Mwanaume bahili wa kazi gani?

Mwanaume bahili wa kazi gani?

We mbona ukienda kuhonjombora hauombi risiti ya vitu ulivyovitoa? Mbona hautozwi ushuru wa uchakavu unaomfanyia mwanamke? Let's play fair games men
Hapo kumbuka natumia nguvu zangu na hisia zangu swala la kumchafua sio kweli maana nae anapata utamu
 
Wanawake wabovu kwa kupenda pesa! Kama wao ndio wanatengeneza...
 
Mapenzi Hapo,pesa inaongeza upendo jamani. Tusiwe waongo tukubaliane na hili tu. Pesa sabuni ya roho
Uko sawa kabisa mama... Lkn naww uwe unatoa za kwako tutumie!!!
Sio unashadadia mapenz pesa huku za kwako umeficha kibindon
 
Uko sawa kabisa mama... Lkn naww uwe unatoa za kwako tutumie!!!
Sio unashadadia mapenz pesa huku za kwako umeficha kibindon
If you know my may he will tell,akikwama Nina msaidia effectively...
 
View attachment 502106

View attachment 502107

Upendo ni muhimu katika mahusiano, lakini mwanaume kuwa na fedha hufanya mapenzi kuwa na mvuto zaidi. Mwanaume ni lazima awe na fedha kwa ajili ya kumnunulia mpenzi wake zawadi mara kwa mara siyo leo amemnunulia mpenzi wake kijizawadi ndiyo asubiri mwakani, lakini pia kumtoa mpenzi wake out au kuwa na mitoko ya mara kwa mara ni muhimu achilia mbali kuwa na kawaida ya kumtumia mpenzi wake fedha za matumizi mbalimbali na pia muda wa maongezi kwenye simu yake yote haya ni muhimu kwa mwanaume kumhudumia mpenzi wake.

Mambo haya yanatakiwa kufanywa na mwanaume bila kusubiri kuombwa na mwanamke maana si kila mwanamke anajua kuomba omba lazima mwanaume ajue wajibu wake wa kumhudumia mpenzi wake badala ya kusubiri mpaka aombwe. Kila mwanamke anapenda kuwa na mwanaume atakayemudu kumhudumia kwa kila kitu hapo ndipo mapenzi yanapokolea na mwanamke kujitoa kwa mwenzi wake na kuhakikisha anampa raha wakati wote.

Huu ujumbe hauna maana ya kuwananga na kuwatweza wanaume wasio na fedha, la hasha, najua kutokuwa na fedha ni suala la muda tu lakini pale utakapojaaliwa hata kidogo jitoe kwa kumpa mwenzi wako fedha na kumnunulia vijizawadi vidogo vidogo na yeye anaiona hali yako atakuheshimu.

Kuna ile mijanadume ambayo ina fedha lakini mibahili ka nini, hiyo ndiyo uzi huu unawahusu sana. Jamanieeee Wanaume msiwe wabahili kuwahudumia wapenzi wenu kwani ubahili utawafanya kila mwanamke awakimbie na mwisho wa siku utaishia kuitwa shemeji

Kwa wanawake wenzangu. Kamwe tena naomba kusisitiza, Kamwe usijitie kiherehere kumhudumia mwanaume, kumbuka fedha zako zikiisha atakutosa na kutafuta mwanamke mwingine.

Ni ushauri wangu wa bure

CC: charminglady, Nifah, Miss Natafuta, snowhite, BADILI TABIA, gfsonwin, King'asti, Super women 2,
Mbona mnajijengea utamaduni usio na kichwa wala miguu? Yaani tena unatoa hadi ushauri!
Ndo nyie tunaotaka waume zenu waishiwe alafu tujue Tania zenu halisi.

Kununua zawadi au kumtoa mpenzi wako out hakuna jinsia.
Pili inakupasa ujue kuwa mti wa mapenzi haupaliliwi na mwanaume peke yake. Ni jitihada za wapendanao kuhakikisha penzi linazaa matunda yaliyotarajiwa.

Hii tabia ya wanawake kusema mwananume ndo anajukumu la kumtunza mwanamke, ndiyo inayofanya wengi wenu mnakimbiwa na mnajikuta mnajiuza indirect.

Nakushauri tafuta pesa zako za kununua vicha na kujihudumia ndipo utafute mwanaume anayekufaa. Nje ya hapo utaishia kuzijua size za wanaume kila uchwao
 
Hivi formula ya kusolve shida na lawama za mwanamke itapatikana lini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom