Mwanaume Miaka 30 bado unakaa kwenu!

Mwanaume Miaka 30 bado unakaa kwenu!

thebogo055

Member
Joined
Jun 22, 2020
Posts
19
Reaction score
176
Katika vitu ambavyo sikubaliani navyo ni huu msemo!! Jamani maisha yanapiga nyiee! Maisha yanachapa kama fimbo.

Ukiona by that age uko kwako unajimudu mambo ya maana mshukuru Mungu.

Kuna watu wame hustle sana lakini wapiii, wamepambana sana lakini wapi.. washasalitiwa na marafiki, wapenzi, mitaa so the only option ni kukaa home kuchora ramani za kutoboa kimaisha.

Siamini wamekaa home bila mipango kwa miaka 30.

Na wengi wanaopenda kuwa bully watu wa hivyo ujue hawajawahi kuwa katika hali hiyo.. ndugu yangu usiombe yakukute.. maisha sio fair kabisa..

Shukuru Mungu, shukuru kwa kila jambo acha kukebehi wenye maisha mabovu.

By the way nyumbani is the only safe place ya kutulia kama mambo yatakuendea kombo.

Maana marafiki watakuchoka ukiishi kwao na huna msaada, mwanamke atakukimbia au kukufukuza kama mambo sio mambo.

Lakini ukiwa home ndugu zako wa nyumbani hawatakuchoka na watakuvumilia wakiona focus yako.

Tupambane sana mpaka wale ma age mate zako wakuite MKUU, KIONGOZII, na majina mengine.
 
Nakupata mkuu.

Kiafrika kupanga nyumba au kujenga nyumba na uhame kwenu inaonekana kama jambo la maendeleo, lakini kimsingi si kweli.

Kuwa na msimamo wa kifedha uweze kufanya jambo lolote linalowezekana kufanywa ndio jambo la msingi. Ukipenda kuhama kwenu na kuanzisha kwako ni sawa maana utakuwa na uwezo huo, ukipenda kubaki kwenu na kama nafasi (space) ipo, kaa tu.

Usihame kwenu sababu tu ya umri au sababu watu wa umri wako wengi hawakai kwao. Tafuta pesa kwa ajili ya kuwa na msimamo ama miguu (base) ya kukuwezesha kufanya chochote upendacho. Mtu kumuacha baba na mamaye maana ya moja kwa moja sio kuhama nyumbani kwenu.
 
off course, kama kuna hiyo opportunity kwa nini asiitumie?

Sio lazima kila mwanaume apange au kujenga nyumba.

Vipi umechoka na visababu vya niko busy bimkubwa this mshua that etc?
 
Mwaka huu umekuwa mgumu sana kwangu mambo karibia yote hayajakaa vzr. Uzuri nilikuwa nimeandaa shamba langu la miti la kutosha Lina miaka nane kwahyo bado miaka miwili nivune na nikivuna sikosi ata milioni 15 Ila nawaza mpaka miaka miwili ije kuisha nitakuwa nafanya nini? nimejenga nyumba thamani Kama milioni 50 sijaoa nawaza sibora niuze hii nyumba nifanye michakato ya maisha kuliko kukaa kusubiri miaka miwili ya kuvuna miti wakati umri wangu ndo Kwanza miaka 30?
 
Mwaka huu umekuwa mgumu sana kwangu mambo karibia yote hayajakaa vzr. Uzuri nilikuwa nimeandaa shamba langu la miti la kutosha Lina miaka nane kwahyo bado miaka miwili nivune na nikivuna sikosi ata milioni 15 Ila nawaza mpaka miaka miwili ije kuisha nitakuwa nafanya nini? nimejenga nyumba thamani Kama milioni 50 sijaoa nawaza sibora niuze hii nyumba nifanye michakato ya maisha kuliko kukaa kusubiri miaka miwili ya kuvuna miti wakati umri wangu ndo Kwanza miaka 30?
Uza fasta.
 
Hahaha nawashangaa mtu unazaliwa duniani unafia duniani someone hata hapo mwezini tu kama kufika hapa Mars mmeshindwa.

Nyumbani ndio wapi?!
 
KIla mtu na maisha yake. Mtu kukaa kwao kinapunguzia nini? Ukiona mtu anakaa kwao na ana miaka 30, mpe michongo ya kazi ili aondoke hapo. Kumsema mtu anakaa kwao wakati humsaidii kwa lolote ni mambo ya kiswahili.
Katika maisha yangu huwa nawaogopa sana watu wenye mambo ya kiswahili kiswahili. Unakutana na mtu anakuuliza unafanya kazi gani? kazi yangu inakuhusu nini? Vijana peaneni michongo ya kupiga pesa. Mambo ya kusema semana ovyo yashapitwa na wakati. Ndiyo maana nyumba za kishua wamezungushia ukuta mrefu wenye kozi 8 na juu wameweka waya wa shoti na geti kali.
Duuu , kukaa kwenu at the age of 30 isn't Fair
 
Hili swala linategema na familia yenu ikoje especially katika swala zima la kiuchumi, mimi nisingepata mchongo mbali na nyumbani mpaka leo ningekuwa naishi home mpaka nioe, sababu sehemu ipo ya kutosha na home kwa sasa kuna upweke mkubwa sana coz yupo bimkubwa na mjuu wake tu. Sioni dhambi ya mtu kuishi kwao mpaka huo umri.
 
Back
Top Bottom