Mwananyamala Hospital, Hali Mbaya Wodini!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwananyamala Hospital, Hali Mbaya Wodini!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwita Maranya, Mar 29, 2012.

 1. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wadau,
  Nilikuwa hospitali ya mwananyamala kumjulia hali ndugu yangu aliyelazwa pale.
  Kwakweli nilichokishuhudia wodi ya watoto ni cha kusikitisha sana. Watoto wamelazwa watatu kila kitanda kimoja na wengine wamelazwa chini!!
  Kutokana na wodi hiyo ya watoto ''kufurika'' manesi na wauguzi wameamua kuzuia watu wanaokwenda kuwaona wagonjwa wao kuingia wodini, hivyo kuwalazimisha wanaouguza watoto kutoka nje kuongea na ndugu zao ama kupokea vyakula.
  Kwa hali ya sasa ya mfumko wa magonjwa, na kwa namna wodi ya watoto ilivyofurika, ni dhahiri kuwa hali za watoto waliolazwa ziko shakani huenda wakajikuta wanaambukizwa magonjwa wasiyotarajia kutokana na mazingira walimolazwa.

  MY TAKE:
  Serikali inapashwa kuchukua hatua za haraka ili kuwanusuru watoto wetu na kadhia wanayokumbana nayo ktk hospitali zake, na bila shaka itaanza na hospitali ya Mwananyamala.
   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Madaktari walienda Ikulu kumaliza kero zote hizo...sasa hivi wanaamini hali ni shwarii...:ranger:
   
 3. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Sasa hapa kwa ukweli sijui ni nani wakuonewa huruma!!Madaktari walijitosa,wakawa wanahitaji support yetu kidogo tu,tukawatosa!!!
  Nakumbuka kuna mwana JF mmoja aliorodhesha haki za msingi za mtanzania wa sasa!
  Kukosa matibabu,ni haki ya msingi
  Kukosa ajira,kukosa elimu,kutukanwa majukwaani,pia tunaona ni haki ya msingi!

  Kwa mtaji huu,itatuchukua muda mrefu sana,kujua nini kifanyike kutoka hali mbaya kwenda kwenye unafuu!!
   
 4. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Acha uvivu wa kufikiri, siku mwanao analazwa kitanda hicho na wengine wawili hutayasema haya! Wanaoteseka ni watanzania wasio na kosa
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  hela zipo arumeru saa hizi
   
 6. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwita Maranya, karibu Tanzania, habari ya huko utokako?!, hivi wewe ndo umegundua leo leo kuwa kwenye hosp za serikali hasa hapa dar es salaam mgonjwa zaidi ya mmoja hulala kwenye kitanda kimoja?!, mbona hili nila zamamni sana?!, hata hivyo, hili la watu kuzuiwa kuingia ndani ya wodi ya watoto mbona tulishazoea kuwa ndio utaratibu?!. Nakuunga mkono kuwa hali ni mbaya pale mwananyamala, lakini hali ni hivyo hata temeke na amana. Pendekeza nini kifanyike?
   
 7. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  HII NDIYO MOJA YA KERO YA MADAKITARI HATA WAKAAMUA KUGOMA. LAKIni kwa UFINYU WETU NA KUWEKA ITIKADI MBELE ZA SIASA HATUKUWAUNGA MKONO NA BADALA YAKE TUKAWA tunawatuhumu KUWA ETI ULE MGOMO NI KWA MASILAHI YAO BINAFSI YA MISHAHARA MIKUBWA. NA TUKADIRIKI HATA KUTAKA KUANADAMANA ETI KUPINGA MGOMO WA MADAKITARI, HATUKUISHIA HAPO TUKATAKA KWENDA KUWASHITAKI MAHAKAMANI.

  PTYUUUUUUUUUUUUUUUUUUU!!!!!! WATANZANIA TUMELOGWA NA ALIYETULOGA AMESHAKUFA!!!!!!!!!!!!

  MY TAKE: HAKUNA SABABU YA KULALAMIKA KWA HILI KWANI TUNAYAPENDA HAYA!!!!!!!!!!  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu wa kaya aliahidi kuyashughulikia matatizo yote yaliyobainishwa na madaktari, na akaahidi kuyapatia "majawabu" haraka iwezekanavyo.
  Badala ya kujipongeza kwa kikombe cha gahawa ungeonekana wa maana sana kama ungemkumbusha mkuu wa kaya atoe haraka "majawabu" ya matatizo ya sekta ya afya nchini.
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Pamoja na kwamba serikali ilijitahidi kuwatumia watanzania hao hao wanaoteseka kuwabandika sura mbaya madaktari hadi kuonekana hawafai mbele ya jamii, bado nadhani wanao wajibu wa kuendelea kupigania mazingira bora ya kazi.

