Mwanasiasa bora kijana 2012 Tanzania

Mwanasiasa bora kijana 2012 Tanzania

Mleta mada ungetaka kuutendea haki uzi huu ungepaswa kumuweka Mhe. Zitto Kabwe kwenye orodha yako japo kwa vyovyote vile wachangiaji wa hapa jukwaani najua wasingempa kura kwa sababu za kiushabiki.
Kwangu mimi hakuna anayemkaribia Zitto. Mwenye kupinga hili naomba apinge kwa ushahidi wa vigezo vilivyowekwa hapo juu.
 
jj myika, hana roho ya ufisadi,hana misimamo binafsi linapokuja swala la maslahi ya umma, ni mtu wa hoja, ni mtu anaejitambua vema, ni mtu asiyejali wa kwao tu bali watanzania wote, mcha Mungu, asiyependa makuu, mtu wa utaratibu hakurupukii mambo, anaetafakali kabla ya kunena. Dogo huyu ndiye mfano bora wa vijana wanasiasa.
mnyika hana tamaa ya madaraka kama MZITTO KABWELO!
 
Kwanza mshusha uzi umejaa ukristo, haiwezekani vijana hao wote wakawa wagalatia watupu. Huwezi sema kati ya vijana hao Mh. Zito Zuberi kabwe hawezi kuwa mfano wa kuigwa, huo ni ujinga, udini, na kuji fanfa hujui wakati akili unazo. Binafsi nime udharau uziwako kama nilivyo kidharau CDM.viva Zito,ww ndio kiongozi unae faa kuongoza taifa hili,
nilionya mapema nikasema Udini, Ukanda hauna nafasi katika hoja hii. kama wajumbe wengi wataomba Zitto awepo basi nitamuweka.
 
Mh. John Mnyika.

Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), Mhe. John Mnyika ametolewa nje ya bunge muda huu na
Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kukataa kufuta kauli yake kuwa Rais Kikwete ni dhaifu
wakati alipotakiwa kufanya hivyo. Mnyika ametolewa nje ya bunge wakati wabunge wakichangia
mjadala wa bajeti ya serikali mwaka wa fedha 2012/13 iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni.
Mnyika atarudi bungeni kesho saa tatu asubuhi.

Mnyika: Tumefika hapa tulipo kwa Udhaifu wa Rais Kikwete - YouTube

Mh. Deo Filikunjombe
Hivi punde katika Kongamano ya miaka 51 baada ya uhuru, mwasiasa machachari na mbuge wa
Ludewa Mh. Deo Filikunjombe ametoboa ukweli kuwa kuna kasumba na dhana potofu miongoni mwa
watanzania wakidhani kuwa nchi hii (Tanzania) ni mali ya CCM. Hii nchi si mali ya CCM bali
ya watanzania

Mhe Peter Serukamba

Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia CCM Mhe Peter Serukamba amesema suala la baadhi ya wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupinga posho lilikuwa ni unafiki.

Mh. Godbles Lema
"Vitisho ni vingi hatutaogopa nipo tayari kwa jambo lolote lile sitaacha harakati nipo
tayari kufa hata sasa. Taarifa na ushahidi tunao kwamba kila kinachoendelea sasa kwenye
siasa kinaratibiwa na Idara ya usalama wa taifa. Katika kutafuta ufumbuzi wa nchi kuna watu ambao
watatolewa sadaka na sisi tupo tayari kutolewa sadaka.

Mh. January Makamba

wote waliozaliwa kabla ya 1961 waachane na mawazo ya Urais maana watatupotezea muda ...
tunahitaji rais wa dot.com atakayeendana na changamoto za leo

Mh. Halima mdee

Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee na Mkurugenzi wa Jukwaa la Uchumi la Dunia kwa Bara la
Afrika(WEF) Elsie Kanza, ni miongoni mwa viongozi wanawake 11 wa kisiasa kutoka barani
Afrika waliotunukiwa tuzo ya kuwa viongozi wanawake wa juu wenye nguvu katika siasa.

wakati raia wengine wakibomolewa nyumba ambazo kama ilivyo ya Mchungaji Lwakatare,
zilijengwa kinyume cha sheria, Mbunge huyo amehamia na kuishi kwenye nyumba yake.

Serikali imetakiwa kumdhibiti na kumuondoa, kisha kuibomoa nyumba ya Mbunge wa Viti Maalum
(CCM), Mchungaji Getrude Lwakatare.

Mdee ambaye pia ni Waziri kivuli wa Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi,
aliunganishwa katika orodha ya wanawake jasiri katika masuala ya siasa barani Afrika kwa
mwaka 2012.

Zitto Kabwe
[h=5]Narudia, mwaka 2015 sitagombea Ubunge. Nitafanya kampeni ya Urais, ama mimi kama mgombea wa CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa CHADEMA. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo ni vema niwaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa wetu. Huu ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa Jimbo langu na mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005.[/h]

inabidi sasa turejee kauli mbiu za miaka 50 iliyopita za Uhuru ni Kazi. Tuseme Demokrasia ni Kazi. Demokrasia sio lelemama.

