KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,960
- 40,301
Furaha katika maisha yetu hazitokani na wingi wa mali tunazojilimbikizia bali inatokana na kuridhika na kile ambacho muumba amekujaalia na ufurahie kuwa nacho...wanadamu wengi wa nyakati hizi wamekuwa wakihangaishwa na mali kwa kudhani kuwa mali ndio kila kitu maishani mwao...hata wakajikuta tayari wameshakuwa watumwa wa mali....kiasi kwamba wapo tayari kufanya lolote ili wapate mali.
...muda wao mwingi wanautumia kutafuta mali hata wakashindwa kukifurahia kile kidogo ambacho muumba amewajaalia....watu hawa hawana Baraka mbele za MUNGU kwani wamekosa shukrani kutoka ndani ya nyoyo zao...ingawaje kwa nje wanaonekana ni matajiri lakini ni mafukara wa kutupwa mioyoni mwao....muda mwingi hawana raha maishani mwao kwani wanaangaishwa na mali kuliko afya zao....na kipindi chao cha kuishi hapa duniani ni kifupi sana....