Wana JF naombeni ushauri. kuna mwanaume nilikuwa nawasilana nae kwa simu baadae tukaonana siku ya kwanza akaanza kunipa sera zake nikamwambia nipe muda wa kufahamiana. lakini nilipokutana nae mara ya pili amekuwa akitaka tufanye ngono nikamkatalia na kila tukiendelea kukutana suala la kufanya ngono ndo msisitizo wake hadi ananiboa hata sina tena hamu ya kuendelea kukutana nae. Nikamjibu kuwa kuhusu ngono kwa sasa asahau sasa kila akinipigia simu anasema ajafurahishwa na msimamo wangu. misimamo yangu mingine ya maisha haijamgusa ila suala la kukataa kufanya ngono ndo limemgusa. pia katika kukutana nae tumekuwaq tukipata tu soda na chakula cha gharama ya kawaida ana sijawahi hata kupokea fedha yake ila amekuwa akiniambia yaani wewe ndo mwanamke wa kwanza kula fedha yake, pia nikimwambia anionyeshe anapokaa anasema eti anaishi na mdogo wake hivyo hawezi kunipeleka kwa sababu hajawahi kumpeleka mwanamke nyumbani kwake pia mama mwenye nyumba yake anamfikiriaje kwani hana tabia hiyo. kwa hayo wana JF nataka kumtema kama naona anifai vile Naombeni ushauri.