Bado hakuna kijana leo aliejitokeza wakuweza kusema anasimama kipekee na kupigana kiuzalendo. Vijana wengi bado wapo kuogopa senior party members na hawataki kuwaudhi viongozi wao wa juu for the most part even where it is clear there thinking is wrong and outdated.

Kwanini nasema hivi lazima tujue ya kwamba fikra ya vizazi huwa zinabadilika (there is much evidence on HR recruiting process on how to attract age groups) mfano wengi waliozaliwa kabla ya uhuru na leo ni viongozi ni watu ambao waliopitia kwenye socialization process ambayo walipopata elimu kipindi hicho walikuwa considered ni privilege na wao walitambua hivyo.

Therefore you expect these people to demand respect kutokana na wao walivyolelewa na kukuzwa kwenye jamii. Na ni watu ambao hawa expect challenges from there subordinates even in sectors where they must be challenged.

Tofauti ni kwamba viongozi vijana wa leo wengi wametokea kwenye system ambayo privilege is not so much the case kuliko huwezo, kiongozi imara au mzalendo wa leo ni yule ambaye anaweza challenges za dunia ya leo, kama ni siasa inabidi kuelewa wasio nacho hawawa-angalii tena wasomi kama zamani (ni watu spesho) hivyo wanahitaji kuelimishwa kuhusu matendo ya siasa na maamuzi ya kisiasa vinginevyo fujo na hasira kwenye jamii zitakuwepo kutokana na baadhi ya maamuzi.

Yote kwa sababu maamuzi mengi bado yanatokana na watu ambao wanadhani ni spesho (generation independence) na arrogance yao imezidi kiasi kwamba ufisadi pia wanadhani si swala la kuulizwa. Kwakuwa viongozi wa leo wanashindwa kuwaelimisha those days are gone and cant challenge them for their decisions wao ni kuitikia, kuhamasisha au kukaa kumya. Ni kielelezo tosha hawajui siasa za leo hivyo si wakuitwa wazalendo.
 
Mods naomba mniwekee poll nimemwongeza Zitto kabwe kutokana na mambi ya wachangiaji.
 
Zitto ni kinyonga ambaye hadi sasa rangi yake haijajulikana hivyo haakisi taswira ya kijana anayetakiwa hapa

mtasema mengi juu ya Zitto lakini ukweli ni kwamba ktk wote waliotajwa hapo hakuna wa kumlinganisha na Zitto
 
Kweli bazee Zito ni jembe mim namkubali zingine shutuma zinazotolewa ni fitina tu
 
Wakuu,

nimekuja na hoja yangu ya msingi kabisa kwamba tunataka tumtambue mwanasiasa kijana ambaye anaweza
kutuvusha 2015. Kutuvusha si kwa maana agombee urais la hasha bali kwa matendo yake basi awe mfano wa kuigwa
kwa sisi vijana wenzake na taifa kwa ujumla. kama mnavyojua taifa bila vijana basi hilo ni taifa ufu. kijana
huyu atambulike kitaifa.

Katika topic hii nimechukulia kijana ni yule mwenye miaka 30 hadi 45. sote na wengi wachangiaji wa jukwaa hili
karibia 80% tuna umri huo na sasa tumpate huyu kijana mwezetu ili awe role model (mfano wa kuigwa) wetu na
tumtambue kitaifa na kumheshimu.

Nimejaribu kuangalia na kupitia pitia baadhi ya wanasiasa vijana nimekuja na mapendekezo ya majina sita - nafikiri
kati ya haya tunaweza kumpata huyu role model wetu. Nasisitiza hoja ziwe:

1. Uzalendo wa taifa lake
Kijana huyu awe amejitoa kwa taifa lake, bila kujali itikadi yake awe radhi kupoteza uhai kwake kwa nchi yake
awe mtetezi wa wanyonge, asiye mwoga wala mbadhirifu wa mali za umma. Asiwe na tamaa kiasi anaweza
kununuliwa au kurubuniwa na mafisadi.

2. Maisha na uhusiano wake na jamii inayomzunguka(matendo yake);
Asiwe na kashfa ya ufisadi, uzinzi, wizi wa mali ya umma na mambo, umalaya na mambo yoyote machafu ambayo
jamii imekuwa inayapigia kelele. asitumie uheshimiwa wake kujipatia kipato binafsi na mengine yanayofanana nahayo.

3. Awe mwerevu -- uwezo wake kiakili hapa tutaangalia hoja zake alizowahi kuzitoa iwe bungeni au hata katika
mikutano ya hadhara ndani na nchi ya nchi jee zina mantiki kwa jamii yetu, je ni mifano ya kuigwa kwa jamii.
Tunamwangalia pia uhusiano wake na wanasiasa wenzake ndani na nje ya chama chake. Overall mchango wake
ndani ya chama na taifa kwa ujumla.

