Mwandishi APIGWA risasi na Polisi

Mwandishi APIGWA risasi na Polisi

Tumaini Makene,

Post yako mbona haieleweki? Shaban ndiye nani? Aliyepigwa risasi?

Kama ndiye aliyepigwa risasi, una maana kuwa Mama Jay ndiye mkewe?

Kama Mama Jay ni mke wa Shaban (aliyepigwa risasi), polisi walikuwa wanamtafuta mke wa Shaban?

Kama walikuwa wanamtafuta mke wa Shaban, ina maana wanaishi vyumba tofauti?

Kama wanaishi vyumba tofauti, ilikuwaje Mama Jay aliwafungulia polisi mlango wa chumba alimokuwepo Shaban?

Kama aliwafungulia mlango polisi, ilikuwaje tena polisi wakapishana na Mama Jay akitokea kwenye kibanda?

Au kuna Mama Jay wawili waliopanga kwenye hiyo nyumba?

Kama kuna Mama Jay wawili waliopanga kwenye hiyo nyuma, can you put this clear in your post please?
 
Tunamtakia heri mhanga, polisi hawawezi kutoa tamko bado hawajapewa na aliyewatuma. Na hata hilo tamko litakapokuja kutoka linakua jepesiiii wakati tukio limehatarisha maisha ya binadamu.Huenda kweli ikawa ni bahati mbaya you never know ila kwa trend ya hawa polisi wetu na rekodi ya mauaji ya raia ya hivi karibuni inakua vigumu sana kukubali kwamba ni bahati mbaya.

Hata kama angekua ni mhalifu waliyemkusudia, kitu ambacho sio sahihi bado hapakua na mazingira ya kumpiga risasi.

Sometimes namkumbuka mzee ruksa kwa kufanya kitendo cha kiungwana alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani 1976 kuwajibika kwa kesi ya shinyanga ingawa hakuhusika moja kwa moja[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]. I non't know who, but some one must go, at least this time.[/FONT]
 
...Usishangae kesho ukisikia walikuwa wanapambana naye kwa masaa mawili kwa kuwa alikuwa na silaha hatari etc etc. Yote kwa yote no excuses charminglady.
Nchi wanaipeleka kubaya! askali polisi anaruhusiwa kushambulia kwa risasi? tena mtu hajaweke resistance yoyote wana mshambulia? Hao wametumwa na Pinda, au Mkuu wa usalama taifa
 
Polisi, Kombe walimfananisha na jambazi.... Kweli tutakwisha.....
 
Jeshi la polis, linafanya kazi kwa matakwa ya watu wachache tena ni kwa maslahi ya chama
 
Nchi imewashindwa, wanaanza kutaka kutoa roho za watu, dhambi inazidi kuwatafuna hao
 
Baadhi yetu tumefika hospitali. Tulikuwa na mmoja wa wana JF senior. Alinikuta pale. Alikuwepo mwandishi mwenzake na Shaban na mfanyakazi mwenzake mwingine. Kisha akaja mwandishi mwenzake mwingine na pia akafika Absalom Kibanda, Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima na Mwenyekiti wa TEF.

It is just another sad story kwa kweli kama wengine walivyokwisha kusema hapa. Waandishi tumeweza kuzungumza na mke wa Shaban, Mama Jay. Kitu ambacho hakiingii akilini eti polisi wa anti crime hawawezi hata ku spot exactly chumba cha mhalifu wanayemtafuta kwa mabunduki na mabastola, wanaanza kupita wanauliza uliza kwa wapangaji wenzake.

Wanaelekezwa mlango au chumba cha mtuhumiwa wanayemtafuta, Mama Jay. Bado wanakosea mlango, wanaenda kugonga kwa Mama Jay mwingine, bila tahadhari wala kujitambulisha wanaingia ndani wote kishari, kisha wanafyatua risasi kumuelekea Mama Jay (mke wa Shaban), ambaye ananusuriwa na kitendo kile cha wao kuingia kwa kasi kwa kupamia mlango kama wahalifu, anadondoka, risasi zinapigwa zinampata mwandishi wa habari, kama unavyoona kwenye picha, almanusura impate kwenye moyo. Fikiria nini yangekuwa matokeo yake. Risasi kupiga moyoni.

Kisha askari hao ambao tulitarajia wawe weledi hasa linapokuja suala la uhai wa mtu, wanaambiwa hapo si kwa Mama Jay mnayemtafuta, mbona tuliwaelekeza mlango ule pale. Kama hiyo haitoshi, askari mmoja akataka kuitoa ile risasi kwa Shaban kwa mikono. Kufuta ushahidi? Bahati nzuri Shaban aligoma, muda huu wangesharuka. Yangekuwa mambo ya kupigwa na vitu vizito. Imeshindikana.

Nane, maana hatujui filamu hii itageuzwa namna gani baadae hata kufikia tisa na kumi, wakati wanaondoka pale nyumbani kwa Shaban, akipelekwa hospitali, wakapishana na Mama Jay mtuhumiwa aliyekuwa anawindwa na hao anti crime police. Maana inasemekana wakati zogo likiendelea alikimbilia kibanda fulani mtaani hapo hapo. Wameoneshwa Mama Jay mliyekuwa mnamtafuta si huyo hapo, wala...hawakuwa na habari naye tena.

