Mwanaume anapotongozwa na mwanamke

Ha ha ha wanaume kutongozwa siku hizi kawaida sana. Tunatofautiana wanaume wanasema (nakutaka, nakupenda, nakuthitaji nk) lakini wanawake wanatenda kuonyesha kuwa (nakupenda, nakutaka, nimekuzimia, nakuhitaji nk)

Tatizo kubwa kwa wanaume walio wengi ni kutokuelewa wakati wanatongozwa na wanawake, kwani wanawake wengi wanapomtaka mwanaume fulani kimapenzi huwa hawasemi direct, bali vitendo/matendo yao. Sasa kutafsiri vitendo hivyo ndo ngoma.
 
Kwa kweli kipindi chetu ilikuwa taabu kidogo m'mke kumtongoza m'me. Yaani walikuwa kwa mateeeeeendo matendo utawatambua tu! Kizazi hiki cha dot com bana anakwambia live bana nakutaka. Ukibishabisha anaanza I will do everything to get you mazee! Ombea asiwe anakacheo hapo kazini utamtambua mpaka akupate ndo mambo yatakwenda msuano!
Kwa kweli sio vibaya mtu kutumia uhuru wake! Kwa sisi wengine hali hii inatustua kidogo na ni nadra sana!
 
Watu tunatofautiana,wapo wengine ambao humuona msichana kama vile ni kiruka njia na hajiheshimu,wapo wengine ambao watatangaza kila kona na mengineyo mengi.Lakini kwangu mimi binafsi huwa ninamuheshimu sana msichana aliyeweza kunikabili na kunieleza ukweli wake hata kama sitakubaliana na ujumbe wake,na huwa ninamchukulia kama mtu anayejiamini na ambaye atakuwa mke bora kwa mumewe kwa kuwa ana uwezo wa kueleza hisia zake na hata kama mambo hayaendi vizuri katika familia basi atazungumza bila kuficha hisia zake.

Kwa upande mwingine kuna wale ambao hawawezi kumkabili mwanaume na kumueleza ukweli ila wanaonesha kwa vitendo,hao mimi ndio wala huwa sina muda nao hata aje kwangu hajavaa nitamuangalia tu kwakuwa ilinitokea kuiwa karibu na mkurugenzi wangu ambaye alipenda muda mwingi kuwa na mimi hasa wakati wa kunywa kahawa na mida ya lunch,tatizo alikuwa anapenda sana kuvaa vimini ambavyo viko juu yua magoti basi muda wote tunaokuwa pamoja mimi nakuwa na kazi ya kuchungulia nguo zake za ndani na alikuwa hajui hasa kukaa,na nikimtazama tukikutanisha macho basi napewa tabasamu na kurembuliwa juumambo yalikuwa mengi tu ya mitego basi mtoto wa kisukuma nikajua amenipenda nikazungumza.Alivyokuwa mstaarabu wala hakunijibu vibaya aliniambia tu nitakujibu jumatatu ofisini.Jumatatu nafika ofisini nakutana na barua ya kufukuzwa kazi kwa sababu ya utovu wa nidhamu.toka siku hiyo nikakoma kumtongoza msichana kutokana na ishara anazonionesha mpaka anitamkie wazi.
 
Mimi nshazoea kutongozwa na wasichana huwa mda mwingine hata walionizidi umri ila mimi huwa sikubali kwani huwa hata akisemaje naona moyon kwang hayupo hata kidogo
 
Demu akinitongoza clembi coz ataniona nyoka wa kibisa,nafanya mambo yangu af uyo najikataa kmya kmya kwa kuwa km aliweza kuntongoza mm ashindwi kumtongoza mwingine,nshafagia mademu 15 wenye style izo.
 
Watu tunatofautiana,wapo wengine ambao humuona msichana kama vile ni kiruka njia na hajiheshimu,wapo wengine ambao watatangaza kila kona na mengineyo mengi.Lakini kwangu mimi binafsi huwa ninamuheshimu sana msichana aliyeweza kunikabili na kunieleza ukweli wake hata kama sitakubaliana na ujumbe wake,na huwa ninamchukulia kama mtu anayejiamini na ambaye atakuwa mke bora kwa mumewe kwa kuwa ana uwezo wa kueleza hisia zake na hata kama mambo hayaendi vizuri katika familia basi atazungumza bila kuficha hisia zake.