  Na sisi wengine tusio madkatrai lakini kama tuna uwezo wa kusaidia kuchangia uboresaji wa huduma za afya tujitahidi kuendelea kuchangia, ndugu zetu wanapata shida sana katika kupata huduma za afya.
   
 10. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,635
  Likes Received: 1,992
  Trophy Points: 280
  Mods ipe Sticky thread hii ili tuwaonyeshe Watanzania wenzetu na ulimwengu mzima hali ya hospitali zetu.
   
 11. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Gama,
  Nipo jijini Dar es salaam mkuu sijatoka ng'ambo.
  Mara ya mwisho nilikwenda hospitali ya mwananyamala mwaka juzi mwezi wa kumi kumtolea damu ndugu yangu, alikuwa amelazwa pale, hali katika wodi ya watoto haikuwa vile nilivyoikuta leo. Temeke nilifika mara ya mwisho mwaka jana mwezi wa nane nilipeleka majeruhi wa bodaboda lakini hali haikuwa nzuri sana ingawa sikuona mtu amelazwa chini.

  Mkuu wangu nadhani katika hili la sekta ya afya (huduma za hospitali) kuna kazi kubwa sana ya kufanya, nadhani ni muda muafaka tutafute namna ya kuishawishi serikali iongeze bajeti ya wizara ya afya hasa katika uboreshaji na ukarabati wa miundombinu, kwani nyingi zilizopo zilijengwa miaka mingi sana na sasahivi zimeelemewa na wingi wa wagonjwa. Inapofikia hatua wagonjwa wawili ama watatu wanatumia kitanda kimoja hiyo ni wazi kwamba hospitali zetu zimezidiwa sana.
   
 12. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Tunaipenda ccm wakati yenyewe haitupendi
   
 13. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Na bado akina Rejeo wanaona CCM bado inafaa kutuongoza. Kweli nakubaliana na wadau waliotangulia katika makala zingine kwamba UKIONA NDUGU YAKO ANASHABIKIA CCM, INABIDI UMPELEKE KWA DAKTARI AKAPIMWE AKILI
   
 14. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye kuyashughulikia hayo matatizo yaliyoainishwa na maDaktari wakati wa mgomo sijui....lakini kuyatolea majibu ya haraka mbona mkuu wa kaya alishalifanya hilo! Na ilimchukua siku 2 tu kuyatolea majibu..na aliyatoa siku ile alipokutana na 'wazee wa Dar es salaam' kama kina mzee wa Upako etc! Majibu aliyoyatoa siku ile Tanzania nzima tunayajua...sisi (maDaktari) tulijaribu...tukashindwa...tunasonga mbele! Kazi kwenu waTanzania, zamu yenu sasa!
   
 15. raybse

  raybse Senior Member

  #15
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hali ni mbaya zaidi katika wodi zingine zote mkuu!! Mwananyamala Hospitali Huduma zinazotolewa pale za afya ni mbaya kiasi kwamba zinafikia hata kuvunja haki za msingi za Binadamu......jamani mi nadhani tusiwe wengi wa maneno matupu tu nyuma ya Keyboards zetu....Tufunge safari siku moja twende pale tukajionee wenyewe...HALI YA HUDUMA NI MBAYA NA NI ZA KIWANGO CHA CHINI SANA WAGONJWA WANALALA ZAIDI YA MMOJA....DAWA NA VIFAA TIBA HIVYO NDO HUSISEME!! HII MIGOMO YA MASAKTARI ILIYOPITA NDIO ILIKUWA LENGO KUU KATIKA HAYA YOTE!! WATANZANIA KAMA KAWAIDA YETU USHABIKI WA KIJINGA!! KWA HIYO TUSILALAMIKE MAY BE THIS IA WHAT WE DESERVE!!
   
 16. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Wanadamu tumepewa akili ya kutambua zuri na baya, lakini hatuitumii! Tumepewa akili ya kujiwekea mazingira bora ya kila sehemu lakini hatutaki kujishughulisha, viongozi walioko madarakani pamoja na uchache wao wengi wetu hatukutaka kuongozwa na wao, lakini bado wamelazimisha kutuongoza na hatuwezi kuwafanya kitu zaidi ya kulalamika na kujiongezea stress.
  Shida ya vitanda mahospitalini ni jambo ambalo linahitaji utashi wa viongozi wetu wa kizalendo, misitu tunayo na nguvu kazi tunayo! Unaajiri vijana ambao watakuwa kazi yao ni kutenengeza thamani za mahospitalini na shuleni nk ili kuondokana na hizi kero, lakini viongozi wetu kwa kuwa wote lao ni moja basi hawajui shida kama hizi.
  Tuwakatae 2015, watanzania wenzangu tuwakataeni hawa viongozi waroho jamani walishashiba hawajui wenye shida.
   
Loading...