Ombwe dhahiri, mbadala wa CCM ni chama kipya
Mayage S. Mayage
MAKALA zangu mbili katika matoleo mawili yaliyopita ya gazeti hili zimeniunganisha kwa karibu katika pembe tatu; kwa maana ya mimi binafsi, wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na mtendaji wa mkuu chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa.
Hata hivyo, katika muunganisho huo, wengi na hasa wapenzi wa CHADEMA, hawakufurahishwa na ujumbe mfupi (sms) niliotumiwa na Dk. Slaa, akiponda ushauri wangu kwa chama hicho wa kujikita zaidi katika kufanya siasa badala ya kutumia muda mwingi kuendesha uanaharakati wa maandamano, nikijenga hoja kwamba 2015 si mbali, wabunge wa CHADEMA wanatakiwa kuja na programu za maendeleo kwa wananchi wa majimbo yao ili yasije yakakikuta yaliyokikuta chama cha
NCCR-Mageuzi mwaka 2000.
Kwa kuwa wasomaji wangu wengi, katika kunipa pole kuhusu ujumbe huo wa Dk. Slaa wakiniomba nisikate tamaa kuendelea kutoa ushauri kwa chama hicho kipenzi cha Watanzania wamejaribu pia kuwasiliana moja kwa moja na Dk. Slaa ili kujiridhisha kama kweli ujumbe ule ni wake, na kama kweli ule ndio mtazamo na majibu yake kwa ushauri wangu ule kwa chama chake, niwashukuru nyote mlioguswa kwa ujumla wenu na yote masuala hayo mawili na kufanya mawasiliano nami.
Hata hivyo, kabla ya kuanza mada yangu ya leo, niwaombe miongoni mwenu nyote mlioguswa na makala zote mbili zile, na lakini pia mkaguswa na ujumbe mfupi wa Dk. Slaa kwangu, niteue ujumbe mfupi (sms) wa msomaji mmoja, ambaye kwa kumfahamu kwangu naamini ni bado mtu mwenye fikra na maoni huru ambayo hayajaathiriwa na itikadi za siasa za vyama vyetu.
Msomaji wangu huyo, Absalom Kibanda, ambaye ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Freemedia, baada ya kupitia makala zangu zote mbili na pia kusoma mrejesho wa Dk. Slaa kwangu kwa makala ya wiki ile ya nyuma, alinitumia ujumbe huu: Kaka umefanya kazi kubwa. Katika hili, nadhani Dk. Slaa alihamaki bila sababu kwa kuwa hata kama ulichokiandika kilimkera kwa sababu zozote zile, iwe ni kwa upotoshaji au kupingana na mwenendo wa CHADEMA, bado alipaswa kuonyesha ustahimilivu na ukomavu wa kisiasa (0754 001010).
Baada ya utangulizi huo, niwaombe wasomaji wangu tuendelee na mada ya leo. Makala hii ya leo nimeiandika nikisukumwa na msomaji wangu mmoja katika makala ya wiki iliyopita. Msomaji huyo, baada ya kuyapitia maandishi yangu, alinitumia ujumbe ufuatao:- Habari ndugu mayage! Naitwa Deo Makilika, nipo safarini kuelekea IR (Iringa). Katika makala yako ndani ya Raia Mwema ya Nov 30-Dec 6, pg 22, inaonyesha umeanza ku-lose mwelekeo, hivi inawezekanaje kukosa chama mbadala cha kusimamia uzalendo katika nchi yenye wazalendo wengi?
Huu ni upotoshaji mkubwa, nashauri uwe unafanya utafiti wa kina kuliko kuandika kwa hisia au jumla jumla, utakuwa mwandishi mzuri sana. Kila la kheri! (0719 935250).
Katika makala yangu ya wiki iliyopita, iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho: Sababu tunayo, tuwangoe 2015, niliandika kwa kutoa ushauri kwa Watanzania wenzangu kuungana kwa pamoja ili kuuondoa na kuutupa baharini mfumo mzima wa utawala uliopo kwa sasa, kwa kuwa taasisi zake zote, katika matukio mawili tu ya sakata la Richmond na lile la aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, zimeonyesha zinausimamia na kuulinda kwa ustadi mkubwa mfumo wa rushwa na ufisadi uliotamalaki nchini.
