Mwandishi aliyeandika taarifa ya Waziri Mchengerwa kuhama Wizara ya Utalii na gari ya TANAPA aitwa polisi

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Mwandishi wa Habari, Charles Mulinda ambaye anadaiwa kuandika habari kuhusu madai ya Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa kukaa na gari la mradi uliopo chini ya mamlaka ya hifadhi za Taifa (TANAPA) kinyume na utaratibu anadaiwa kuitwa kituo cha Polisi pamoja na kwenye Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kitengo cha 'Cyber' ambacho ushughulika na makosa ya kimtandao.

Mwandishi huyo amesema kuwa mara baada taarifa hiyo kuchapishwa amepokea simu tofauti zikimtaka kulipoti kwenye mamlaka hizo, ambapo leo Septemba 29, 2022 saa mbili asubuhi ametakiwa kufika kituo cha polisi kati Jijini Dar es salaam licha ya kutoelezwa sababu ya kuitwa.

Akifafanua kuhusu taarifa hiyo amesema kuwa kabla ya kuichapa walizingatia misingi ya habari kuiandaa, ambapo ametaja gari hilo kuwa ni Nissan Patrol Wagon lenye namba za usajili 02JU0480 ambalo lilitolewa kwa msaada na Taasisi ya Frankfurt Zoological Society (FZDS) kwa TANAPA ili kutumika kwenye mradi.

Amefafanua "Sisi tulipata 'tip' ya stori ya gari la TANAPA tukaifuatilia kama wanahabari tukaandika stori baada ya kuhakikisha imekaa kihabari imekamilika pande zote. Baada ya kuandika habari nikapata wito kutoka Cyber na TCRA, Cyber nao wana kitengo chao pale TCRA nyuma, tulienda pale tukaambiwa aliyetuita kaenda Morogoro lakini yeye alitwambia kaenda Kibaha tulipoongea nae kwa simu ya mwenzake pale ofisini."

"Leo majira ya saa nne (jana) asubuhi nimepokea simu kutoka Central wakaniambia wananihitaji iwezekanavyo mapema kesho saa mbili asubuhi (leo), sijaambiwa ni kwa ajili ya nini wamesema tuonane saa mbili.

Akieleza kuhusu habari hiyo amesema walipata ukweli kuwa Waziri Mchengerwa ambaye awali alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii amekaa na gali hiyo kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu .

Amesema kuwa Afisa Habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii aliyemtaja kwa jina la Mapepere licha kukanusha taarifa hizo zilizochapishwa kuhusu madai ya gari hilo kuwa mikononi mwa Waziri, amedai awali nae akiwa ni kati ya vyanzo vya taarifa hiyo aliwathibitishia kuwa gari hilo lipo mikononi mwa Waziri Mchengerwa.

"Moja ya maafisa wa Wizara mwanzo kabla ya kutoa tamko la kukanusha alituthibishia kwamba hili jambo ni kweli Waziri gari alilichukuliwa na analo. Tunajua sio vizuri kuweka wazi vyanzo lakini kwa kuwa huyu mwanzo alithibitisha na baadaye tunaona anakanusha ndio maana nasisi tunalazimika kueleza hivi."

Aidha, amedai kwa taarifa walizozipata ni waliojichukulia magari nje ya utaratibu sio Waziri Mchengerwa tu, amedai kwa taarifa walizonazo baadhi ya viongozi au maafisa wa Serikali ngazi za juu wamekuwa na tabia ya kuchukua gari wanazodhani ni nzuri zaidi kwenye baadhi ya Taasisi ambazo zipo ndani ya Wizara zao wakati wanapokuta maeneo waliyopangiwa hayana gari nzuri kama wanavyotaka.

Amesisitiza "Habari aina chembe chembe ya uongo na hatuna dhamira ya kumchafua yeyote" lakini amesema haki na taratibu zikifuatwa ukweli wa jambo hilo utajulikana.

Hata hivyo amesema katika kutaka kuthibitisha ukweli wa suala habari hiyo katika hatua za kuiandaa walimpigia Waziri Mchengerwa lakini hakupokea simu na walilazimika kumtumia maswali kwa njia ya ujumbe ambapo wamedai aliufungua lakini hakujibu chochote.

Itakumbukuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan mwishoni mwa Mwezi Agosti 2023 alifanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri ambapo alimteua aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi. Ambao kwa sasa Wizara hiyo hipo chini ya Waziri Angela Kairuki.
 
Baada ya kupata taarifa je mwandishi alimtafuta mheshimiwa kupata ufafanuzi zaidi
Kwann ampigie simu.... Hii itakuwq sio tena uhandishi wa habari.. Ila itakuwa ni uoga..

Kama aliona na ana uthibitisho hakuna haja kupata ,kupata ruhusa kwa muhusikaaa
 
Kuna vitu vidogo sana ambavo waandishi wanadili navo kuliko vya msingi, that's why bongo hii mwandishi ambae ninayemjua na kumfuatilia yupo conscious and very aware na tasnia yake ni Pascal mayalla pekee. Waandishi wengi wa habari kanjanja na Hawana uelewa Mpana wa mambo.
 
Back
Top Bottom