Nafikiri sisi ndiyo tunaharibu utaratibu mzima wa mapenzi. Hivi kweli kisasa unaweza kumbana mwenza wako asifanye anachotaka especially kama hajaoa? Atleast ukishaolewa una say walau mtu akawa na heshima kwako. We mwanaume ambaye hujaoa unataka kuwa na final say kwa GF au BF unapoteza muda wako.
Maisha ya mapenzi ukiyajua wengi wangeolewa na kuoa ila tu tuna kitu kimoja kinaitwa haraka, tena siku hizi hilo pepo ni kote kote. Mtu mmekutana nae mara moja kesho analeta hadithi za kwenda kwa wazazi kujitambulisha kweli inaleta maana? Ki upeo tu hivi unafikiri kwamba waliopita hawakuwa wazuri? Au macho yamepofukia kwako hataona tena? Tuache ushamba siku hizi unaruhusiwa kuuliza kama mapenzi ni ya wiki, siku, miezi au miaka? La sivyo unampotezea tuu achukue time. kuweni wawazi jamani uongo hatusaidii wala kujenga kwenye suala zima la mapenzi.
Na wewe mwanamke unayependa mizoga (wanaume walioowa) kuwa na heshima mwenzio ameomba mapenzi hajasema kwamba mkewe ni mbaya wala hajui kitu, amekutamani tu, una hiari ya kusema ndiyo au hapana, ukisema ndiyo uwe radhi kufata masharti. Usitume message wala kupiga simu at danger time, uwe uwe radhi kuwa mtiifu kwa kila utakachoambiwa la sivyo ukiona mashart huyawezi potezea tafuta wa size yako.
Mwe mwaume kuwa mkweli umeoa na unataka games siyo mapenzi ya ukweli, ili umueweke bibie sawa siyo uanze hadithi za alinacha, ooh mke wangu siyo powa kabisa, hana shape kama yako, piga tu anytime unayotaka mie naongea si ndiyo kidume. Umeula wa chuya!! utaleta maafa.
Gooda day!