Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,356
Wasichana wengi hupata bahati ya kugundua madhaifu ya wachumba wao mapema sana.
Madhaifu mengine huwa ni makubwa kiasi cha kuhatarisha furaha, amani, umuhimu katika jamii, afya na hata maisha ya msichana husika hasa pale watakapoingia katika ndoa.
Wapo wasichana wengi tu ambao pamoja na kugundua madhaifu hayo huwa "wanakomaa" na wanaume wao na mara nyingi kwenda kuishi kwa mateso. Unajua ni kwa nini?
Zipo sababu nyingi lakini nataka leo tujadili hii moja: Wanawake wengi wanawafanya wanaume wao kuwa wa maonyesho.
Wanawake wana wivu wao kwa wao!
Mwenzao akiwa na mchumba mwenye mafanikio, huanza maneno ya pembeni kuwa "hana lolote, ataachwa tu".
Hupigwa umbea na fitina na hata baadhi ya marafiki hudiriki kwenda kujitongozesha kwa shemeji, au kumlengeshea shemeji demu mwingine, ili mradi tu hujuma za kumharibia rafiki yao
Sasa msichana anapopata habari kuwa kuna marafiki-maadui wanaotamani na hata kufanya juhudi za kumkosanisha na mtu wake, huamua "kuwakomoa" kwa kuhakikisha mahusiano hayavunjiki.
Sasa balaa huwa pengine mwanaume alishagundulika "hafai", lakini kwa vile msichana hataki kuonekana ameshindwa au kusemwa kuwa "ameachika", hujikuta akiendelea kuvumilia tu na hata kukubaki au kulazimisha kuingia kwenye ndoa,
anakufa na tai shingoni dadeki...