No body is safe. This is not an issue of somebody. Nchi inageuzwa pole pole, police state.

Kwa hiyo katika nyumba hiyo kuna Mama J mhalifu na Mama J ambaye si mhalifu (Mke wa Shaban)! Wakaonyeshwa Chumba cha Mama J mhalifu wao wakaenda kwa Mama J ambaye si mhalifu! Wakaingia na kuanza kupiga risasi hovyo? Wakamkosa Mama J badala yake risasi ikampiga Baba J kisha wakakimbia bila kumkamata Mama J mhalifu ambaye walipishana naye?

Duh hapa kuna maswali meeeeengi kuliko majibu! Huyo Mama J ni mhalifu wa aina gani hadi hao polisi wafike na kuanza kumwaga risasi? Ina maana basi atakuwa ni mhalifu sugu na walikuwa na habari kwamba she is armed to the teeth! Sitaki kuumiza kichwa changu
 
Post yako mbona haieleweki? Shaban ndiye nani? Aliyepigwa risasi?

Kama ndiye aliyepigwa risasi, una maana kuwa Mama Jay ndiye mkewe?

Kama Mama Jay ni mke wa Shaban (aliyepigwa risasi), polisi walikuwa wanamtafuta mke wa Shaban?

Kama walikuwa wanamtafuta mke wa Shaban, ina maana wanaishi vyumba tofauti?

Kama wanaishi vyumba tofauti, ilikuwaje Mama Jay aliwafungulia polisi mlango wa chumba alimokuwepo Shaban?

Kama aliwafungulia mlango polisi, ilikuwaje tena polisi wakapishana na Mama Jay akitokea kwenye kibanda?

Au kuna Mama Jay wawili waliopanga kwenye hiyo nyumba?

Kama kuna Mama Jay wawili waliopanga kwenye hiyo nyuma, can you put this clear in your post please?
Hakuna kisichoeleweka hapo, unless wewe ndo huelewi..... In short, nyumba ile ina mama J wawili, mmoja mke wa mwandishi (Mwandishi ni shaban na ndo aliyepigwa risasi) na wa pili ndo mtuhumiwa. Polisi waliingia chumba cha mwandishi badala ya mtuhumiwa ambaye hakuwepo home kwake. Wakati wanaondoka kwenda hospitali wakakutana na mtuhumiwa njiani lakini hawakuwa na time naye...
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Madhara ya kunywa viroba wakiwa kazini, nadhani hawa polisi wanyang'anywe bunduki wabaki na virungu tu otherwise watatuua sana, polisi ni adui mkubwa kabisa wa raia, nilishasema NIKIMKUTA POLISI ANAPAMBANA NA NYOKA WALLAH NAMSAIDIA NYOKA
 
Hapo tusubiri kuambiwa ni tukio la kawaida kikosi cha intelejinsia
 
Jamani Ritz wewe ni binadamu wa kawaida kweli? Kwani kuna msemaji wa polisi hapo? Nilitegemea wewe kama mchangiaji wa kwanza umtakie huyo mwandishi Get Well Soon. Ah Ritz!

Wewe vipi mie nimefanyaje? Mijitu mingine bana...hii habari aijaeleza vizuri kisa hicho.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo kali! anayefungua mlango ndiye anayepigwa risasi?........... Kama walimhisi kwa nini wasimkamate alipofungua mlango?........... Kama hili tukio ni la kweli basi nchi haiko salama!.........ukombozi unahitajika haraka sana....
 
Tz hakuna jeshi la polisi kabisa. Kila wakati wanataka kufanya mazoezi ya kutumia silaha. Haya hayatofautiani na mauaji ya mwangosi. Tegemea hoja nyepesiiii kama ni upepo tu huu utapita.
 
Huku mbele ni kubaya zaidi kama tusipoamua leo kuwa basi hatutaki tena hizi defender kunyima watu Amani usiku.

Ni wachache sana humu ndani ambao wakikutana na gari ya patrol usiku hawataogopa au kukimbia, ilitakiwa iwe the inverse(ukiwaona ufurahi ujue ulinzi na msaada umefika).


Nijuavyo mimi hata kama kweli wangefanikiwa kupata chumba sahihi cha mtuhumiwa, ingefaa wafanye yafuatayo
1. Wabishe hodi
2. Wakifunguliwa Wajitambulishe
3. Wahakikishe mtuhumiwa wao ndio huyo
4. Wamuambie Kosa lake Wamuaresti
5.Wamsomee Haki zake
6. Wampeleke kizuizini.

In the process kama angeleta ubishi au ukorofi ndio wawe a little cohesive. Akiendeleza ubishi akiwa na silaha fatal ndio wamtandike gun (sio kuua) ya kumpoza tu.


Lakini hapa nchi ya maziwa na asali ni tofauti.
 
EMT Angalia vizuri mkuu!Mbona alichokiandika kinaeleweka kabisa!Au ndio kazi zakiwakilishi?Tuache kutumika ovyo kama makarai yazege jamani!Gorofa likiisha hatuna thamani!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom