Bishop Hiluka
R I P
- Aug 12, 2011
- 7,150
- 14,724
SIKUWAHI kabisa kuwaza kwamba ofisi yangu, ambayo mwenyewe nilipenda kuiita studio, ingeweza kuwa na kiza cha kutisha kiasi kile na hata kufikia hatua ya kunifanya kupagawa na kuogopa mno, mpaka lilipotokea la kutokea katika siku moja majira ya saa sita usiku. Ulikuwa ni usiku ambao sitausahau na ndio maana niliamua kuubatiza jina la Usiku wa kizaazaa!
Kwanza nilidhani labda nilikuwa kwenye usingizi wa mang’amung’amu kwa sababu ya pilikapilika nyingi za kutwa nzima ya siku hiyo zilizokuwa zimenichosha na kunifanya kupitiwa na usingizi, na kwamba yote yaliyokuwa yakitokea yalitendeka wakati nikiwa nipo ndotoni, hivyo, jinamizi la ndoto mbaya isiyoeleweka lilikuwa linanisumbua ndotoni.
Hali ile ikasababisha jasho jepesi lianze kunitoka sehemu mbalimbali za mwili wangu, huku nikihisi ubaridi fulani wa woga wa aina yake ukinitambaa mwilini na mapigo ya moyo wangu yakibadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida!
Wakati nikiwa katika hali ile mara hisia zangu zikanitanabaisha kuwa ile haikuwa ndoto bali ni kitu halisi kilikuwa kinatokea muda huo ndani ya studio yangu. Hisia za tukio lile zikasababisha koo langu likauke ghafla huku nywele zangu zikinisimama kichwani kwa hofu.
Hata hivyo, mara hii milango yangu ya fahamu ilikuwa makini zaidi huku nikijaribu kuishirikisha akili yangu kikamilifu katika kuniletea taarifa za kuaminika ili kujaribu kubaini endapo tukio lile lilikuwa katika mlolongo wa yale matukio ya ndotoni au la!
Nilianza kusikia sauti za ajabu ajabu sana zisizoelezeka ambazo zilikuwa zinasikika kwa fujo pasipo mpangilio kutoka katika kila pembe ya chumba kile na kugeuka kero kubwa masikioni mwangu. Hatimaye niliyakodoa macho yangu kwa hofu huku nikiyatembeza mle studio kutazama huku na kule, na hapo nikakutana na ukungu wa giza nene machoni mwangu.
Hali ile ikanifanya niyatulize vizuri mawazo yangu huku nikijaribu kufikiria vizuri kama ni kweli nilikuwa ndani ya studio yangu au nilikuwa sehemu nyingine ambayo ni tofauti kabisa na studio yangu. Kama ningekuwa mlevi ningeweza kusema labda pombe ya siku hiyo ilikuwa imechanganywa na kemikali au ilikuwa kali kupindukia. Lakini wapi!
Swali kubwa lililonijia kichwani mwangu kwa wakati huo ni je, pale nilikuwa wapi? Sikupata jibu la haraka, hivyo nikaamua kupeleka mikono yangu huku na kule nikijaribu kupapasa ili kujipa uhakika wa wapi nilipokuwa, nilijikuta naigusa computer yangu, kisha nikaishika notebook yangu na vitu vingine vilivyokuwa mbele yangu juu ya meza yangu ya kiofisi. Kwa kufanya vile taratibu fahamu zangu zikaanza kurejewa na uhai.
Niligundua kuwa kumbe nilikuwa bado nimeketi kwenye kiti changu kirefu cha ngozi cha kiofisi ndani ya studio yangu na kwamba muda mfupi tu uliopita nilikuwa nafanya kazi kwenye computer yangu iliyokuwa mbele yangu juu ya meza.
Hali ile ikazidi kunichanganya sana! Sasa maswali zaidi yakazidi kuzunguka ndani ya kichwa changu, je, kama nilikuwa ndani ya studio yangu na muda mfupi tu uliopita nilikuwa nafanya kazi, ni nini basi kilikuwa kimenitokea? Je, ni ulikuwa ni mlolongo mrefu wa matukio ya ndotoni? Hapana… hii haikuwa ndoto! Na kama haikuwa ndoto ni nini basi kilikuwa kinaendelea?
“Hivi naota ama ni kweli?” nilijikuta nauliza kwa sauti yenye kitetemeshi kana kwamba kulikuwa na mtu mwingine ndani ya studio yangu niliyekusudia kumuuliza ili anipe uhakika kuwa sikuwa naota. Ili kuhakikisha kama kweli sikuwa naota nikajifinya kidogo kwenye mkono wangu wa kushoto ili nione kama nilikuwa mzima. Finya yangu ya woga ilinifanya nitumie nguvu kubwa na hivyo nilipata maumivu makali sana.
“Ooh shit!” niling’aka kwa sababu ya maumivu makali yaliyochanganyika na hasira.
“Hmm! Kwani saa hizi ni saa ngapi? Mbona…” niliwaza na kuyakatisha mawazo yangu, nikageuza shingo yangu kuangalia ukutani mahali ilipokuwa imetundikwa saa kubwa ndani ya studio lakini sikuweza kuona kitu bali ukungu wa giza nene ulitanda machoni mwangu.
Nikainua mkono wangu wa kulia ambao niliutumia kuvaa saa, nia ilikuwa kuitazama saa yangu ya mkononi aina ya Hublot Big Bang Ferrari King Gold niliyoiagiza kutoka Dubai kwa dola za Marekani 43,600, sikuona kitu badala yake nilishangazwa kuona kuwa bado ukungu wa giza nene ulikuwa umetanda machoni mwangu. Nikachanganyikiwa maana sasa sikujua tatizo lilikuwa ni nini, macho yangu yalikuwa yamepofuka au giza lilikuwa limetanda ndani ya studio!
“Hapa ni kujikakamua, mimi mtoto wa kiume, sitakiwi kupoteza tumaini kipumbafu hivi,” nilijisemea huku nikijaribu kuinuka lakini nguvu fulani kama sumaku ilinirudisha kwenye kiti. Sikukata tamaa nikapapasa juu ya meza na kuchukua simu yangu aina ya Sumsung Galaxy S7 na kuiwasha tochi ili nione, cha ajabu nayo haikutoa mwanga!
“Oh my God! Inamaana nimeshakuwa kipofu!” nilijikuta nasema kwa huzuni huku nikijitahidi kuyakodoa macho yangu yaliyoona ukungu wa giza nene mbele yangu, nikiwa na hofu kubwa…
Naitwa Maximillian Njamba, maarufu kwa jina la ‘Sauti ya Jamii’, jina nililopewa na jamii yangu, hasa kwa sababu ya kazi nzuri niliyokuwa nikiifanya ya kuisemea jamii yangu, kazi ya uandishi wa makala zilizofanyiwa uchunguzi wa kina kwenye gazeti la Rindima. Gazeti la kila siku ambalo pia nilikuwa mhariri wa makala.
Itaendelea…