Mwanasheria mkuu mpya wa Serikali ni dhaifu sana!

Mwanasheria mkuu mpya wa Serikali ni dhaifu sana!

Siasa na uendaji ni vitu viwili tofauti. Kujieleza kwa mdomo na kuandika ni vitu viwili tofauti; wasema uongo kama wanasiasa wanaweza kuzungumza jukwaani hata masaa mawili lakini ukimwambia aandike anaweza kushindwa kujaza kurasa mbili kwa maneno yake mwenyewe.

Mwanasheria mkuu alikuwa mtendaji si mwanasiasa. Na watendaji wamezoea kutafuta reference kabla ya kuzungumza
 
Kwa hakika huyu AG mpya ni pigo kubwa kwa watanzania.Kwa kweli amepwaya kupita kiasi!

Tangu aingie ofisini kwa mwezi sasa huwezi kuamini kama ni mwamasheria aliyeiva kiasi cha kupewa cheo kikubwa namna hiyo!

Akiitisha vikao vya kiofisi hadi unamuonea huruma! Kujieleza hajui! Kichwani anaonekana kama haijui sheria kwa kiasi kikubwa mno! Mikataba haijui vizuri kama mtu mwenye cheo cha juu serikalini!

Ikiwa hayo hayajatulia leo akaongea bungeni kwa mara ya kwanza kwenye hoja nzito! Kujieleza kukamshinda tena! Hajui kutofautisha kati ya waziri wa mambo ya nje na waziri wa mambo ya ndani! Hivi kweli Mathias Chikawe ni waziri wa mambo ya nje? Ameishia kutoa maelezo ya juu juu tu eti jambo liko mahakamani lisijadiliwe! Kwa kiwango kipi lisijadiliwe? Kweli ameshindwa kuweka vigezo vya kipi kijadiliwe na ni kipi kisijadiliwe? Mbona spika ambaye ni bush lawyer ameweza?
Miongoni mwa sifa za anayepewa cheo kikubwa kama hicho ni kujiamini na kuhakikisha makosa ya hovyo wakati wa kujieleza hayatokei! Vingine basi huo utakuwa ni udhaifu mkubwa!

Huyu AG kwa kweli ukifanya naye kikao hadi unamuonea huruma! Ni mweupe na asiyejiamini!

Huyu cheo alichopewa ni mzigo mzito kwake na watanzania hatuna siku mbili mtajionea haya ninayowaambieni leo!

Tumpe muda huenda akazoea mazingira na akafanya vizuri. Ingawa anaonekana sio muongeaji mzuri
 
Wote mliomsupport mtoa mada ni empty tins

Huwa ni vigumu kukubali ingawa inawezekana. Muhimu pia kujua weledi wa anaetukana wenzie. Kwa kawaida mgonjwa wa akili sio rahisi kujijua hata aambiwe kuwa kaharibkiwa
 
Mtoa mada mbona babako ni dhaifu watu hawasemi, anza na babako, then uwaseme wengine

Baba yake unamfahamu au unataka kuwafurahisha wanajamvi? Inawezekana pia una udugu wa karibu na mrithi wa Werema.
 
Obama mbona muongeaji sana lakin kauporomosha uchumi wa marekani,Utakuwa unakufuru kwa Mungu,Mungu ndiyo anaumba vinywa vya wanadamu.Nabii Musa hakuwa muongeaji kwa taarifa yako lakn Mungu alimtumia.

Obama kaporomosha uchumi wa Marekani kuliko Bush!!?? Unamfananisha Nabii Musa na mwanasheria mkuu aliechaguliwa kidhaifu na kiongozi dhaifu!!??

Mtu aliesoma na kukabidhiwa cheo then hawezi kujieleza ni mpumbavu tu.... hana akili kabisa!!
 
Jamaa ni Boya kabisa yaani Tundu Lissu anampelekesha sana. Ni kuhusu kikao kinachoendelea sasa hivi tar.20.03.2014 Muswada wa Sheria ya wakala wa usimamizi wa maafa ya mwaka 2014. Anajing'ata sana,kigugumizi kingi,mara ajikune kichwani sidhani kama atamudu mikiki mikiki ya Bunge hili... Na bado Wabunge wa Zanzibar hawajamjia juu.
 
Eti AG anadai akisoma hiyo Sheria kwa kiingereza ndo inakuwa tamu. Naona ka-panic.
 
Maskini mpaka Mh.Sitta anamuonea huruma mpaka anamnong'oneza kuwa "DON'T ARGUE WITH HIM" Pale Masaju alipoanza kumjibu Lissu "Ngojaaa ngojaaaa"
 
Wamezima UMEME bungeni wakati Mkosamali anachangia,kwa kweli Mwenyekiti Zungu anambeba sana Masaju.
 
ila mshahara mwenzako upo pale pale mwisho was mwezi
 
Back
Top Bottom