Mwanasheria Mkuu: Serikali haitagharimia Mahakama ya Kadhi

Sengeon

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
529
112
Akizungumza kupitia taarifa ya habari Itv Mwanasheria Mkuu ametangaza Rasmi kuwa Mahakama ya Kadhi itahudumiwa na Waislamu Wenyewe.

Amesema kuwa Serikali haina Dini na Kamwe haitajihusisha na maswala ya imani za Kidini.

Mwanasheria pia amesema kuwa Mahakama hiyo ilishakuwepo na ilikuwa ikihudumiwa na Waislamu wenyewe.

Hii ni Habari njema sana kwa wale wote ambao walikuwa wanajisikia vibaya kugharamia Dini isiyokuwa yao.

Naipongeza sana Serikali kwa kuamua hivyo.

Mungu ibariki
Tanzania.
===================

Wakati muswada wa kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi ukitarajiwa kujadiliwa katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, amesema haitakuwa na athari yoyote hasi nchini.

Masaju alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza katika mahojiano maalum na NIPASHE jijini Dar es Salaam akifafanua juu ya muswaa huo hasa baada ya kuwapo kwa dalili za mvutano kuhusu uanzishwaji wa mahakama hiyo.

Alisema tatizo lililopo ni kwamba serikali haijachukua hatua madhubuti kuwaelimisha wananchi namna ambavyo mahakama hiyo itakuwa inaendesha kazi zake.

"Suala la Mahakama ya Kadhi limekuwapo tangu zamani na ilikuwa ahadi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Serikali hatuoni kwa nini suala hili lisifanikiwe," alisema.

Masaju alisema Watanzania lazima watambue kuwa Mahakama ya Kadhi itahusu mambo ya Waislamu wenyewe ambayo ni mirathi, ndoa na talaka.

"Sioni kwa nini isifanikiwe kwa sababu mahakama hii haiwahusu watu ambao siyo Waislamu na pia haitakuwa ya kulazimisha," alisema.

Alisema Mahakama hiyo kwa sababu itakuwa inashughulikia masuala binafsi kama ndoa na talaka ambayo serikali haishughuliki nayo.

Alisema serikali imekuwa ikishughulika na masuala ya jinai kama vile wizi, watu wanaokula rushwa hivyo mambo binafsi kama ya talaka haishughuliki nayo.

Aliongeza kuwa kujiunga katika Mahakama ya Kadhi itakuwa ni hiari hata miongoni mwa Waislamu na gharama za uendeshaji wake serikali haitahusika.

Masaju alisema suala hilo kama wananchi wakielimishwa haliwezi kuleta mgogoro kwa kuwa ni kitu cha kawaida na linafanyika katika baadhi ya nchi.
Alisema kimsingi suala hilo linakuzwa na baadhi ya vyombo vya habari na kusisitiza kuwa Watanzania ni wamoja na watabaki kuwa wamoja.

Aliongeza kuwa watu ambao hawataki mahakama hiyo wataenda kwenye mahakama nyingine za kawaida.

"Pamoja na Mahakama ya Kadhi kuamua masuala hayo, mahakama za kawaida zitabaki kuwa na mamlaka ya kusikiliza masuala ya talaka, mirathi na ndoa," alisema.

Alisema wakati wa Bunge Maalum la Katiba Waislamu walitaka suala hili liingizwe katika Katiba mpya, lakini serikali iliona yasiingizwe kwa sababu ni ya imani za dini na hivyo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliahidi serikali itapeleka muswada bungeni.

Akijibu swali la kwamba huenda kuwasilishwa bungeni kwa muswada huo sasa kunalenga kuvuruga Watanzania kuacha kufikiri masuala muhimu yaliyopo mbele kama uchaguzi mkuu, Masaju alisema siyo kweli.

Alifafanua kuwa masuala yote kama ya kura ya maoni kuamua Katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu yote yana umuhimu na yataenda sambamba.

