Siku hizi watoto wadogo wengi sana wapo HIV positive. Na baahati mbaya katika michezo kuna vitu vyenye ncha kali watoto wamekuwa wakichezea na kushirikiana hususani nyembe za kuchongea penseli na nail cutter. Pia ktk kucheza pamoja endapo wana vidonda ni rahisi sana kuambukizana kama mmoja ni HIV+. Kuna mtoto wa shemeji yangu wife alimkuta anashika shika vidonda vya mwenzake ambaye inasemekana ni HIV+. Kwa mazingira kama haya watoto ni rahisi sana kuambukizwa HIV. Hili ni fundisho kuwa tusipende kuwadhania vibaya wenye HIV, wapo wengi wana HIV na hawakupata kwa njia ya uzinzi.
Nakupa scenario ya nyingine; Dada yangu ana ugonjwa wa sukari, kwa hiyo hujipima sukari kila siku na kujichoma sindano. Siku moja katoto kangu kakasema nako kanataka kupima, akakachoma na kukapima. Binafsi hadi leo huwa sielewi dada alitumia sindano mpya kumchoma mwanangu au alitumia aliyotumia yeye kujichoma? Kwa mfano huu nadhani unaweza kuona ni kiasi gani watoto wetu wapo katika mazingira ya hatari wawapo nyumbani na hata shuleni.
Pole sana mkuu, mwenyezi MUNGU awape nguvu. HIV kaipata shule au hapo hapo nyumbani kwa watoto anaoshinda nao na most likely ni vitu vye ncha kali. Kama unatabia ya kuwapeleka wanao kwa kinyozi kunyoa, tafadhali hakikisha hawachongwi. Ktk kuchonga mara nyingi mashine zile huwa zinakata au kukwangua, imagine mashine imetoka kumnyoa mtu mwenye vidonda halafu ije imkwangue mwanao?