Katika hilo, nilitoa ushauri kwa wazalendo wenye uchungu wa kweli wa namna utajiri na rasilimali za nchi hii zinavyotafunwa kifisadi, kuanzisha chama cha siasa makini sasa, si kusubiri kesho na Watanzania wakiunge mkono kwa nguvu zote, ili mwaka 2015 tuondokane na mfumo huu wa kulindana baada ya kamati teule mbili za Bunge letu, zilizochunguza suala la Richmond na Jairo kutufumbua macho juu ya hali halisi inayofanywa na watendaji wetu serikalini.
Hilo la kuwataka wazalendo wa kweli kuanzisha chama cha siasa makini cha kutuongoza Watanzania kuungoa mfumo wa sasa, ndilo lililomuudhi msomaji wangu Deo Makilika, anayeamini nimeanza ku-lose (kupoteza) mwelekeo na nimefanya upotoshaji mkubwa kwa ushauri wangu wa kuanzishwa chama mbadala cha kusimamia uzalendo na hivyo kuhoji; hivi inawezekanaje kukosa chama mbadala cha kusimamia uzalendo katika nchi yenye wazalendo wengi?
Naomba nimhakikishie ndugu yangu Deo na wasomaji wangu kwa ujumla wao kwamba sijaanza kupoteza mwelekeo. Kama Deo anaujua vizuri mwelekeo wangu, basi naomba aamini kwamba uko pale pale, haujatikiswa. Hata hivyo, napenda kumhakikishia kwa uwazi kabisa na bila shaka yoyote ndugu Deo kwamba kwa Mtanzania yeyote anayefuatilia siasa za nchi hii, hahitaji kufanya utafiti wowote ili kujua kuwa hadi sasa ninapoandika makala hii na inaposomwa na wasomaji wangu, ndani ya nchi hii, hatuna chama chochote mbadala cha kusimamia uzalendo huo tunaouhitaji Watanzania baada ya miaka mingi ya kunyonywa, kudhulumiwa na kuteswa na baadhi ya Watanzania wenzetu wachache waliokosa uzalendo kwa nchi yao kupitia mikataba mibovu ya umeme, madini na mingine mingi.
Najua wasomaji wangu watanishangaa kwa tamko langu hili la kusema hadi sasa hatuna chama cha siasa chochote ambacho ni mbadala wa CCM 2015 ili kituongoze katika kutupeleka kule ndoto yetu sote inakotuelekeza twende. Hadi sasa, tunavyo vyama 17 vya upinzani vyenye usajili wa kudumu. Baadhi ya vyama hivyo hata wanaoviongoza hawajulikani. Vyama hivyo ni pamoja na CHADEMA, CUF, TLP, NCCR-Mageuzi, UDP, NLD, NRA, TADEA, UPDP, MAKINI, FORD, CHAUSTA, DP, Jahazi Asilia, PPT-Maendeleo, SAU na UMD.
Nawaomba Watanzania tutoke nje ya ofisi au nyumba zetu kwenda kwa wananchi wenzetu tuwaulize vyama hivyo vinasimamia itikadi na sera gain? Tuwaulize ni chama gani kimeisimamia kwa ustadi hoja yake ya kuwakomboa Watanzania kutoka mikononi mwa madhila ya CCM kwa maendeleo ya nchi na watu wake kwa kauli na vitendo vinavyofanana na jinsi viongozi wao walivyo na wanavyoishi.
Najua wasomaji wangu hao watakaonishangaa, katika orodha hiyo ya vyama 17 vya upinzani watanishangaa kwa sababu imani yao iko katika CHADEMA na wanajua na kuamini kuwa ndicho chama mbadala kitakachokomesha ufisadi na mafisadi katika nchi hii na hivyo, kutufikisha kwenye Tanzania tunayoitaka.
Binafsi bado sijashawishika na chama hicho, na hasa baada ya kushindwa kusimamia hoja moja tu ya posho ya vikao kwa wabunge na watendaji serikalini, hoja ambayo kinasema imo ndani ya sera zake.
