Mwanaume anapotongozwa na mwanamke

tatiana.

Member
Mar 20, 2011
41
15
nisaidieni jamani...napata majibu yanayonichanganya... kina kaka na hata kina dada hebu niambieni..mwanaume anapotongozwa na mwanamke anajisikiaje??? ni nini mawazo yake??? Je, unamchukuliaje mwanamke liyekutongoza
 
Ingawa haikuzoeleka, hakuna cha ajabu. Mara nyingi ikiwa mwanamke kakutongoza ni kuwa mnafahamiana kabla, ingawaje zipo kesi za "love at first sight". Mwanamke anapokutongoza atakuwa amejiamini hata kukukabili, na zaidi kwa kukuhisi kuwa unaona haya kiasi huwezi kuanza wewe. Na ikiwa huna majukumu (unaye wako tayari), kubali bila ya kusita, sio kwa sababu ya kumhurumia au kwa sababu umejiona umepata cha bure na ukaanza kujipandisha chati. Ikiwa humtaki kwa dhati bora urudishe majeshi nyuma. Dhambi itakuwa kumkubalia kutaka kutumia fursa baadaye ukamwacha. Hili sikushauri.
 
Hebu jiangalie kuna kitu chochote ambacho kinaweza kumfanya m'ke akavutika nacho kwako, na upendo ukawa ni sababu ya tu kutaka kuingia kwako. Katika hali hiyo unaweza kumsoma taritibu kutokana na alivyo kupitia vipengele tofauti na lazima utamgundua tu. Hivyo usifanye haraka ktk kuaccept offer hiyo kwa kuona umepata mteremko. Wala usitie shaka sana juu ya m'ke kumtongoza m'ume kwani kwa sasa hiyo ni hali ya kawaida. Na hadi mwanamke kufikia kukutongoza, mara nyingi huwa ameshatanguliza ishara ila hukumuelewa au hukutaka kumuelewa tu. Be care usiogope
 
nisaidieni jamani...napata majibu yanayonichanganya... kina kaka na hata kina dada hebu niambieni..mwanaume anapotongozwa na mwanamke anajisikiaje??? ni nini mawazo yake??? Je, unamchukuliaje mwanamke liyekutongoza

Ni hatua ya mapenzi tuu, hakuna jipya
 
Ha ha ha wanaume kutongozwa siku hizi kawaida sana. Tunatofautiana wanaume wanasema (nakutaka, nakupenda, nakuthitaji nk) lakini wanawake wanatenda kuonyesha kuwa (nakupenda, nakutaka, nimekuzimia, nakuhitaji nk)
 
Hilo mbona jambo la kawaida!lilianza toka enzi za ADAM na HAWA/EVA,Hawa alimtongoza Adam
 
Jeff Hawa alimtongozaje Adamu, ebu nisomee kifungu kinachosema? Ongea kitu ambacho ni real. Kumtongoza mwanaume ni kitu cha kawaida. Unajua kwa wanawake haitsumbui nigeuza macho na kujishebedua siyo lazima nikwambie nakupenda. matendo yanaonyesha tu. Hata kwa mwanaume siyo lazima uniambie the way unavyobehave ndiyo nitakapojua kwamba huyu ananihitaji na automatic inatiki. wewe unayesubiri etu uwambiew nakupenda wakati unadanganywa Pole zako.
 
Inategemea anauzikaje bana kama vp nampotezea tu polepole i mean kistaarabu ,lakini vivyo hivyo wenge la kutongozwa inategemea ushakutana mara ngapi na hali hii na ujasiri ulio nao wa kukisimamia unacho kiamini bila kujali kua umeomba au umeombwa mahusiano binafsi mi mara kibao tu huwa wananizingua na mbaya zaidi huwa ving'ang'anizi mbaya na ukimtosaaaa!!!atakuletea hata mkono wa Albino getho.
 
nisaidieni jamani...napata majibu yanayonichanganya... kina kaka na hata kina dada hebu niambieni..mwanaume anapotongozwa na mwanamke anajisikiaje??? ni nini mawazo yake??? Je, unamchukuliaje mwanamke liyekutongoza

Mpendwa mbona siku hizi mambo ya kawaida na mdada akishapita akaona una nini haogopi kukutokea :lol:
 
Hakuna ubaya na wanaume wengi wanaweza kukubali hali hi ila baadhi wanaweza kuuliza maswali kama yafuatayo. Umeshawatongoza wangapi? Je ni kitu gani kinachokuvutia kwa mwanaume mpaka ufikie uamuzi wa kumtongoza? Je kesho kesho kutwa wakati uko na huyo uliyemtongoza na ukamuona mwingine aliyekuvutia utakuwa tayari kumtongoza pia? na kumpiga chini huyo uliyekuwa naye?

YouTube - Justin Bieber - Never Say Never ft. Jaden Smith
 
Mh hii ni ya kisasa zaidi siye wa zamani ngoja tukae pembeni
 
nisaidieni jamani...napata majibu yanayonichanganya... kina kaka na hata kina dada hebu niambieni..mwanaume anapotongozwa na mwanamke anajisikiaje??? ni nini mawazo yake??? Je, unamchukuliaje mwanamke liyekutongoza

Mh, umegusa pabaya, mimi inanisumbua sana hii... :focus:
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom