Mwandishi Mayage S. Mayage umepotoka hatudanganyiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandishi Mayage S. Mayage umepotoka hatudanganyiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Dec 7, 2011.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wana JF niliwahi kusema huko nyuma kuwa Gazeti la Raia Mwema huko tuendako ndio gazeti litakalo tumika kukiangamiza chama cha CHADEMA. Nimesoma makala ya leo kwenye gazeti hili ya Mayage S. Mayage nimegundua pasipo shaka kuwa Mwandishi huyu alitoka kule alikokuwa na kuandika makala za mwanzo za kuisifia chadema ili kuwavuta wasomaji na hasa wapenzi wa Chadema ili baadaye afanye kazi anayoifanya sasa hivi ya kukibomoa.

  Mayage katika makala yake ya leo anasema hajaona chama mabadala wa CCM na anashauri kuanzishwe chama kipya badala ya hivi vilivyopo yeye anavilinganisha na NGOs , mimi namshangaa Mwandishi huyu anayejiona mahiri mimi nammuno ni mjinga tena asiyejiamini kama yeye hajaona vyama mbadala wa CCM kwa nini asianzishe yeye chama chake kwa malengo hayo, anakazana kusema hajaona chama kianzishwe kipya anasubiri nani amwanzishie chama kitakacho kuwa mbadala, nani anafikiri atamwanzishaia chama cha kuendana na matakwa yake kama si yeye mwenyewe.

  hapo tukisema umetumwa utasema tunakusingizia. Mimi nimshauri kuwa hana haki ya kufikiri kwa niaba yetu yeye kama anafikiri chama mabadala wa CCM bado asubiri hao anaofikiri watamwanzishia chama siyo kulalamika hakuna chama, sisi wenzio tumeshamwona mbadala wa CCM wala hatuhitaji kuambiwa na mtu mwenye macho haambiwi tazama. Nimshauri pia Dr Slaa asiangaike kujibu watu kama hawa lengo lao mbona linfahamika ni kuivuruga Chadema kabla ya 2015.
   
 2. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hili ndilo tatizo kubwa tulilonalo wana CDM!!jana kuna mada nilichangia!nikatoa hoja kwamba tuna ombwe la uongozi pale juu na kwa kuwa chama bado kipo katika fikra za waanzilishi!na mwenyekiti wetu kwa uongozi wake ameshindwa kukitoa kwenye fikra hizo!!

  Na nikainisha mambo mengi!na mwishowe nikasema M wenyekiti mbowe hakuna namna ni lazima atoke kwa ustawi wa chadema na kwa maendeleo ya chama!!!

  Nikatukanwa,nikadharirishwa sana na wanachadema wenzangu ambao mimi sijui chama chochote cha siasa zaid ya chadema,mbaya zaid nimeanza piga kura 95 nikiwa si mwanachama wa chama chocote! Na nilipiga hata umri haujatimia!!!

  Na nilijiunga chadema yapata miaka 2 iliyopita!!!ila chadema pale juu kuna mapungufu !!tutake tusitake!!na huo ndio ukweli!!!Mbowe ni muhimu aondoke!
   
 3. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  Asitulazimishe tufanye anayoyataka , sisi tumeamua kukiunga mkono chadema kwa ajili ya ukombozi wetu .......wasioupande tunawajua na ipo siku wataficha sura zao kwa aibu
   
 4. M

  Malova JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  huyu mtu anabahati mbaya sana kwa kufikiri kwake kwa staili ya msemo wa msaburi "kwa kutumia makalio" kwasababu anaowaambia huwa hawaendeshwi kwa hisia. wanaanalyse mambo ndipo wanachukua hatua. mpe pole sana
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Nenda CCM huko matakwa yako yatatimia. Chadema hakuna atakayesikiliza ujinga wako.
  Mbowe bado ni kiongozi safi hata ccm mnafahamu.

  Narudia kusema tena nenda ccm waliokutuma. Kwetu Chadema haatukubaliani na mawazo ya kijinga kama nyie mnavyosikiliza mawazo ya kijinga ya wakina nape nyauye
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Nilichofurahia katika hoja yako na maneno yako mengi ni moja. Kwamba mwandishi kama anaona hapajawa na Chama mbadala ya CCM na anataka watu waanzishe Chama mbadala ya CCM yeye angekuwa wa kwanza kufanya hivyo badala ya kutoa maagizo katika ombwe.

  Asante sana.
   
 7. only83

  only83 JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kujua kuandika na kuongea sio sifa ya kuwa mwandishi wa habari......tumsamehe bure!!!
   
 8. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hili ndilo tatizo kubwa! Kila anayekuja na hoja ya udhaifu uliopo CDM anadhaniwa kuwa ni CCM!!!WAPENDWA haya ni katika kujenga chama!!!

  Mguu tulionza nao sio sahihi!!wananchi wamechoka,nasi twatumia nafasi hiyo kuona kila jambo tulifanyalo ni sahihi!!!ok wengine tuna mawazo ya kipumbavu!!ila mkumbuke kisemwecho sahihi ata tufanyeje,tupinge kitajidhirisha tu! Ni suala la muda!!na ngoja tuone! 2015 si mbali!
   