Ndugu zangu, katika mwelekeo na upepo unaoikumba dunia ya sasa, mabadiliko ya uongozi wa chama cha siasa ndani ya nchi yetu ni lazima. Tena basi, mabadiliko hayo yamerahisishwa na watawala wetu wa sasa pamoja na makada wa chama chao tawala kwa sasa. Ndiyo maana mara zote napoteza nguvu zangu kukishauri CHADEMA ambacho Watanzania wanaelekea kukiamini kuwa ni mbadala wa CCM, kitoke kwenye uanaharakati na kuingia kwenye siasa zinazotia matumaini na zenye lengo la kukamata dola na usimamizi thabiti wa vyombo vya dola kwa misingi ya kidola, na hivyo kuwaongoza wananchi kwa kuonyesha njia.
Ndani ya CHADEMA wapo wanasiasa wazuri tu, wanaofanya siasa kweli, lakini hao hawana sauti wala nafasi ya kukielekeza chama hicho ni ipi njia sahihi ya kufanya siasa. Wenye sauti na ushawishi (influence) ndani ya chama hicho ni wanaharakati hali inayokifanya chama hicho kuendeshwa kiharakati kwa asilimia 80 na asilimia 20 inayobaki ndiyo inayofanya shughuli za kisiasa.
Narudia tena kusema, fursa hii iliyopo kwa sasa ni tunu ya pekee kwa CHADEMA. Kimeingia Jimbo la Igunga kwa mara ya kwanza na ndani ya siku 28 tu, kimekubalika kwa zaidi ya asilimia 40. Hiyo tu ya Igunga, ilitosha kuwaelekeza viongozi wa CHADEMA ni dira gani ya kufuata ili mwelekeo huo wa wananchi wa Igunga uwe mwelekeo wa nchi nzima kuelekea 2015.
Badala yake, wanapoteza muda kulumbana kuhusu umeya wa Manispaa ya Arusha, kana kwamba bila umeya huo hakitakuwa na hadhi ya kisiasa. Wanapoteza muda wao kuzungumzia muswada na sheria mpya ya mabadiliko ya Katiba Mpya kana kwamba muswada na sheria hiyo ikiandikwa kwa utashi wao ndiyo itakayopiga kura mwaka 2015 na kukipeleka Ikulu.
Serikali na Rais wake, Jakaya Kikwete pamoja na chama chake, wamekubali kilio cha muda mrefu cha Watanzania kuwa na Katiba Mpya ya nchi. Binafsi, nilitaraji baadhi ya watu wetu weledi wa masuala ya Katiba, baadhi ya wanasiasa na hasa wa CHADEMA, wangekitumia kipindi hiki cha kuelekea uandishi wa Katiba Mpya, katika kufanya utafiti na udadisi wa ni Katiba ipi bora katika nchi za dunia hii, ili iwe mfano wa Katiba mpya tunayoitaka katika mazingira ya kijiogorafia, kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa Taifa letu.
Ndugu zangu, katika mazingira haya ya sasa ambayo Watanzania wamekata tamaa na kuishiwa kabisa matumaini ya kuendelea kutawaliwa na CCM, CHADEMA kinaonekana kuwa mbadala kwa kuwa katika udhaifu wa vyama vyote vya siasa vilivyopo, kinaonekana kuwa na unafuu wa udhaifu kuliko vingine. Lakini hiyo haitufanyi tusahau msemo wa kwamba hata katika msafara wa ndege aina ya bundi, lazima apatikane bundi wa kuwaongoza wenzao waliomo katika msafara huo.
Kwa upepo wa mabadiliko unaovuma duniani kwa sasa, na ambao Watanzania hatuna njia yoyote ile ya kuukwepa tukiwa chini ya utawala huu wa CCM ya aina ya sasa, inayoshindwa kuchukua hatua stahiki kwa mafisadi wanaoifisadi nchi yetu na kuendekeza urafiki na uswahiba katika masuala ya msingi ya uongozi wa nchi na yanayogusa uhai na uchumi wa Taifa letu, upepo huo unaweza kabisa kutusukumia mikononi mwa hata shetani au chama cha ovyo ili mradi tu kutimiza dhamira na nia yetu ya mabadiliko hayo.
