Mwanaume mtaalamu jikoni

Mwanaume mtaalamu jikoni

angalau mwanamme mmoja amethubutu sema hali halisi

Tafsiri nzuri ya mke ni msaidizi,huwezi kutoka kwenye pilika umechoka halafu uje upike,na usiniambie na yeye alikua kwenye pilika kwani hilo sio jukumu la msaidizi,akishakuwa na pilika anakua sio msaidizi,ninapooa ninaoa coz nahitaji msaidizi na kupika ni moja ya majukumu yake!
 
Kwa nini asiwe na hobby za kiume?
Huoni tatizo hapo?
Kesho akija kasuka tatu kichwa akwambia ni hobby utashangaa?(kwa mnaosuka ipotezeeni nimetoa tu mfano hapa)

A man is a man
a woman is a woman
japo tunajitahidi kuweka politics kulingana na tunayoyataka
lakini kila gender ina nafasi yake

Sasa wale ambao upishi ni kazi unawaweka kundi lipi? Je Ali mapilau ana mapungufu kama akipika pilau la christmas kwa familia.........
 
Hahahahahaah naona ilikuwa varangati la kukata na shoka....kupika kwa Mwanaume hata siku moja hakuwezi kupunguza status yako kama Mwanaume mahali popote pale duniani, lakini ukiwa na mtu ambaye bado ameganda katika mawazo ya mwaka 47 basi inaweza kuwa kasheshe ya hali ya juu hata kusababisha mahusiano yafikie tamati. Hakuna mahali popote pale ilipoandikwa kwamba kupika ni majukumu ya mwanamke. Tamaduni hubadilika pia kutokana na wakati. Katika nchi nyingi za Afrika miaka kama 30 au hata zaidi iliyopita ilikuwa ni nadra sana kumkuta mwanamke engineer, pilot au doctor au anayeendesha gari leo wamejaa tele baada ya kuelewa kwamba hata mwanamama anaweza kabisa kuwa engineer, doctor au hata kuendesha gari au kuwa rubani wa ndege.

Haya mawazo ya ajabu sana!!
 
I got a question for you guys,

Katika mazingira yetu ya kibongo bongo bado hakikubaliki sana kwa mwanaume kuingia jikoni na kupika, haswa na wanaume wengine. Akifanya hivyo basi ataitwa majina kibao na yatasemwa mengi juu yake mf.mume bwége,kakaliwa, kalishwa limbwata, sio mwanaume kamili n.k.
Sasa swali langu ni kama hayo hapo juu yanamhusu mwanaume ambae anaishi na mwanamke , vipi yule asieishi na mwanamke(mpenzi/mke)?Pengine anaweza akawa anaishi na ndugu, dada wa kazi au hata mwenyewe.Huyu tumwite nani? Maana kama kukaliwa kakaliwa na nani?Limbwata kapewa na nani?Ubwége kavishwa na nani?Uanaume kavuliwa na nani?

Nadhani ni muda sasa tuanze kukubali wanayofanya wengine na kuwaacha wajihukumu wenyewe.Kama wewe hutaki/huwezi hamna haja ya kumwita anaefanya majina ya ajabu.Baki tu ukishangaa!!

Na hawa wanaopika maotelini wanaitwa je? Au kwavile ni ajira haina noma
 
angalau mwanamme mmoja amethubutu sema hali halisi

Yes,ukweli lazima usemwe kama kuna mtu anaogopa kusemwa ili kamwanamke anakokavizia kasimkatae eti ni ka independeti womani kapotelee huko huko!
 
angalau mwanamme mmoja amethubutu sema hali halisi
Jamani mbona mfumo wa maisha umebadilika ndio maana sasa hata mke kupika inakuwa ngumu,nyumba nyingi sasa kuna wasaidizi wa kazi kwa wale ambao wazazi wote ni wafanyakazi .

Hatukatai kwamba mwanamke anajukumu la kusimamia nyumba kuanzia mapishi, usafi na mengineyo ila kama mwanaume akiamua kupika kwa mapenzi yake yeye sio mbaya ila sio kuwa jukumu lake.

