Mimi kwenye swali la mapenzi na ndoa ninabakia na kauli hizi ambazo zimejenga mizizi katika jamii:
1. Mapenzi kipofu/Anayependa haoni/Kipendacho moyo.
Mtu akipenda kweli anaziba macho na kutia pamba masikio. Anakuwa hasikii, haoni. Anakosa muda wa kuijadili nafsi yake. Kilicho na nguvu hapa ni mapenzi na wala sio sababu nyengine kama jamii au familia. Hili la mwisho linauma (kutengana na familia yako) lakini ndivyo ilivyo.
2. Ndoa hufungwa mbinguni.
Si mara zote na si wote wameoa/wameolewa na wale hasa waliowataka. Popote utakapoangukia, ikiwa hakuna sababu za msingi kugeuka nyuma, inakubidi udumu katika ndoa.
Kwa kujibu swali lako Boss, kwa kuunganisha na hizo points mbili za juu, nitaoa yule ninayempenda.