WADAU NAWASALIMU SANA, naomba nipate mchango wenu kimtizamo wa chanya zaidi kwa maslahi ya vyama vyetu na Taifa kwa ujumla,katika miaka ya hivi karibu kuanzia 2010 mpaka sasa kuelekea uchaguzi mkuu 2015 pamekuwepo na vijana utitiri kuwa wanasiasa ama kwa ushabiki tu au kuwa na uzalendo,mosi kumekuwepo na vijana wanasiasa wadogo ambao wamekuwa tunu kwa taifa jinsi wanavyojenga hoja nzito nzito kwa mawanda mapana yenye nia ya dhati kuleta maendeleo ya jamii zetu na imefika mahali jamii hizo imewakubali hao vijana na kuona kuwa ndio marais wajao,mawaziri na wabunge wanaokuja baadaye,mathalani kuna vijana wanasiasa NGULI kama ZITO KABWE,JAMES MBATIA,MWIGULU MCHEMBA,JOB LUSINDE wameonekana kuwa wana maono mapana na taifa letu kwa hoja zao nzito. Na kuna wanasiasa NGUMBARU kama JOHN MNYIKA,LEMA,HALIMA MDEE,JAMES KAFULILA,MACHALI,MKOSAMALI,STEVEN MASELE,TUNDU LISU,WENJE,MSIGWA ,JANUARY MAKAMBA n.k ambao wanachipukia kwenye siasa hizi za leo kwa takribani miaka mitano,swali je katika hawa vijana wanasiasa baadhi niliotaja hapa na wengine wanaofahamika ni mwanasiasa yupi anakubalika na kupendwa na jamii na anayefaa kuendelea kuwa kiongozi wao ?. naomba michango yenu kwa maslahi ya taifa letu.nawasilisha