Vyama vya siasa vya kambi ya upinzani tulivyonavyo, vipo na vilianzishwa kwa sababu ya fursa ya kikatiba. Vingi ya hivyo, vinafanya siasa za kubabaisha ili vionekane vipo kwa sababu vilisajiliwa kama vyama vya siasa. Hata viongozi wao wengi ni watu ambao huko nyuma walishindwa kuishi katika masharti na misingi ya uzalendo na utaifa enzi za chama kimoja na kujikuta wakitupwa nje ya mfumo, na hivyo walianzisha vyama vya siasa watakavyotumia kama jukwaa la kuwasema mahasimu wao hao wa zamani.
Nihitimishe makala yangu hii kwa kusema tunahitaji kuwa na chama cha siasa kitakachoanzishwa na kundi la watu linalochukizwa na mwenendo wa utawala wa chama kilichoko madarakani leo, ambao hautoi matumaini ya kuwaondolea Watanzania maadui wakuu watatu waliotangazwa miaka 50 iliyopita; ujinga, maradhi na umasikini.
Tunahitaji kuwa na chama cha siasa, kitakachoanzishwa na kundi la watu wenye uzalendo wa kweli kwa taifa lao, wanaoamini kwamba ardhi ya kutosha tunayo, siasa safi ambayo imeendelea kusimamia misingi ya amani na utulivu iliyowekwa na waasisi wa taifa letu tunayo, isipokuwa tumeshindwa kufika katika safari yetu kwa sababu tu tumekosa uongozi bora. Kwa hiyo, kuanzia sasa, tunahitaji kuwa na uongozi bora wa nchi, unaotokana na chama kipya bora cha siasa, kitakachoanzishwa na watu wenye dhamira hiyo katika nafsi zao.
Tulivyonavyo sasa, havina tufauti na NGOs tunazozijua. Ni vyama vya kutafuta fedha za ruzuku ndani na nje ya nchi, ili walau familia za wanaoviongoza ziishi maisha yanayofanana na familia za watawala wetu.
Ndiyo maana waliomo ndani ya vyama hivyo, wakikosa tu fursa ya ulaji, hukimbilia kuisaka fursa hiyo ndani ya vyama vingine ili tu wafanikishe ulaji. Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa wanasiasa aina ya Magale John Shibuda wanaweza kukubali kukifia chama chao cha sasa pindi ubunge utakapowaponyoka. Naomba kuwasilisha!
Ujinga wa MayageAnayebisha abishe lakini huyu bwana anamtumikia
- Mayage anakiri kuwa CHADEMA ni kipenzi cha watanzania halafu anasema binafsi yeye hakijamshawishi kuwa mbadala wa CCM. Kama kimeweza kuwa kipenzi cha watanzania waliowengi inawezekana hakijamshawishi yeye kutokana na upeo wake ndio maana mnaweza kuwa darasa moja mmoja anapata zero na mwingine division one uwezo wake wakuelewa mambo hawezi kutushawishi watanzania wengi waliowapenzi wa CHADEMA kama alivyokiri mwenyewe.
- Mayage anasema CHADEMA hakijamshawishi na wala si mbadala halafu bado anapoteza muda kukishauri huu si ujinga mwingine. Halafu anasema tena hii ni fursa pekee kwa CHADEMA kwa vipi wakati ameshauri kianzishwe chama kingine.
- Aliponiacho hoi zaidi ni hapo ni kuhusu Katiba, kwa maneno yake anasema, Binafsi, nilitaraji baadhi ya watu wetu weledi wa masuala ya Katiba, baadhi ya wanasiasa na hasa wa CHADEMA, wangekitumia kipindi hiki cha kuelekea uandishi wa Katiba Mpya, katika kufanya utafiti na udadisi wa ni Katiba ipi bora katika nchi za dunia hii, ili iwe mfano wa Katiba mpya tunayoitaka katika mazingira ya kijiogorafia, kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa Taifa letu.Unafanya utafiti wa nini halafu uupelekewapi wakati hakuna mfumo mzuri wa kupokea tafiti zako.
Nawasilisha hoja
Ombwe dhahiri, mbadala wa CCM ni chama kipya
Mayage S. Mayage
MAKALA zangu mbili katika matoleo mawili yaliyopita ya gazeti hili zimeniunganisha kwa karibu katika pembe tatu; kwa maana ya mimi binafsi, wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na mtendaji wa mkuu chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa.
