Mwandishi Richard Masatu ameuawa!

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
263
Kutoka katika Facebooka ya Frederick Katulanda Tarehe Jumatano, Agosti 10, 2011 saa 2:43 mchana: Kumeandikwa hivi:



TANZIA: Imenichukua muda kuamini, pengine hii ndiyo sababu ya kuchelewa kuwafahamisha kuwa Tasnia ya Habari Mwanza imepata pigo kubwa baada ya Mwandishi Richard Masatu ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Gazeti la KASI MPYA kufariki Dunia akiwa anapatiwa Matibabu katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure.

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Marehemu amekufa kutokana na majeraha ya kushambuliwa na watu wasiojulikana. Kwa sasa mwili wake upo Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa Uchunguzi kutokana na kukutwa na majeraha ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali, chini ya Kidevu, jicho la kulia ikiwa na kupigwa na kitu kizito usoni upande wa kushoto.
 
Rip mr Masatu ila uchunguzi ufanyike maana inavyoonekana kauliwa lazima waliohusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria
 
R.i.p masatu jamani kisa ni nini??au ndio utajiri maana huko kuuwana waongeze mabasi ,mahotel kazi rahisi sana
mola mrehemu aliko
 
Ri Masatu ila uchunguzi ufanyike maana inavyoonekana kauliwa lazima haki itafutwe

haki iko mbinguni my dear nimeshasimamia na kufwatilia mauwaji zaiidi ya 7 kwa waliouwa matokeoyake ni kupoteza Muda na ndio maana
wenye kusoma nyakati walaah Mungu amrehemu aliko
 
r i p richie mungu akulinde na akutoe huko uliko na akusamehe makosa yako amina!..
 
Rip Masatu.
Tunahitaji serikali mpya itakayowajali, kuwalinda na kuwahakikishia usalama wananchi wake.
 
r i p richie mungu akulinde na akutoe huko uliko na akusamehe makosa yako amina!..

angalia maombi mengine yanasikiwa asije tolewa MBINGUNI akapelekwa Jehanum jamani tumwachie Mola Amlinde alikko
 
Yote yana mwisho kisha na wao watakufa tuuuu, hakuna atakayepaa
 
RIP masatu. walisababisha hiyo wote wakatubu vinginevyo damu ya mtu haiendi bure. Mungu akulaze mahala pema peponi AMEN.
 
Back
Top Bottom