Je wale wanaume ambao wanakipato kidogo je sio wanaume kutokana tu pato la familia linatoka kwa mama.......ukiangalia kwa hivyo mambo mengi sivyo kama inavyoonekana katika jamii.
 
Yes,ukweli lazima usemwe kama kuna mtu anaogopa kusemwa ili kamwanamke anakokavizia kasimkatae eti ni ka independeti womani kapotelee huko huko!

Hamna haja ya kuleta dharau kwenye hii thread.Huyo "ka" au "anaekavizia" wafikishie ujumbe kupitia PM, au waanzishie thread.
 
Watu wanadai eti siku hizi mambo yamebadilika,yamebadilikaje?Majukumu ni yale yale,mwanamke ni mwanamke na mwanaume ni mwanaume!Majukumu ya mwanaume hayaweziw ya mwanamke na ya mwanamke hayawezi kuwa ya mwanaume!
 
Ilikuwaje akajikuta huko
alianzaje
sio baada ya kushindwa kufit kwenye kazi za kiume???
Akakimbilia huko?
Ukisoma post za nyuma nimesema angalau wao unaweza waelewa

Sasa wale ambao upishi ni kazi unawaweka kundi lipi? Je Ali mapilau ana mapungufu kama akipika pilau la christmas kwa familia.........
 
Hamna haja ya kuleta dharau kwenye hii thread.Huyo "ka" au "anaekavizia" wafikishie ujumbe kupitia PM, au waanzishie thread.

Kabla sijasema mengi hebu nipe tafsiri ya neno DHARAU,ili nipate uhakika kama unajua unachokizungumza!
 
Nauliza swali:

Kazi za nyumbani kama vile, kupika, kufua, kufagia na kupiga deki, kuosha vyombo, kwenda kisimani/bombani kuchota maji n.k. Tunapata wapi kuwa ni kazi za kike?

Wakati huo huo hizo kazi zikiwa ni za kuajiriwa na kuna kipato ghafla bin vuu, zinageuka kuwa za kiume... Ajabu!

Labda niulize tena hii kusema kuwa hizo ni kazi za kike ni kwa mujibu wa Imani za Dini, Mila na desturi au ni kwa mujibu wa jamii zinazo tuzunguka?

Naomba wale wenye kutaka kujibu watoe reference aidha kwa mujibu wa imani zao au kwa mujibu wa mila na desturi zao, ili tuone kukataa au kukubali kwao kunatokana na sababu fulani.

Karibuni.
 
utakuwa hujaona jibu langu?
Walianzaje?
Sio kwa kushindwa kufit kwenye kazi za kiume?
Na kutafuta refuge kwenye upishi?
Nawaheshimu kwa kuovercome fear zao na kujitokeza katika jamii kama wapishi
kile kitendo cha kujikuta huko tayari ni tatizo
ilianzaje????

Mwenyewe nimeuliza mpaka muda huu sijapata jibu.
 
naona umeanza nielewa sasa
iko kikekike sana
hata kama anapata hela
sababu cha kujiuliza
ni ilikuwaje akajiingiza kwenye upishi
kama sio kwa kushindwa kufit kwa wanamme?

inawezekana ni ajira haina noma lkn imekaa kikikekike vile (ina matiti nadhani)
 
Gender roles zipo tu
tunakataa just to feed our ego
au kuficha misfit zetu kwenye gender tulizopo
au umagharibi zaidi

Watu wanadai eti siku hizi mambo yamebadilika,yamebadilikaje?Majukumu ni yale yale,mwanamke ni mwanamke na mwanaume ni mwanaume!Majukumu ya mwanaume hayaweziw ya mwanamke na ya mwanamke hayawezi kuwa ya mwanaume!
 
Ilikuwaje akajikuta huko
alianzaje
sio baada ya kushindwa kufit kwenye kazi za kiume???
Akakimbilia huko?
Ukisoma post za nyuma nimesema angalau wao unaweza waelewa

Chukua tano!Halafu waendelee kulalama eti majibu hawajayaona!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom