kupata taarifa za kiintelijensia. Sasa jiulize kwanini hawazuii mkutano wa CCM kutokana na taarifa za kiintelijensia kuwa BAVICHA wamepanga kuwasaidia wao kuzuia mkutano wa CCM badala yake wao polisi ndio wamejazana kuulinda ni kwanini wasijazane pia kulinda mikusanyiko ya wapinzani kama wafanyavyo ya CCM baada ya kupata taarifa hizo hizo za kiintlijensia?! Ngumu kuelewa!

Ngoja nione 1954 atakavyokujibu
 
Tulimumu. umeandika vizuri sana...sisemi hivyo kwa unafiki. bali kwa dhati kabisa...lugha yako pia ni ya ustaarabu mkubwa kinyume na wengi wanaodhani dola inawakandamiza....congratulations... Umegusia suala la intelijensia ninavyoelewa mimi kwa uzoefu wangu intelijensia ni neno pana...linaweza kumananisha taarifa kutokana kwa sources mbalimbali wakiwemo wachambuzi na hata polisi wenyewe wanaofanya kazi kwa siri ndani ya jamii...lakini pia maana yake nyingine ni uchambuzi wa issue yenyewe unaofanywa na polisi wenyewe kwa kuzingatia uzoefu, taaluma na mafunzo yao, kwamba suala hili likifanyika matokeo yake yatakuwa hivi na vile kwa hiyo polisi tufanye hivi...

Neno uchochezi maana yake pia ni pana...unaweza ukaandika makala yenye mwelekeo wa propaganda kwa lengo la kuwashawishi watu...ukisemas na kuandika kuwa kiongozi Fulani ni dikteta na bila kuthibitisha udikteta wake na kwa kufanya hivyo ukiwa na lengo la kiitikadi au kisiasa, huo pia ni uchochezi kwa maana unahamasisha jamii imchukie kiongozi huyo au mamlaka...

Sheria ile ya magazeti kwa maana ya Newspaper Act ya 1976 imeweka wazi ni maana ya uchochezi lakini hata Penal code imeainisha vipengele kuhusu masuala haya pamoja na masuala ya uhaini....

Uchochezi kwa hakika limelezwa wazi katika sheria zetu za nchi....lakini kinachojitokeza ni kuwa wananchi wengi hawajui sheria...lakini ignorance of the law is no defence...

Polisi wanalazimika kuweka tahadhari kuhsiana na mkutano wa CCM kwa sababu baadhi ya Wana-CHADEMA wanasema watajaza huko Dodoma kwa kile wanachoita eti 'kuisaidia' polisi kuzuia mkutano wa CCM...Wana-CHADEMA wametangaza publicly kuwa vijana wapatao 5,000 watakuwa huko Dodoma kuzuia mkutano huo...Sasa polisi hawawezi kupuuza habari hizi...CCM nao wanasema kuwa hao sijui BAVICHA na waje huko Dodoma kwani wataona cha mtemakun... Ni wazi polisi hawawezi kupuuzia 'majigambo' hayo ya pande zote mbili kwa hiyo lazima waweke ulinzi kwani uongozi wa nchi utakuwa kule...Mikutano ya CCM mara nyingi huwa inakuwa na amani isiyohitaji usimamizi wa polisi wengi...lakini safari hii lazima polisi wawepo kwa kuwa 'wajivuni' wa CHADEMA wanataka kuleta fujo...

Sheria ya uchochezi ililetwa na wakoloni, ikarithiwa hivyo hivyo kutoka India. Ililetwa na wakoloni kuwakandamizi kuwadhibiti watawaliwa / waafrika wasidai uhuru / haki zao hata pale wanapoonewa. Nyerere aliwahi kusema hatukudai uhuru ili kubadirisha mirija ya unyonyaji kutoka kwa wakoloni weupe na kuiweka kwa wakoloni weusi
 
Ifike mahala wahariri mue na nidhamu kwa taifa lenu.
Kupotosha ili gazeti liuzwe haikubariki.
Itafika mahala tuwe kama China ili nchi isonge mbele.
Kuweka korodani mezani Kisha kubonda kwa kilo ya uzito wa kilo kumi, yasambae ndipo tutaheshimiana.
 
Wangeandika police waua majambazi alafu sio kweli wasingeitwa, hii ina maana kuwa police wanataka tu ziandikwe magazetini habari za kuwasifia tu hata kama ni za uongo, hivo hivo kwa mheshimiwa MTUKUFU
 
mmmhhhh huku tulipofikia ni bora tujadili singeli maana tutafungwa wengi hasa sisi wazee wa barza za gahwa
 
Ukweli unauma sana.Serikali baada ya MADAWATI itayarishe na kujenga magereza,maana kwa mwendo huu nusu ya watanzania watmalizikia huko.
Huku tulipofikia tunatakiwa tujadili mambo ya diamond na wema na mipira tu maana haya ya siasa ni treason duuh
 
NINAFURAHA SANA MOYONI KWANI PANAPO MAJALIWA 2020 TUTAWAONDOA SWISMSWISM KILAINI SANA NA KAZI NI NYEPESI LAINI KAMA MAINI.
TUOMBEANE UZIMA TU..............
 
Back
Top Bottom