"Wakristo ni majirani wa Waislamu, Waislamu na Wakristo wanaishi pamoja, katika baadhi ya familia wengine kuna Waislamu na Wakristo, mwanasheria mmoja aliniuliza ni amri ipi iliyokuu kuliko yote akasema, mpende Mungu wako kwa moyo wako wote, mpende jirani yako kama nafsi yako, Waislamu ni jirani zetu," alisema.

Masaju alisema kutugwa kwa sheria hii ni kuwezesha Mahakama ya Kadhi kufanya kazi kwa kufuata utaratibu bila kuingilia mambo mengine ya serikali.

"Hii siyo mara ya kwanza kutunga sheria. Mtusaidie kama taifa, sioni sababu Watanzania kupigana na kupinga suala la Mahakama ya Kadhi na kusababisha kuvunjika kwa amani," alisema.

Aliongeza kuwa Zanzibar wana Mahakama ya Kadhi, hivyo itakuwa jambo la kushangaza kwa nini Tanzania Bara kusiwe na mahakama hiyo hali ambayo italeta manung'uniko kwa Waislamu waliopo bara.

Alisema kwa waliosoma Chuo Kikuu cha Sheria Dar es Salaama suala la mahakama ya Kadhi hufundishwa kwa mwaka mzima ili kulielewa vizuri.

Alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inatumika hata Zanzibar, hivyo siyo jambo zuri bara kusiwe na Mahakama ya Kadhi kwani itawafanya Waislamu waliopo bara wasononeke.

"Tumeona Waislamu wanaona na Wakristo, hiki ni kitu cha kawaida kabisa hakuna sababu ya kulipinga, sisi wote tunategemeana, sisi ni ndugu, binadamu tunaoishi pamoja.
Suala la Mahakama ya Kadhi limekuwa likizungumzwa sana bungeni tangu Augustino. Mrema alipopeleka hoja binafsi akidai Mahakama hiyo mwaka 1998.

Tangu wakati huo mwaka 1998 - 2000 iliundwa kamati ndogo ya Bunge kulishughulikia suala hilo chini ya Mwenyekiti wa wakati huo, Arcado Ntagazwa, aliyekuwa mbunge wa Muhambwe na baadaye liliibuliwa tena mwaka 2002 na Thomas Ngawaiya aliyekuwa mbunge wa Moshi Vijijini na likashughulikiwa na Kamati ya Katiba, Utawala na sheria chini ya Mwenyekiti wa wakati huo, Athumani Janguo akiwa mbunge wa Kisarawe.

Baadaye suala hilo lilirudishwa serikalini chini ya Tume ya Kurekebisha Sheria kati ya 2006 -2008. Tume hiyo ilikuwa chini ya Mwenyekiti Profesa Ibrahimu Juma.

Chanzo: IPP Media
 
Kuna uzi hapa , wameulizwa mahakama ya kadhi ni nini? Wameshindwa jibu.
 
mwana04.jpg



Mwanasheria mkuu wa serikali Mh. George Masaju amesema mahakama ya kadhi itakayoanzishwa kisheria haitahudumiwa na serikali na itakuwa ya hiari kwa waumini wa dini ya kiislamu watakaoiridhia katika masuala ya ndoa, talaka, mirathi pamoja na wakfu na kutaka wanasiasa kuacha kukuza mijadala ya suala hilo kwa maslahi yao binafsi.
Akizungumza katika mahojiano maalum na vyombo vya habari vya IPP Bw.Masaju amesema uwepo wa mahakama hiyo utaisaidia serikali katika kuipunguzia mzigo wa mlundikano wa kesi uliopo hivi sasa hivyo ni bora dini zote zikaiunga mkono.

Aidha mwanasheria mkuu huyo wa serikali amekiri madhaifu yaliyofanywa na serikali ya kutotoa elimu kuhusiana na faida ya mahakama ya kadhi kuwa yamechangia pia mjadala kuhusiana na uanzishwaji wake.

Kuhusiana uwepo wa mjadala huo kulenga kuifanya jamii iache kujadili mambo yanayolikabili taifa ambayo ni upigaji kura ya maoni ya katiba pendekezwa, uandikishwaji wa wapiga kura pamoja na uchaguzi mkuu amesema.

source ITV
 
Sasa ni kinini kinafanya sheria iende bungeni kuanzisha hii mahakama? Kama ni ya waislamu tena amesema ni ya hiari alafu itagharamiwa na waislamu wepi? Kivipi? Sheria itaweka utaratibu wa kugharimia? Na hii sheria ni ipi?

Kitu cha hiari hakidumu. Nisawa na ujamaa. Kila kitu ni Mali ya umma matokeo yake hakuna anayewajibika. Na isitoshe kwenye kesi kuna mshtaki na mshtakiwa na mara nyingi mshtakiwa akipewa awe na hiari haendi mahakamani.

Hapa kuna kitu kimejificha. Either mwanasheria mkuu kasema uongo ili mwanaharamu apite au kuna ajenda ya kisiasa.
 
hii mahakama hii isije ikaonea tu wanawake,maana nchi zenye sharia wanawake hawana uhuru kabisa,kuolewa tu ni mpaka kaka yake akubali,mwanamke akipewa talaka haondoki na kitu,hizo mahakama zinafundiwa na Saudi arabia huko matajiri wa mafuta
 
Nadhani hapo Sasa huu mjadala utakuwa umepatiwa njia rahisi ya ufafanuzi......... Pence wengi hapaharibiki jambo,ishu ndogo ilikuwa inaelekea kuligawa Taifa.
 
Sasa ni kinini kinafanya sheria iende bungeni kuanzisha hii mahakama? Kama ni ya waislamu tena amesema ni ya hiari alafu itagharamiwa na waislamu wepi? Kivipi? Sheria itaweka utaratibu wa kugharimia? Na hii sheria ni ipi? Kitu cha hiari hakidumu. Nisawa na ujamaa. Kila kitu ni Mali ya umma matokeo yake hakuna anayewajibika. Na isitoshe kwenye kesi kuna mshtaki na mshtakiwa na mara nyingi mshtakiwa akipewa awe na hiari haendi mahakamani.
Hapa kuna kitu kimejificha. Either mwanasheria mkuu kasema uongo ili mwanaharamu apite au kuna ajenda ya kisiasa.

Akifanya propaganda, malengo utapeli kura za waislam uchaguzi mkuu.
 
hii mahakama hii isije ikaonea tu wanawake,maana nchi zenye sharia wanawake hawana uhuru kabisa,kuolewa tu ni mpaka kaka yake akubali,mwanamke akipewa talaka haondoki na kitu,hizo mahakama zinafundiwa na Saudi arabia huko matajiri wa mafuta
Uhuru wa wanawake ni upi na mipaka yake ni ipi?
 
Hawa jamaa kutaka kubebwa na serikali ndio maana hata mashule,hospitali wameshindwa kujenga zao.Walizonazo hazilingani na muda ambao hii dini imekuwepo hapa nchini.

Mbadikike na muwe wabunifu.
 
Hii ina dhiirisha makafiri wengi wanaochangia humu jf ni mbululaz au wanachuki binafsi maana huu muswada ulishawekwa wazi na kila mtu angeweza kuuona then ndo wangesema huo upuuzi wanaofikiria

Taarifa ya habari Itv umeitazama usiku huu saa mbili? Ndivyo alivyoongea.
 
Haaa Haaa Haaa Haaa.
Hii kitu ni ngumu sana kukubalika hasa upande wa Serikali maana haina Dini. ♧♧♣♣
 
Uhuru wa wanawake ni upi na mipaka yake ni ipi?
Hapa nimewasema wanawake nikirelitisha na wanaume,kwa mfano huko saudi arabia wanawake hawaruhusiwi kuolewa hadi kaka yake akubali,au ndugu yake yeyote yule wa kiume,kwenye talaka pia mwanamke anaondoka bila chochote,au labda ningetumia neno haki za wanawake ndo ningeeleweka vizuri,nimesema uhuru nikimaanisha kipengele cha haki sawa kwa wote,unaweza ukawa na uhuru na usiwe na ruhusa ya kufanya mambo flani,hivyo uhuru unakuwa sio 100 perce
 
Back
Top Bottom