Mwanasheria Mkuu: Serikali haitagharimia Mahakama ya Kadhi

Mwanasheria Mkuu: Serikali haitagharimia Mahakama ya Kadhi

Hapa nimewasema wanawake nikirelitisha na wanaume,kwa mfano huko saudi arabia wanawake hawaruhusiwi kuolewa hadi kaka yake akubali,au ndugu yake yeyote yule wa kiume,kwenye talaka pia mwanamke anaondoka bila chochote,au labda ningetumia neno haki za wanawake ndo ningeeleweka vizuri,nimesema uhuru nikimaanisha kipengele cha haki sawa kwa wote,unaweza ukawa na uhuru na usiwe na ruhusa ya kufanya mambo flani,hivyo uhuru unakuwa sio 100 perce
Nimekupata!

Hata hivyo, Haki za binadamu ni mjadala mpana sana katika dunia hii inayochagizwa na mazingira ya uwepo wa haki za kisheria na haki za kiitikeli.

Hizo unazoziona ni haki za wanawake au wanaume inawezekana wanawake au wanaume wa Saudi Arabia hawazioni katika mtazamo wako bali wanaona ndiyo sehemu ya maisha yao katika uwepo wao.

Kuziondoa inawezekana ikaonekana ni kuwaondolea haki yao!
 
Mwanasheria mkuu wa Tanzania mh. George Masaju amesema serikali haitajihusisha na mahakama hiyo kwa vile inaanzishwa kwa misingi ya kidini na serikali ya jamhuri ya muungano haina dini.

Taarifa ya habari saa 2 ITV.

mahakama ya kadhi??
 
Last edited by a moderator:
Wewe kama unataka haki sawa baina ya ke na me, mpeane zamu na mumeo ya kubeba mimba na kuzaa


SHERIA YA MUNGU USIILETEE HOJA ZAKO ZA BEJING

mungu wako siyo lazima awe mungu wa kila mtu.
Serikali haina dini ila watz tuna haki ya kuwa na dini kila m1 kwa utashi wake.
 
Mahakama ya kidini ya kikatoliki imezindua leo shughuli zake kwa mwaka huu. Sisi pia tunazindua kesho kitaifa hahaha
 
safi sana mwanzo mzuri ikianza kazi mtaikubali na mta ruhusu tupate rudhuku.sasa munazani ni ya kukatana mikono na kupigana mawe,Kenya Uganda hata Zenji inagharamiwa na Serikali.mdogomdogo tutaelewana tu sisi ndgu.
 
Mpuuzi huyu, aache hizo danganya toto! Katika Uislamu, Mahakama ya Kadhi, ni Ibada! Serikali inajihusishaje na Ibada ya Dini moja? Kumbe ndiyo sababu ya Masaju kupewa nafasi hiyo, ili atuletee chokochoko za kidini! Apotelee uchochoroni! MAHAKAMA YA KADHI TANZANIA, HAIKUBALIKI!!!!!! Period!

Mkuu uhuru wa kuabudu kwako una maana gani?
 
mwana04.jpg



Mwanasheria mkuu wa serikali Mh. George Masaju amesema mahakama ya kadhi itakayoanzishwa kisheria haitahudumiwa na serikali na itakuwa ya hiari kwa waumini wa dini ya kiislamu watakaoiridhia katika masuala ya ndoa, talaka, mirathi pamoja na wakfu na kutaka wanasiasa kuacha kukuza mijadala ya suala hilo kwa maslahi yao binafsi.
Akizungumza katika mahojiano maalum na vyombo vya habari vya IPP Bw.Masaju amesema uwepo wa mahakama hiyo utaisaidia serikali katika kuipunguzia mzigo wa mlundikano wa kesi uliopo hivi sasa hivyo ni bora dini zote zikaiunga mkono.

Aidha mwanasheria mkuu huyo wa serikali amekiri madhaifu yaliyofanywa na serikali ya kutotoa elimu kuhusiana na faida ya mahakama ya kadhi kuwa yamechangia pia mjadala kuhusiana na uanzishwaji wake.

Kuhusiana uwepo wa mjadala huo kulenga kuifanya jamii iache kujadili mambo yanayolikabili taifa ambayo ni upigaji kura ya maoni ya katiba pendekezwa, uandikishwaji wa wapiga kura pamoja na uchaguzi mkuu amesema.

source ITV

Hivi huyu Mwanasheria mkuu Jaji George Masaju anaongea yeye kama mwenye taaluma ya sheria au vipi? Issue sio gharama bali ni kujadili suala la kidini ndani ya serikali na kulifanya litambulike kisheria.

Nafikiri watanzania wote tunahitaji kufanyiwa scanning ya ubungo ili kuona kama bongo zetu ziko sahihi kwani shule tumeenda lakini tuna-behave kama bado tunaishi kwenye mapango i.e. zama za mawe ila hata wale wa zama za mawe hawawezi kuwa kama baadhi yetu!
 
Yaani kweli nimfuge nguruwe wangu, na wakati namfuga mara bucha langu linachomwa moto, na nikifanikiwa kumuuza kodi yangu iende serikalini na baadae iende kwenye ibada!!! wakati huo ulikuwa unanikebei,unanichomea bucha langu, unaniita kafiri na kunikatisha tamaa kufanya mradi huo…ningekufikiria kama ungenisapoti!!!
Dini yangu inanikataza nisitoe talaka na kwamba nikioa ni huyo huyo mpaka Mungu atakapotuachanisha..sasa itakuwaje kodi yangu ika shiriki ktk kutoa talaka???!!!
Mbona kufanya ibada zinazofanyika serikali haikuombwa kutoa ruhusa??? Ibada ya kuswali,kutoa taraka nk mbona serikali haikuombwa ruhusa??
 
safi sana mwanzo mzuri ikianza kazi mtaikubali na mta ruhusu tupate rudhuku.sasa munazani ni ya kukatana mikono na kupigana mawe,Kenya Uganda hata Zenji inagharamiwa na Serikali.mdogomdogo tutaelewana tu sisi ndgu.

Kwa nini hoja ya mahakama ya kadhi hushamiri kila kipindi cha uchaguzi kikifika?
 
Suala hili wanasiasa waliojifia ndiyo wamelifanya ndiyo hoja kwao.
 
Yaani kweli nimfuge nguruwe wangu, na wakati namfuga mara bucha langu linachomwa moto, na nikifanikiwa kumuuza kodi yangu iende serikalini na baadae iende kwenye ibada!!! wakati huo ulikuwa unanikebei,unanichomea bucha langu, unaniita kafiri na kunikatisha tamaa kufanya mradi huo…ningekufikiria kama ungenisapoti!!!
Dini yangu inanikataza nisitoe taraka na kwamba nikioa ni huyo huyo mpaka Mungu atakapotuachanisha..sasa itakuwaje kodi yangu ika shiriki ktk kutoa taraka???!!!
Mbona kufanya ibada zinazofanyika serikali haikuombwa kutoa ruhusa??? Ibada ya kuswali,kutoa taraka nk mbona serikali haikuombwa ruhusa??

Taraka=Talaka
 
Inasikitisha kuona mtu ana comment kitu asichokuwa na hakika nacho. Dada uliyepost hapo juu unapotosha.

mifano tunaiona kwa nchi za kiislamu na ilo liko wazi wewe inaonekana unakubali kitu ambacho hujui,haki za wanawake zinaenda kupotea .Nchi za Kislamu mwanamke hana haki kabisa,anatumika kama chombo cha STAREHE NA KUJIFUNGUA TU
 
Kama majaji walipata mgao ESCROW. Mi naona bora tuanzishe SHARIA kama SAUDI ARABIA tujue moja ukiiba unakatwa kichwa
 
Hawa jamaa kutaka kubebwa na serikali ndio maana hata mashule,hospitali wameshindwa kujenga zao.Walizonazo hazilingani na muda ambao hii dini imekuwepo hapa nchini.

Mbadikike na muwe wabunifu.

Hivi we bavicha kwanini usinyamaze muda mwingine?
 
Back
Top Bottom