 9. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Huyo jamaa kama vipi awasubiri wajinga wenzie wanaofikiria kama Bi Mkora wa mjengoni ndo washawishiane, CHADEMA kwa mifano halisi kimeonyesha kuwa ni chama kinachoweza kuichukua hii nchi na hao Mafisadi wake waliomtuma wakatafuta pa kutokea.Muulizeni kilichomtoa Habari Corpoaration ni nini,, kama sio njaa,sasa anakuja kwenye magazeti ya magreat thinker anamwaga upupu,tumuacheni tu huyo cause siku ya siku atakuja tafuta pa kuifichia hiyo sura yake.
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mayage anatoa maoni yake kama mtu mwwenye uhuru wa kusema kile anachokiamini lakini wewe unamuona kuwa amepotoka. na wewe hapa unatoa maoni yako kama mtu mwenye uhuru wa kutoa maoni yako, kwa nini tusikuone na wewe kuwa umepotoka kwa sababub unachokifanya ni sawa na kile alichokifanya Mayage?
   
 11. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  excellent!!!!!!!mimi ni people"s power!!!lakini bado haijageuka na kuwa bangi kwangu!!!!tudiscusss!!tuache matusi!!!!tudiscusss kwa hoja!!!!
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,511
  Trophy Points: 280
  ntogwisangu, kumbe wewe ni mwanachama kama ulivyosema, hivyo huko kwenye chama chenu, hakuna taratibu za ukosoaji?.
  Nilitumaini wewe kama mwanachama mwaminifu wa Chadema, utatumia njia sahihi za ukosoaji na sio kumwaga mtama hapa kwenye kuku wengi!.

  Ukosoaji wa wazi, mtuachie sisi tusio na vyama!
   
 13. S

  SHIMBONONI Senior Member

  #13
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kama mwandishi Mayage S.Mayaye ni 'chakula cha wajanja' tusimlaumu sana sbb anaishi na kufanya kazi kwa kutegemea maelekezo ya wanaomtumia.
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Asante kwa kunielewa Pasco. kama yeye aliudhiwa na hoja, angezijibu kwa hoja, si kuanza kumwandama mtoa hoja
   
 15. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mimi nataka kuanzisha chama namwomba mayage s mayage aje awe mwenyekiti ili tuweze kuitoa ccm madarakani.
  kwa maelezo zaidi ani pm.
   
 16. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  hakika napenda vitu vizuri kama hiki!!ni kweli nikiwa kama mwanachama sipaswi kuyasema haya katika mazingira kama haya!!sasa labda tatizo lipo wapi sasa?na hapa ndipo hoja yangu ya msingi inapoanzia!!!chama kimeshindwa kabisa kuweka taratibu ambazo mwanachama anakuwa na authority ya kujiona mwanachama!!!chukulia mfano mimi nahishi mjini!kata yangu inaongozwa na chadema!!!haya yote nilishaongea na watu wengi wa huku chini ambao ni viongozi wa chadema!!!!hawakupi taratibu ya kuyafikisha malalamiko haya sehemu husika!!!na kukupa matumaini ya majibu yake!!mwishowe mnabaki kupingana na mwenyekiti wako wa tawi!!ana suluhisho la matatizo yako!!!NA HAPO NDIPO HOJA INAKUJA KAMANDA MBOWE YATOSHA SASA!!!!!TUWAPE WENGINE NAFS KWA BUSARA NA UNYENYEKEVU!!!SI WIVU,SI UNAFIKI!!NDO UHALISIA!!!!!
   
 17. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mbona huzungumzii waliokujibu? hilo ombwe la uongozi ni lipi lisokuwa na uchambuzi wa kutosha? mafanikio haya ya cdm yametokana na uongozi upi kiasi kwamba uliopo ni ombwe? Nikushauri jambo moja tu.. kama unakipenda chama ainisha kasoro zilizoko za kiuongozi na mafanikio yaliyopatikana kupitia huo uongozi kisha pendekeza
  dira mpya na aina ya viongozi unaofikiri wanaweza kutufikisha kwenye malengo yako.

  Ila kwakifupi sana nikwambie tu Mbowe, Slaa, Zitto, Mnyika, Mdee na wengineo ni matatizo makubwa sana kwa ccm, wanatamani hata leo wafutike.. siasa za nchi yetu chini ya serikali ya ccm zinataka viongozi jasiri kwa tukio lolote la kinyanyasaji na hili ndilo lililopo kwa cdm.
   
 18. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  katika hao uliowataja kwangu kwa sasa labda mnyika na mdee na slaa,hao wengine hapana!!!
   
 19. L

  Luiz JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe ndio mwenye mapungufu kujiunga kwako na chadema mapema ndio kuclete matatizo ndani ya chama ucpende kutumika dogo chama kina taratibu na kanuni zake huo ni mtizamo wako wewe ndio unaleta matatizo ndani ya chama na unafiki wako.
   
 20. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  CDM watafakari kwa kina suggestions zinazotolewa
   
Loading...