Hata hivyo, katika muunganisho huo, wengi na hasa wapenzi wa CHADEMA, hawakufurahishwa na ujumbe mfupi (sms) niliotumiwa na Dk. Slaa, akiponda ushauri wangu kwa chama hicho wa kujikita zaidi katika kufanya siasa badala ya kutumia muda mwingi kuendesha uanaharakati wa maandamano, nikijenga hoja kwamba 2015 si mbali, wabunge wa CHADEMA wanatakiwa kuja na programu za maendeleo kwa wananchi wa majimbo yao ili yasije yakakikuta yaliyokikuta chama cha
NCCR-Mageuzi mwaka 2000.
Kwa kuwa wasomaji wangu wengi, katika kunipa pole kuhusu ujumbe huo wa Dk. Slaa wakiniomba nisikate tamaa kuendelea kutoa ushauri kwa chama hicho kipenzi cha Watanzania wamejaribu pia kuwasiliana moja kwa moja na Dk. Slaa ili kujiridhisha kama kweli ujumbe ule ni wake, na kama kweli ule ndio mtazamo na majibu yake kwa ushauri wangu ule kwa chama chake, niwashukuru nyote mlioguswa kwa ujumla wenu na yote masuala hayo mawili na kufanya mawasiliano nami.
Hata hivyo, kabla ya kuanza mada yangu ya leo, niwaombe miongoni mwenu nyote mlioguswa na makala zote mbili zile, na lakini pia mkaguswa na ujumbe mfupi wa Dk. Slaa kwangu, niteue ujumbe mfupi (sms) wa msomaji mmoja, ambaye kwa kumfahamu kwangu naamini ni bado mtu mwenye fikra na maoni huru ambayo hayajaathiriwa na itikadi za siasa za vyama vyetu.
Msomaji wangu huyo, Absalom Kibanda, ambaye ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Freemedia, baada ya kupitia makala zangu zote mbili na pia kusoma mrejesho wa Dk. Slaa kwangu kwa makala ya wiki ile ya nyuma, alinitumia ujumbe huu: "Kaka umefanya kazi kubwa. Katika hili, nadhani Dk. Slaa alihamaki bila sababu kwa kuwa hata kama ulichokiandika kilimkera kwa sababu zozote zile, iwe ni kwa upotoshaji au kupingana na mwenendo wa CHADEMA, bado alipaswa kuonyesha ustahimilivu na ukomavu wa kisiasa (0754 001010).
Baada ya utangulizi huo, niwaombe wasomaji wangu tuendelee na mada ya leo. Makala hii ya leo nimeiandika nikisukumwa na msomaji wangu mmoja katika makala ya wiki iliyopita. Msomaji huyo, baada ya kuyapitia maandishi yangu, alinitumia ujumbe ufuatao:- "Habari ndugu mayage! Naitwa Deo Makilika, nipo safarini kuelekea IR (Iringa). Katika makala yako ndani ya Raia Mwema ya Nov 30-Dec 6, pg 22, inaonyesha umeanza ku-lose mwelekeo, hivi inawezekanaje kukosa chama mbadala cha kusimamia uzalendo katika nchi yenye wazalendo wengi?
Huu ni upotoshaji mkubwa, nashauri uwe unafanya utafiti wa kina kuliko kuandika kwa hisia au jumla jumla, utakuwa mwandishi mzuri sana. Kila la kheri! (0719 935250).
Katika makala yangu ya wiki iliyopita, iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho: Sababu tunayo, tuwang'oe 2015, niliandika kwa kutoa ushauri kwa Watanzania wenzangu kuungana kwa pamoja ili kuuondoa na kuutupa baharini mfumo mzima wa utawala uliopo kwa sasa, kwa kuwa taasisi zake zote, katika matukio mawili tu ya sakata la Richmond na lile la aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, zimeonyesha zinausimamia na kuulinda kwa ustadi mkubwa mfumo wa rushwa na ufisadi uliotamalaki nchini.
Katika hilo, nilitoa ushauri kwa wazalendo wenye uchungu wa kweli wa namna utajiri na rasilimali za nchi hii zinavyotafunwa kifisadi, kuanzisha chama cha siasa makini sasa, si kusubiri kesho na Watanzania wakiunge mkono kwa nguvu zote, ili mwaka 2015 tuondokane na mfumo huu wa kulindana baada ya kamati teule mbili za Bunge letu, zilizochunguza suala la Richmond na Jairo kutufumbua macho juu ya hali halisi inayofanywa na watendaji wetu serikalini.
