Mwanaume shoga aamua kukiri redioni kufanya biashara hiyo

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Shoga-moro-3.jpg

Morogoro: Katika hali isiyo ya kawaida, kijana Karimu Said (25) almaarufu Anti Karimu aliyekiri kufanya biashara haramu ya kuuza mwili (ushoga), ameangua kilio redioni wakati akiutangazia umma wa Watanzania kuachana na dhambi hiyo aliyodumu nayo kwa miaka saba.

Ilikuwa Alhamisi iliyopita, Karimu alifika katika ofisi ndogo za gazeti hili za mkoani hapa na baadaye alitinga kwenye Kipindi cha Mcharuko wa Pwani cha Radio Planet FM kinachoendeshwa na mtangazaji mahiri, Warda Makongwa akishirikiana na Farham Abraham.

Lengo la Karimu lilikuwa ni kutubu dhambi yake hiyo sambamba na kumuomba msamaha Mwenyezi Mungu na Watanzania kwa jumla.

Akiwa hewani laivu kwenye kipindi hicho na watangazaji hao na mwandishi wetu, Karimu alisimulia kilichomwingiza kwenye ushoga kuwa ni umaskini uliotokana na vifo vya wazazi wake.

“Baada ya wazazi wangu kufariki dunia na mimi kumaliza darasa la saba hapa Morogoro, nilikwenda Dar kutafuta kazi. Nilipofika nilipata kazi ya ndani (house boy) kwa bosi mmoja.

“Nikiwa hapo, bosi wangu wa kike na wanaye walikwenda likizo kijijini, mimi nilibaki na bosi wa kiume.

“Siku moja huyo mwanaume alinirubuni akanipeleka beach (ufukweni) na baadaye Mlimani City ambako alinilazimisha kunywa pombe.

“Tuliporudi nyumbani aliniingilia, tangu hapo kila siku akawa akinifanyia hivyo. Mkewe aliporudi alinikanya nisimwambie, nikajikuta namuonea wivu huyo mwanaume hata akiwa na mkewe.

“Hali hiyo ilisababisha mkewe kujua na kunitimua,” alisema Karimu.
Alisema kuwa baada ya kutimuliwa alirejea kwao Morogoro na kuendelea na ushoga akijiuza kwenye madanguro yaliyopo ltingi na Kahumba mjini hapa.

Alipoulizwa wateja wake wakubwa ni watu gani, Karimu alifunguka kuwa ni waume za watu wakiwemo baadhi ya vigogo wa serikali.

Mwandishi wetu alipomtaka kuelezea changamoto alizokumbana nazo, alifunguka huku akiangua kilio studio: “Changamoto ni nyingi zikiwemo za kupigwa, kupata bwana akakulipa elfu arobaini lakini ukifika geto kwake, ukishamhudumia, anakugeuka na kukunyang’anya fedha.

“Nimeyatafakari matukio yote hayo, ndipo nikaungana na rafiki yangu aliyenipeleka kanisani ambako niliombewa hadi nikaanguka, nikapoteza fahamu, nilipozinduka nikajiona niko kwenye ulimwengu mwingine na kujutia dhambi hiyo ya ushoga, hivyo naomba Mungu na Watanzania wanisamehe,” alisema Karimu huku akilia.

Chanzo: globalpublishers
 
Mungu amuongoze katika njia safi daima. Hili nalo ni janga la Taifa
 
Dar ukija uwe na akili zako timamu... Ndo wakome kuvamia jiji letu. Na tena waendelee kunyooshwa tu wakija na ushamba na ushog wao humu. Yaani ajabu kabisa toto la kiume linabanduliwa af linabembelezwa lisiseme na linakaa kimya na kuendelea tu kuliwa. Tina bil aibu eti na lenyewe "linamwonea wivu mke wa baksha wake" si ufala huu..
 
wanaume wanaotia mashoga nao wa ajabu sana ...wanatudhalilisha wanaume wengine tunaonekana kamambwa,,,,katubu na kugundua njia iliyo njema ndiokitu chema kwa sasa....wapo wngi na vijana wanapendahata mashoga tena usiotarajia....ni shetani kazini kamwaga spirit chafu kwa jamiii na haya mambo ya haki haki sijui nini upuuzi...
 
aise so sad
Angetaja na majina la huyo firahuni aliyemfundisha mchezo mbaya
Sijui ni mdudu gani huyu anayeshambulia kizazi hiki
 
Katika hali isiyo ya kawaida, kijana Karimu Said (25) almaarufu Anti Karimu aliyekiri kufanya biashara haramu ya kuuza mwili (ushoga), ameangua kilio redioni wakati akiutangazia umma wa Watanzania kuachana na dhambi hiyo aliyodumu nayo kwa miaka saba.
“Nimeyatafakari matukio yote hayo, ndipo nikaungana na rafiki yangu aliyenipeleka kanisani ambako niliombewa hadi nikaanguka, nikapoteza fahamu, nilipozinduka nikajiona niko kwenye ulimwengu mwingine na kujutia dhambi hiyo ya ushoga, hivyo naomba Mungu na Watanzania wanisamehe,” alisema Karimu huku akilia.
cc: THE BIG SHOW, kahtaan, Ritz,
https://www.jamiiforums.com/members/ritz.34266/
 
aise so sad
Angetaja na majina la huyo firahuni aliyemfundisha mchezo mbaya
Sijui ni mdudu gani huyu anayeshambulia kizazi hiki
Kwani alibakwa? Yy anasema alirubuniwa akaona ni tamu akaendelea mwenyewe hadi kumuonea wivu mke
 
Huyo aache kudanganya watu ndo kwanza anainadi biashara yake huwezi kupona kwa kuombew tu labda angesema alienda hospitali kutibiwa sawa sijawahi sikia shoga anapona kwa maombi tu bila kwenda hospitali na zile sehemu maalumu ambao husaidia wao kupona
 
Humu ndani wapo wa kutosha naona inabidi waache mana hawawezi kupata mimba na kuzaa kma dada zetu......kila cku machoko wanaongezeka hko mbeleni kiama watakiona
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom