Mtoto wa kiume miaka 30 bado unaishi kwenu, huna hata godoro. Jiandae kufa masikini

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,626
Kijana wa kiume una miaka 30 bado unaishi kwenu sikatai lakini huna mbele wa nyuma umekaa tu huna hata godoro na kitanda jua unaenda kufa masikini tu hii ni aibu

Kuna vijana wanakaa tu nyumbani wanakula bure na kulala bure hadi vocha anapewa na bi mkubwa wake acheni hiyo mnatia aibu jitegemeeni sana au hata kama upo kwenu ni sawa tu lakini jitume uwe unachangia income nyumbani sio unakaa tu unakula na kulala ni aibu

Mtu ana miaka 30 kajiridhikia tu kwao hana hili wala lile wala hana mpango wa kuwaza atatoka je kimaisha huko ndo kufa masikini sasa

Na hizi tabia zipo sana hapa dar sana wanaume wa dar ndo zao hizi sijui kawaloga nani

Una miaka kuanzia 22 upo kwenu jitafakari sana aisee jitafakari sana unamiliki simu ya iphone na nyingine za zaidi ya laki 8 hadi milioni 2 wakati hata kitanda huna my dear wewe ni mzigo wa taifa jitafakari sana unaelekea pabaya

Unakuta kijana wa miaka 30 hapa dar anakaa kwao anakula bure na kulala bure tu anamiliki iphone au samsung ya milioni moja hadi milioni 2 lakini hana hata godoro la kununuwa kwa jasho lake hivi hamuwazagi maisha nyie watu?yaani simu ya milioni 2 hata kitanda chako mwenyewe huna?,duuh

Wengine ni vijana wakubwa wao kazi ni kukesha tu gym kutengeneza six pack na kula protein powder wanapiga machuma gym tu hakuna shughuli yoyote ya kipato wanayo kazi kutesa wazazi wao tu wagharamikie na kuilishia mibaba mizima ya gym mario wa dar wazazi wengine mna kazi kweli kweli, hawa wa gym ndo wale kutwa kucha kupost masix pack mtandaoni kudangia majimama na kuzunguka na vibegi vyao vya Gucci's sijui unajikuta kama nani wewe wao kazi yao ni kuwaomba wanawake pesa mtandaoni tu hivi hujiulizi kwamba utatoboa lini?hayo maisha ya umario na kula kwenu bure huchangii hata kitunguu ni hadi lini yaani umejiridhikia tu.

Yaani nyie brothers ambapo tayari mna 30 na zaidi bado mmekomaa na kwenu na hakuna kitu mmewahi fanya maishani andika umeumia na nikwambie ukweli mimi huwa sio mnafiki, hautotoboa kamwe maana kwa age hiyo ya 30 na zaidi upo tu kwenu mtoto wa kiume huna hata godoro au chochote ulonunua kwa hela yako ya jasho jiandae tu kufa masikini na kuishia pabaya.


Acheni kutesa na kuwabebesha wazazi mizigo ya kuwalea ilhali mshakua wakubwa
Acheni kutesa na kuwabebesha wazazi mizigo ya kuwalea ilhali mshakua wakubwa
Acheni kutesa na kuwabebesha wazazi mizigo ya kuwalea ilhali mshakua wakubwa
Acheni kutesa na kuwabebesha wazazi mizigo ya kuwalea ilhali mshakua wakubwa*


MTANISAMEHE LAZIMA TUAMBIANE UKWELI
 
Kweli aisee, wengine tukiwa na miaka 14 tushaanza kujitegemea ilaa ni vile hali kwetu zilikuwa ngumu mpaka Leo tungekuwa kama hao

Mleta mada naona ni type ya sisi kwetu pakavu... ila kwa wenzetu mboga saba mbona kawaida sana kuwa uko home unalalia kitanda alichonunua babako
 
Sio wote wanapenda kukaa majumbani kwao, unakuta wanakosea PIN CODE za maisha kidogo tu. Maisha hayana formular. Kuna siku mambo yatajipa na watatoka kimaisha, mpaka kufikia ma group yote ya whatsapp ya familia watawaweka sura zao profile pic.

Na wengine wanakaa majumbani kwasababu wamefelishwa kimaisha na familia zao hizo hizo.

Maisha ni kama gololi za mbuzi, mara zinakwenda mbele na mara zinarudi nyuma.
 
Kijana wa kiume una miaka 30 bado unaishi kwenu sikatai lakini huna mbele wa nyuma umekaa tu huna hata godoro na kitanda jua unaenda kufa masikini tu hii ni aibu...
Hii kitu ipo sana kwa vijana wa mjini. Tofauti na wale wa vijijini hata kulala na wazazi wao jengo moja ni haramu. Hasa akishafikisha miaka 13 au 14 huwezi kuta bado analala kwa wazazi. Lakini hawa wa mjini ni kwa kiasi ni walemavu, mtu miaka 30 bado unalala nyumba moja na Baba na Mama!!
 
Hakuna ABCD za maisha, kila mtu anaishi vile alivyochagua, angalia wapenda au wenye asili ya Asia, wanakaa wanao na kuzeekea wao na wa toto wao nyumbani kwao,acha wivu na chuki za ajabu, wakikaa kwa wazazi wao wewe inakuuma nn mkuukwanza wanaokufa masikini na wanaokufa matajiri wote watakufa tu
 
Back
Top Bottom