Kwa upande mwingine kuna wale ambao hawawezi kumkabili mwanaume na kumueleza ukweli ila wanaonesha kwa vitendo,hao mimi ndio wala huwa sina muda nao hata aje kwangu hajavaa nitamuangalia tu kwakuwa ilinitokea kuiwa karibu na mkurugenzi wangu ambaye alipenda muda mwingi kuwa na mimi hasa wakati wa kunywa kahawa na mida ya lunch,tatizo alikuwa anapenda sana kuvaa vimini ambavyo viko juu yua magoti basi muda wote tunaokuwa pamoja mimi nakuwa na kazi ya kuchungulia nguo zake za ndani na alikuwa hajui hasa kukaa,na nikimtazama tukikutanisha macho basi napewa tabasamu na kurembuliwa juumambo yalikuwa mengi tu ya mitego basi mtoto wa kisukuma nikajua amenipenda nikazungumza.Alivyokuwa mstaarabu wala hakunijibu vibaya aliniambia tu nitakujibu jumatatu ofisini.Jumatatu nafika ofisini nakutana na barua ya kufukuzwa kazi kwa sababu ya utovu wa nidhamu.toka siku hiyo nikakoma kumtongoza msichana kutokana na ishara anazonionesha mpaka anitamkie wazi.

Pole kwa kufukuzwa kazi jamaangu.
Vipi yule anayejua kuwa wewe ni mume wa mtu na anakujia kuwa anakutaka! naye tumwite jasiri ama ni nini mkuu?
 
Majuzi hapa nimetongozwa na kibinti na ninaomba nikili hapa kwamba hakuna kipindi kigumu kama hicho katika maisha
 
Hii kitu imenikumbusha mbali yaani... Msichana wa kwanza kunitongoza nilitolea nje tena kwa kujitetea kweli! Tena yeye hakutumia hizo ishara mnazosema, alinikabili live! Ila baada ya huyo nimewahi kutoka na ambao ni wao walinitongoza! Kuhusu ninawachukuliaje, kwa kweli ninawaheshimu sana... Hata yule wa kwanza nilimchukulia poa kbs na nilihudhuria harusi yake, sikuwahi kumdharau hata kidogo. Kwa kawaida naheshimu sana msichana anayeweza kuweka wazi hisia zake.
 
Hii habari ni nongwa, usisikie. Shida ya wanawake akikutongoza ina maana anakupenda kweli tofauti na wanaume amabo wengi ni waongo and all they need ni sex.

Sasa shida ni pale unapokuwa wewe humpendi, na unamweleza hivyo lakini haelewi. Weeee, mbona utaona dunia chungu. Na akishidwa kabisa, umemwaga ugali na yeye anamwaga mboga. Anakuharibia kama una mtu. Ni noma aisee.
 
Hii kitu huwa siifagilii kweli aisee, huwa inanipotezea kujiamini mbele ya huyo binti, matokeo yake naanza kumkwepa. Tena wanaonikera zaidi ni wale wanaoshirikisha rafiki zangu, manake huwa wananiandama sana.. Kati ya mabinti wote wanaonitongoza hakuna aliyebahatika kunipata, manake huwa wananifanya niwe na aibu na kuwakwepa kuepuka ku-blush mbele yao... Napendelea kutongoza kuliko kutongozwa.

whuhhwhuuu!
 
Hakuna tatizo kwa mwanamke kumtongoza mwanamke ni tamaduni tu.
Kinamchanya mtu kutongoza ni kwa sababu hisia zinamtuma hivo. hata mwanamke ana hisia pia za kimapenzi tena kuliko hata sisi wanaume ila tamaduni zetu ndo zinatuathiri
Kwa hiyo kama mwanamke akikutongoza wewe una wajibu wa kumkubalia au kumkatalia, hata mie nilishawahi kutongoza na mwanamke japo sikukubaliana nae lakini sikujisikia vibaya kwani alinieleza hisia zake nami nilimjibu kwa upole to the extent that hakuumia sana japo ilikuwa vigumu kwake kunielewa na ilichukua muda zaidi ya miezi miwili kumkatalia.
Ndugu yangu badilika katika hilo.
Thanks
 
Mbona kila siku tunatongozwa na wanawake, imeisha kuwa fashion hakuna cha ajabu hapo.
 
Back
Top Bottom