Hilo la kuwataka wazalendo wa kweli kuanzisha chama cha siasa makini cha kutuongoza Watanzania kuung'oa mfumo wa sasa, ndilo lililomuudhi msomaji wangu Deo Makilika, anayeamini nimeanza ku-lose (kupoteza) mwelekeo na nimefanya upotoshaji mkubwa kwa ushauri wangu wa kuanzishwa chama mbadala cha kusimamia uzalendo na hivyo kuhoji; "hivi inawezekanaje kukosa chama mbadala cha kusimamia uzalendo katika nchi yenye wazalendo wengi?"
Naomba nimhakikishie ndugu yangu Deo na wasomaji wangu kwa ujumla wao kwamba sijaanza kupoteza mwelekeo. Kama Deo anaujua vizuri mwelekeo wangu, basi naomba aamini kwamba uko pale pale, haujatikiswa. Hata hivyo, napenda kumhakikishia kwa uwazi kabisa na bila shaka yoyote ndugu Deo kwamba kwa Mtanzania yeyote anayefuatilia siasa za nchi hii, hahitaji kufanya utafiti wowote ili kujua kuwa hadi sasa ninapoandika makala hii na inaposomwa na wasomaji wangu, ndani ya nchi hii, hatuna chama chochote mbadala cha kusimamia uzalendo huo tunaouhitaji Watanzania baada ya miaka mingi ya kunyonywa, kudhulumiwa na kuteswa na baadhi ya Watanzania wenzetu wachache waliokosa uzalendo kwa nchi yao kupitia mikataba mibovu ya umeme, madini na mingine mingi.
Najua wasomaji wangu watanishangaa kwa tamko langu hili la kusema hadi sasa hatuna chama cha siasa chochote ambacho ni mbadala wa CCM 2015 ili kituongoze katika kutupeleka kule ndoto yetu sote inakotuelekeza twende. Hadi sasa, tunavyo vyama 17 vya upinzani vyenye usajili wa kudumu. Baadhi ya vyama hivyo hata wanaoviongoza hawajulikani. Vyama hivyo ni pamoja na CHADEMA, CUF, TLP, NCCR-Mageuzi, UDP, NLD, NRA, TADEA, UPDP, MAKINI, FORD, CHAUSTA, DP, Jahazi Asilia, PPT-Maendeleo, SAU na UMD.
Nawaomba Watanzania tutoke nje ya ofisi au nyumba zetu kwenda kwa wananchi wenzetu tuwaulize vyama hivyo vinasimamia itikadi na sera gain? Tuwaulize ni chama gani kimeisimamia kwa ustadi hoja yake ya kuwakomboa Watanzania kutoka mikononi mwa madhila ya CCM kwa maendeleo ya nchi na watu wake kwa kauli na vitendo vinavyofanana na jinsi viongozi wao walivyo na wanavyoishi.
Najua wasomaji wangu hao watakaonishangaa, katika orodha hiyo ya vyama 17 vya upinzani watanishangaa kwa sababu imani yao iko katika CHADEMA na wanajua na kuamini kuwa ndicho chama mbadala kitakachokomesha ufisadi na mafisadi katika nchi hii na hivyo, kutufikisha kwenye Tanzania tunayoitaka.
Binafsi bado sijashawishika na chama hicho, na hasa baada ya kushindwa kusimamia hoja moja tu ya posho ya vikao kwa wabunge na watendaji serikalini, hoja ambayo kinasema imo ndani ya sera zake.
Ndugu zangu, katika mwelekeo na upepo unaoikumba dunia ya sasa, mabadiliko ya uongozi wa chama cha siasa ndani ya nchi yetu ni lazima. Tena basi, mabadiliko hayo yamerahisishwa na watawala wetu wa sasa pamoja na makada wa chama chao tawala kwa sasa. Ndiyo maana mara zote napoteza nguvu zangu kukishauri CHADEMA ambacho Watanzania wanaelekea kukiamini kuwa ni mbadala wa CCM, kitoke kwenye uanaharakati na kuingia kwenye siasa zinazotia matumaini na zenye lengo la kukamata dola na usimamizi thabiti wa vyombo vya dola kwa misingi ya kidola, na hivyo kuwaongoza wananchi kwa kuonyesha njia.