4. Awe anapendwa na watu wa jimbo lake na jamii kwa ujumla

Tukishampata atakuwa na heshima kwa vijana wote na sisi sote tutamheshimu kama role model wetu.
Nimependekeza majina sita, narudia Udini, ukabila, uchama havina nafasi katika hoja yangu.

1. John Mnyika - Mbunge wa jimbo la ubungo DSM -- CDM
2. Januray Makamba - Mbunge jimbo la Bumbuli -- CCM
3. Deo filikunjombe - Mbunge jimbo la Ludewa - CCM
4. Peter Serukamba - Mbunge jimbo la Kigoma Mjini - CCM
5. Godbless Lema -- Mbunge jimbo la Arusha Mjini - CDM
6. Halima Mdee - Mbunge jimbo la Kawe DSM - CDM
7. Zitto Kabwe - Mbunge jimbo la Kigoma kaskazini - CDM

katika uchaguzi wangu nimetumia vigezo vitatu hapo juu, narudia tena tujadili hoja hizo - tunamtaka kijana mzalendo
role model wetu ambaye tunaweza kumtambua kitaifa kwa jina la MR & MRS - Tanzania 2015.

QUOTES

Mh. John Mnyika.

Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), Mhe. John Mnyika ametolewa nje ya bunge muda huu na
Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kukataa kufuta kauli yake kuwa Rais Kikwete ni dhaifu
wakati alipotakiwa kufanya hivyo. Mnyika ametolewa nje ya bunge wakati wabunge wakichangia
mjadala wa bajeti ya serikali mwaka wa fedha 2012/13 iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni.
Mnyika atarudi bungeni kesho saa tatu asubuhi.

Mnyika: Tumefika hapa tulipo kwa Udhaifu wa Rais Kikwete - YouTube

Mh. Deo Filikunjombe
Hivi punde katika Kongamano ya miaka 51 baada ya uhuru, mwasiasa machachari na mbuge wa
Ludewa Mh. Deo Filikunjombe ametoboa ukweli kuwa kuna kasumba na dhana potofu miongoni mwa
watanzania wakidhani kuwa nchi hii (Tanzania) ni mali ya CCM. Hii nchi si mali ya CCM bali
ya watanzania

Mhe Peter Serukamba

Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia CCM Mhe Peter Serukamba amesema suala la baadhi ya wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupinga posho lilikuwa ni unafiki.

Mh. Godbles Lema
“Vitisho ni vingi hatutaogopa nipo tayari kwa jambo lolote lile sitaacha harakati nipo
tayari kufa hata sasa. Taarifa na ushahidi tunao kwamba kila kinachoendelea sasa kwenye
siasa kinaratibiwa na Idara ya usalama wa taifa. Katika kutafuta ufumbuzi wa nchi kuna watu ambao
watatolewa sadaka na sisi tupo tayari kutolewa sadaka.

Mh. January Makamba

wote waliozaliwa kabla ya 1961 waachane na mawazo ya Urais maana watatupotezea muda ...
tunahitaji rais wa dot.com atakayeendana na changamoto za leo

Mh. Halima mdee

Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee na Mkurugenzi wa Jukwaa la Uchumi la Dunia kwa Bara la
Afrika(WEF) Elsie Kanza, ni miongoni mwa viongozi wanawake 11 wa kisiasa kutoka barani
Afrika waliotunukiwa tuzo ya kuwa viongozi wanawake wa juu wenye nguvu katika siasa.

wakati raia wengine wakibomolewa nyumba ambazo kama ilivyo ya Mchungaji Lwakatare,
zilijengwa kinyume cha sheria, Mbunge huyo amehamia na kuishi kwenye nyumba yake.

Serikali imetakiwa kumdhibiti na kumuondoa, kisha kuibomoa nyumba ya Mbunge wa Viti Maalum
(CCM), Mchungaji Getrude Lwakatare.

Mdee ambaye pia ni Waziri kivuli wa Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi,
aliunganishwa katika orodha ya wanawake jasiri katika masuala ya siasa barani Afrika kwa
mwaka 2012.

Zitto Kabwe
Narudia, mwaka 2015 sitagombea Ubunge. Nitafanya kampeni ya Urais, ama mimi kama mgombea wa CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa CHADEMA. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo ni vema niwaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa wetu. Huu ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa Jimbo langu na mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005.

inabidi sasa turejee kauli mbiu za miaka 50 iliyopita za Uhuru ni Kazi. Tuseme Demokrasia ni Kazi. Demokrasia sio lelemama.

nawakilisha.
Upo sawasawa ila Zitto please M-delete hafai hata kidogo.
 
Mnyika upo juu sana!

Zitto ni jembe kwa panya 2 haaminiki.
 
Back
Top Bottom