Mwanaume bahili wa kazi gani?

Mwanaume bahili wa kazi gani?

Kwa usawa huu hizi thread tuzitarajie nyingi tuu. Madada zetu skuizi wanachanganyikiwa wanakosa kwa kupumulia. Skuizi hata zile vocha za buku buku nazo wanazipata kwa shda kweli.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
#nimwanzotuugetstrong_realshit abouttostart
 
Mapenzi Hapo,pesa inaongeza upendo jamani. Tusiwe waongo tukubaliane na hili tu. Pesa sabuni ya roho
 
halafu baadae atakuja mwanamke mwingine hapa anasema wanaume hatuthamini utu wa wanawake

SWALI:
kama uko kifedha zaidi mwanaume ataheshimu utu wako kweli?

Badala ya kuwaza kufanya mambo ya kukuza uchumi wenu kwa pamoja mtu anawaza kununuliwa zawadi na kuhudumiwa. You're a grown up woman, Deal with your own problems

ni mtazamo tu
 
Yaani ukisha sema eti nikuhudumie ndo unaharibu kabisa bora hata usingesema ningekufikiria sipangiwi cha kukufanyia!
 
Mbinu ya utajiri ni UBAHILI

Sijazaliwa BANK nikuhonge hela kila saa

Hela haziokotwi, kwa hiyo nikikupa hela yangu iheshimu sana, hujui nimefanya mangapi..nimekwepa mangapi hadi nakupa Pesa...Ifike mahala Pesa iheshimiwe..

Ukipenda kupokea na upende kutoa pia!
 
Hapo inabidi mtangaze kuwa mnauza ili nikija na nunua na kuondoka kuliko kunichuna
We mbona ukienda kuhonjombora hauombi risiti ya vitu ulivyovitoa? Mbona hautozwi ushuru wa uchakavu unaomfanyia mwanamke? Let's play fair games men
 
View attachment 502106

View attachment 502107

Upendo ni muhimu katika mahusiano, lakini mwanaume kuwa na fedha hufanya mapenzi kuwa na mvuto zaidi. Mwanaume ni lazima awe na fedha kwa ajili ya kumnunulia mpenzi wake zawadi mara kwa mara siyo leo amemnunulia mpenzi wake kijizawadi ndiyo asubiri mwakani, lakini pia kumtoa mpenzi wake out au kuwa na mitoko ya mara kwa mara ni muhimu achilia mbali kuwa na kawaida ya kumtumia mpenzi wake fedha za matumizi mbalimbali na pia muda wa maongezi kwenye simu yake yote haya ni muhimu kwa mwanaume kumhudumia mpenzi wake.

Mambo haya yanatakiwa kufanywa na mwanaume bila kusubiri kuombwa na mwanamke maana si kila mwanamke anajua kuomba omba lazima mwanaume ajue wajibu wake wa kumhudumia mpenzi wake badala ya kusubiri mpaka aombwe. Kila mwanamke anapenda kuwa na mwanaume atakayemudu kumhudumia kwa kila kitu hapo ndipo mapenzi yanapokolea na mwanamke kujitoa kwa mwenzi wake na kuhakikisha anampa raha wakati wote.

Huu ujumbe hauna maana ya kuwananga na kuwatweza wanaume wasio na fedha, la hasha, najua kutokuwa na fedha ni suala la muda tu lakini pale utakapojaaliwa hata kidogo jitoe kwa kumpa mwenzi wako fedha na kumnunulia vijizawadi vidogo vidogo na yeye anaiona hali yako atakuheshimu.

Kuna ile mijanadume ambayo ina fedha lakini mibahili ka nini, hiyo ndiyo uzi huu unawahusu sana. Jamanieeee Wanaume msiwe wabahili kuwahudumia wapenzi wenu kwani ubahili utawafanya kila mwanamke awakimbie na mwisho wa siku utaishia kuitwa shemeji

Kwa wanawake wenzangu. Kamwe tena naomba kusisitiza, Kamwe usijitie kiherehere kumhudumia mwanaume, kumbuka fedha zako zikiisha atakutosa na kutafuta mwanamke mwingine.

Ni ushauri wangu wa bure

CC: charminglady, Nifah, Miss Natafuta, snowhite, BADILI TABIA, gfsonwin, King'asti, Super women 2,


Vipi kama sina fedha lkn nina Dushe la ukweli, na nakupa sex ya kutosha?
 
Back
Top Bottom