Mwanasiasa bora kijana 2012 Tanzania

Vijana wa sasa hawaaminiki,wamejaa tamaa,wanafiki,vigeugeu na waoga sana! Wote uliowataja hawajaonyesha sura zao halisi.Tunawataka watu kama Mandela wa SA,Nyerere,Nkrumah,Steve Biko n.k. Zito Kabwe kapata umaarufu kidogo tu,tamaa imemuanza,anataka ikiwezekana katiba ibadirishwe ili agombee uraisi,"HUYU NI WA KUMUOGOPA KAMA UKOMA".Kwa mtizamo wangu tunahitaji watu majasili kama Dr Ulimboka,Kubenea wa MWANAHALISI au yule mwanamama mtangazaji wa BBC aliyeamua kuhatarisha maisha yake kwenda kwa mganga Mwanza ili kufichua mauaji ya ALBINO.Vijana wengi mashujaa hawajaingia kwenye siasa bado,wanajenga taifa kwa ushujaa mkubwa hukohuko waliko.Uliowataja wote wababaishaji,wakikumbana na dhoruba wataangamia.Ushauri wa bure; Role Model anatakiwa awe yule aliyetangulia mbele ya haki,maana hawezi kugeuka jiwe.Ungeweka watu kama;MWANGOSI,KANUMBA,MTEMA,NA YULE MAREHEMU MBUNGE KIJANA WA KIKE, ALIYEKUWA AKIPAMBANA NA WAUZA MADAWA YA KULEVYA.
 
mimi nampendekeza mnyika,ni kijana anayejituma asiye mroho wa madaraka,ila pia namshauri asije akalewa sifa yakamkuta ya mwenzie....human diginity is everything to me
 
namkubali sana mnyika,ila kwa ufupi namshauri asije akalewa sifa kama wale wengi,afanye kazi ya chama na mungu atampa uongozi kulingana na dhamira yake.
 
Kulingana na michango yake kisiasa na kutuomba radhi kwa aliyoteleze. Kwa moyo wangu, namchagua Mh. Zitto.
 
Zitto hawezi kuwa modal wangu kwa sababu hana mchango wowote katika kukijenga chama chake zaidi ya kukibomoa..Kura yangu nampa MNYIKA na LEMA.
 
WADAU NAWASALIMU SANA, naomba nipate mchango wenu kimtizamo wa chanya zaidi kwa maslahi ya vyama vyetu na Taifa kwa ujumla,katika miaka ya hivi karibu kuanzia 2010 mpaka sasa kuelekea uchaguzi mkuu 2015 pamekuwepo na vijana utitiri kuwa wanasiasa ama kwa ushabiki tu au kuwa na uzalendo,mosi kumekuwepo na vijana wanasiasa wadogo ambao wamekuwa tunu kwa taifa jinsi wanavyojenga hoja nzito nzito kwa mawanda mapana yenye nia ya dhati kuleta maendeleo ya jamii zetu na imefika mahali jamii hizo imewakubali hao vijana na kuona kuwa ndio marais wajao,mawaziri na wabunge wanaokuja baadaye,mathalani kuna vijana wanasiasa NGULI kama ZITO KABWE,JAMES MBATIA,MWIGULU MCHEMBA,JOB LUSINDE wameonekana kuwa wana maono mapana na taifa letu kwa hoja zao nzito. Na kuna wanasiasa NGUMBARU kama JOHN MNYIKA,LEMA,HALIMA MDEE,JAMES KAFULILA,MACHALI,MKOSAMALI,STEVEN MASELE,TUNDU LISU,WENJE,MSIGWA ,JANUARY MAKAMBA n.k ambao wanachipukia kwenye siasa hizi za leo kwa takribani miaka mitano,swali je katika hawa vijana wanasiasa baadhi niliotaja hapa na wengine wanaofahamika ni mwanasiasa yupi anakubalika na kupendwa na jamii na anayefaa kuendelea kuwa kiongozi wao ?. naomba michango yenu kwa maslahi ya taifa letu.nawasilisha
 
John John Mnyika, wengine wanakosa sifa, Ila nae angeoa angekamilisha sifa hata ya kuwa Raisi.
 
Back
Top Bottom