Ndani ya CHADEMA wapo wanasiasa wazuri tu, wanaofanya siasa kweli, lakini hao hawana sauti wala nafasi ya kukielekeza chama hicho ni ipi njia sahihi ya kufanya siasa. Wenye sauti na ushawishi (influence) ndani ya chama hicho ni wanaharakati hali inayokifanya chama hicho kuendeshwa kiharakati kwa asilimia 80 na asilimia 20 inayobaki ndiyo inayofanya shughuli za kisiasa.
Narudia tena kusema, fursa hii iliyopo kwa sasa ni tunu ya pekee kwa CHADEMA. Kimeingia Jimbo la Igunga kwa mara ya kwanza na ndani ya siku 28 tu, kimekubalika kwa zaidi ya asilimia 40. Hiyo tu ya Igunga, ilitosha kuwaelekeza viongozi wa CHADEMA ni dira gani ya kufuata ili mwelekeo huo wa wananchi wa Igunga uwe mwelekeo wa nchi nzima kuelekea 2015.
Badala yake, wanapoteza muda kulumbana kuhusu umeya wa Manispaa ya Arusha, kana kwamba bila umeya huo hakitakuwa na hadhi ya kisiasa. Wanapoteza muda wao kuzungumzia muswada na sheria mpya ya mabadiliko ya Katiba Mpya kana kwamba muswada na sheria hiyo ikiandikwa kwa utashi wao ndiyo itakayopiga kura mwaka 2015 na kukipeleka Ikulu.
Serikali na Rais wake, Jakaya Kikwete pamoja na chama chake, wamekubali kilio cha muda mrefu cha Watanzania kuwa na Katiba Mpya ya nchi. Binafsi, nilitaraji baadhi ya watu wetu weledi wa masuala ya Katiba, baadhi ya wanasiasa na hasa wa CHADEMA, wangekitumia kipindi hiki cha kuelekea uandishi wa Katiba Mpya, katika kufanya utafiti na udadisi wa ni Katiba ipi bora katika nchi za dunia hii, ili iwe mfano wa Katiba mpya tunayoitaka katika mazingira ya kijiogorafia, kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa Taifa letu.
Ndugu zangu, katika mazingira haya ya sasa ambayo Watanzania wamekata tamaa na kuishiwa kabisa matumaini ya kuendelea kutawaliwa na CCM, CHADEMA kinaonekana kuwa mbadala kwa kuwa katika udhaifu wa vyama vyote vya siasa vilivyopo, kinaonekana kuwa na unafuu wa udhaifu kuliko vingine. Lakini hiyo haitufanyi tusahau msemo wa kwamba hata katika msafara wa ndege aina ya bundi, lazima apatikane bundi wa kuwaongoza wenzao waliomo katika msafara huo.
Kwa upepo wa mabadiliko unaovuma duniani kwa sasa, na ambao Watanzania hatuna njia yoyote ile ya kuukwepa tukiwa chini ya utawala huu wa CCM ya aina ya sasa, inayoshindwa kuchukua hatua stahiki kwa mafisadi wanaoifisadi nchi yetu na kuendekeza urafiki na uswahiba katika masuala ya msingi ya uongozi wa nchi na yanayogusa uhai na uchumi wa Taifa letu, upepo huo unaweza kabisa kutusukumia mikononi mwa hata shetani au chama cha ovyo ili mradi tu kutimiza dhamira na nia yetu ya mabadiliko hayo.
Vyama vya siasa vya kambi ya upinzani tulivyonavyo, vipo na vilianzishwa kwa sababu ya fursa ya kikatiba. Vingi ya hivyo, vinafanya siasa za kubabaisha ili vionekane vipo kwa sababu vilisajiliwa kama vyama vya siasa. Hata viongozi wao wengi ni watu ambao huko nyuma walishindwa kuishi katika masharti na misingi ya uzalendo na utaifa enzi za chama kimoja na kujikuta wakitupwa nje ya mfumo, na hivyo walianzisha vyama vya siasa watakavyotumia kama jukwaa la kuwasema mahasimu wao hao wa zamani.
Nihitimishe makala yangu hii kwa kusema tunahitaji kuwa na chama cha siasa kitakachoanzishwa na kundi la watu linalochukizwa na mwenendo wa utawala wa chama kilichoko madarakani leo, ambao hautoi matumaini ya kuwaondolea Watanzania maadui wakuu watatu waliotangazwa miaka 50 iliyopita; ujinga, maradhi na umasikini.
Tunahitaji kuwa na chama cha siasa, kitakachoanzishwa na kundi la watu wenye uzalendo wa kweli kwa taifa lao, wanaoamini kwamba ardhi ya kutosha tunayo, siasa safi ambayo imeendelea kusimamia misingi ya amani na utulivu iliyowekwa na waasisi wa taifa letu tunayo, isipokuwa tumeshindwa kufika katika safari yetu kwa sababu tu tumekosa uongozi bora. Kwa hiyo, kuanzia sasa, tunahitaji kuwa na uongozi bora wa nchi, unaotokana na chama kipya bora cha siasa, kitakachoanzishwa na watu wenye dhamira hiyo katika nafsi zao.
Tulivyonavyo sasa, havina tufauti na NGO's tunazozijua. Ni vyama vya kutafuta fedha za ruzuku ndani na nje ya nchi, ili walau familia za wanaoviongoza ziishi maisha yanayofanana na familia za watawala wetu.
Ndiyo maana waliomo ndani ya vyama hivyo, wakikosa tu fursa ya ulaji, hukimbilia kuisaka fursa hiyo ndani ya vyama vingine ili tu wafanikishe ulaji. Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa wanasiasa aina ya Magale John Shibuda wanaweza kukubali kukifia chama chao cha sasa pindi ubunge utakapowaponyoka. Naomba kuwasilisha!
Ujinga wa Mayage
- Mayage anakiri kuwa CHADEMA ni kipenzi cha watanzania halafu anasema binafsi yeye hakijamshawishi kuwa mbadala wa CCM. Kama kimeweza kuwa kipenzi cha watanzania waliowengi inawezekana hakijamshawishi yeye kutokana na upeo wake ndio maana mnaweza kuwa darasa moja mmoja anapata zero na mwingine division one uwezo wake wakuelewa mambo hawezi kutushawishi watanzania wengi waliowapenzi wa CHADEMA kama alivyokiri mwenyewe.
- Mayage anasema CHADEMA hakijamshawishi na wala si mbadala halafu bado anapoteza muda kukishauri huu si ujinga mwingine. Halafu anasema tena hii ni fursa pekee kwa CHADEMA kwa vipi wakati ameshauri kianzishwe chama kingine.
- Aliponiacho hoi zaidi ni hapo ni kuhusu Katiba, kwa maneno yake anasema, Binafsi, nilitaraji baadhi ya watu wetu weledi wa masuala ya Katiba, baadhi ya wanasiasa na hasa wa CHADEMA, wangekitumia kipindi hiki cha kuelekea uandishi wa Katiba Mpya, katika kufanya utafiti na udadisi wa ni Katiba ipi bora katika nchi za dunia hii, ili iwe mfano wa Katiba mpya tunayoitaka katika mazingira ya kijiogorafia, kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa Taifa letu.Unafanya utafiti wa nini halafu uupelekewapi wakati hakuna mfumo mzuri wa kupokea tafiti zako.
Anayebisha abishe lakini huyu bwana anamtumikia
Nawasilisha hoja
Hili Gazeti la Raia Mwema hata Nimeshahau linatoka lini! Hili limekuwa kama Gazeti la Membe
Hili ndilo tatizo kubwa! Kila anayekuja na hoja ya udhaifu uliopo CDM anadhaniwa kuwa ni CCM!!!WAPENDWA haya ni katika kujenga chama!!!
Mguu tulionza nao sio sahihi!!wananchi wamechoka,nasi twatumia nafasi hiyo kuona kila jambo tulifanyalo ni sahihi!!!ok wengine tuna mawazo ya kipumbavu!!ila mkumbuke kisemwecho sahihi ata tufanyeje,tupinge kitajidhirisha tu! Ni suala la muda!!na ngoja tuone! 2015 si mbali!